Katiba Mpya: Mimi ni CHADEMA lakini kwa hili nasema NO, tena Big No

Ofcoz, wasomi waliokuwa wanaunga mkono chadema wameona either wakae pembeni au waingie CCM tu.

Unakaa unapoteza muda kuwashauri Ila wataishia kukutukana sana na kukukosea heshima. Hakina mtu mwenye akili atakubali upuuzi wa namna hiyo.

Mbowe ameshauriwa awaonye vijana wake na ajitahidi kutafuta seminar za uongozi kwa vijana wake, itawajenga kwa sababu heshima haiuzwi na ukiwa na heshima na staha jamii itakuona tu na utaheshimika. Ila kwa Hawa wanaorusha matusi humu aisee inakatisha tamaa sana better ukae pembeni usubiri uteuzi wako uchume chako ule na wanao Hawa wanywa double kick waendelee kupagawa.
 
No wonder watu wengi waliacha kuchangia mada za JF kipindi cha Magu sababu ya wapuuzi waliokuwa wanamsapoti ilikuwa ni matusi tu kuitana beberu, mwizi nk.

Sasa Magu hayupo wameibuka CHADEMA wanajiona kama ndio wameshinda uchaguzi na unapata picha je wakipewa nchi si itakuwa shida?

Tunahitaji upinzani mpya kabisa.
 
Hivi una hoja ya kujibiwa? Hivi Mfano Kabudi aliyekuwa kwenye tume ya warioba, Jana katoa hoja? Hiyo hoja yake unaijibuje?

Kabudi hana hoja kabisa.ana maslahi binafsi so tumpuuze tu,halafu soma mada yangu vizuri mimi sijapinga katiba mpya bali nimeandika jinsi ambavyo haiwezi kufanikiwa na sababu zake
 
Ajenda sio katiba, ya ndani tunayajua,
Msidhani wameshiba, njaa inawasumbua,
Wote hawa maswahiba, msone waziba pua,
Katiba huo ni mwiba, katu huwezi fumua.




Sent from #Kitale # Kenya
 
Mkuu umenena vizuri, hata hivyo binafsi naamini katiba mpya ni muhimu sana ukizingatia ulichokieleza kwenye hoja zako.

Tatizo kwa viongozi wetu ni approach ya jambo hili, wanataka liwe la haraka sana huku wakisahau kuwa tulikuwa chini ya Magu ambapo sauti zetu zilikuwa ni za kugugumia tena chini ya vitanda kinyume chake kesi ya uhujumu uchumi na uhamiaji haramu ingekuhusu ama KUTWALIWA na wasiojulikana.Ila Rais Samia amekubali kukosolewa kuonesha kwamba yuko tofauti na mwendazake tumpongeze kwa hilo.

Cha kufanya, approach her with soft tongue na siyo kusababisha kila mtanzania ajue kwamba mwadai katiba mpya naamini ataelewa mdogomdogo.Mwenyekiti Mbowe naamini una namba za simu za Rais, call and ask her for appointment right?

Zaidi ya hapo akina Mdude wapunguze kauli za kutweza kwa Rais kwa sababu hata na yeye (SSH) anaweza kuturudisha tulikotoka (naomba isiwe hivyo) kwa kuzingatia yeye ana dola na ni sababu ya Mdude kushinda kesi yake.Tukumbuke chini ya Magu Mdude asingekuwa uraiani kwa sasa.

Mwisho, kwa kuzingatia tulikopitia 2015-2020 namuomba Rais aongoze nchi yetu kwa kuzingatia matakwa ya katiba na sheria tulizojiwekea.Pia asione shida kukutana na kujadili na viongozi wa vyama vya wachache kuhusu mustakabali wa nchi yetu.

HII NI NCHI YETU SOTE TUPENDANE.
 

Yaani mkuu nilichokigundua hawa watu hawasomi article nzima.ni wavivu wa kusoma kabisa na hata wakisoma basi hawawezi kutumia akili zao vizuri namna ya kudadavua kujua mtoa mada alikuwa na lengo gani.kuna muda hadi unashamed kwa mtindo huu hata tukishinda ccm haiwezi kutoa nchi.yaani matusi ndio kitu wanachojua
 

Ni kweli kabisa mkuu.then kipindi cha Magu watu wengi walikuwa waoga kuchangia kwa kuhofia mambo ya kutafutwa na kupotezwa kusikojulikana.kiukweli wanachama wengi wa chadema wa sasa sio critical thinkers kabisa.viongozi wana kazi ya kuwafunda wanachama sana
 

Watu kama wewe ndio huwa tuma sema mmekomaa kisiasa na sio hawa wengine ambao akisoma tu heading basi anakimbilia kucomment bila kusoma article nzima
 
Hata ikiwa wewe, yani mrithi wa mali unamuona ni mvuta mibangi na haeleweki utampa mali kweli? So atauza tu na atalewea hiyo pesa na kuwaacha ndugu zake bila kitu🤷
 
Kuna tatizo gani mtu akihama chama kuhama na ubunge wake?
Kama sera ya chama chake wakati anagombea ilikuwa kurejeshwa shule kwa watoto wa kike wanaopata mimba halafu baada ya ushindi chama chake kikabadilisha sera hiyo kuna tatizo gani akihama?
 
Upinzani mpya kabisa upo ACT
 
ukisema mbunge akifa aliyeshika nafasi ya pili ndiye awe mbunge hilo siyo sahihi hata kidigo.kwanza wataanza kuuwana kwa kulogana au kuwindana.Pili kinachoshida ni chama kwa maana ya sera nzuri kukubarika na watu na siyo mtu.ndiyo maana mdhamini wa mgombea ni chama au wanachama husika.
 
Kwani nini faida na harasa ya serikali 3 na zipi faida na harasa za serikali 2? Wenda kila upande ulikuwa unajaribu kujitengenezea mazingira ya upataji kiurahis ndio maana hawakuona vitu vingne zaid ya hilo.
Tulia andika vizuri mkuu,unakimbilia wapi?
 
Chadema hakuna wapumbavu kama wewe. Mtu akishakuwa mpumbavu automatically anakuwa TAGA. So usitufanye wajinga. Upumbavu huu kawaambie mataga wenzio
 
Wangebaki bungeni hiyo rasimu yenye vipengele vya mbunge kuhama na ubunge wake ingepita. Hakuna kitu mpinzani anaweza kukizuia bungeni kwa sababu ya uchache wao. Hivyo kususia walifanya jambo la maana.
Unataka kusema hata hii katiba mpya pia haitawezekana kwa sababu huenda wanao itaka ni wachache?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…