Katiba Mpya: Mimi ni CHADEMA lakini kwa hili nasema NO, tena Big No

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,449
Habari za usiku wanajukwaa. Ni muda mrefu sijachangia chochpte humu wala kuweka bandiko lolote humu zaidi tu ya kusoma mawazo yenu.

Naomba nieleweke kwamba mimi ni mfuasi mtiifu wa chadema na nitaendelea kukitii siku zote.na niweke wazi kwamba sijawahi kukihujumu chama wala sifikirii kufanya hivyo. Nije kwenye mada sasa. CHADEMA tunataka katiba mpya lakini kiukweli suala la katiba mpya haliwezekani.

Kwanini nasema haliwezekani? Kwasababu wakati wa kuitengeneza Rasimu ya pili ya warioba 2014 ili iwe the proposed constitution hawahawa viongozi wetu walikuwa ni wajumbe pale bungeni lakini walishindwa kuendelea kukaa pale bungeni na wenzao wengine kwa sababu tu ya suala la serikali mbili na serikali tatu. Wakabishana weeee hadi kufikia kuiambia serikali ilete hati ya muungano.

Ukiangalia hilo suala la muungano halikuwa na athari yoyote lakini wao wakasusa na kukimbia pale bungeni wakiongozwa na lipumba ambaye leo wanamuona sio mpinzani.ndani ya ile rasimu kuna mambo mengi ya muhimu sana wangeweza kuyapambania ambayo kama wangesusa kwa sababu ya hayo tungewaona ni mashujaa.

Mfano suala la Wabunge kuongoza miaka 10. Waziri na spika kutokuwa wabunge, matokeo ya raisi, wabunge na madiwani kuhojiwa mahakamani, tume huru ya uchaguzi, Mamlaka ya Rais kupunguzwa, mgombea binafsi, mbunge anapofariki basi aliyeshika nafasi ya pili wakati wa uchaguzi basi anakuwa mbunge na wananchi kuwawajibisha wabunge wavivu, mbunge akihama chama basi anahama na ubunge wake na sio mambo ya by election. Mengine nadhani kama ulibahatisha kuyaona kama ulisoma ile draft.

Sasa, ukiangalia kilichowafanya wakasusa ni kitu kidogo na kisicho na maana yoyote ile kwa wananchi.

Binafsi nahisi Rais Samia ameshagundua kwamba hata akisema mchakato urudi upya mambo yatakuwa ni yaleyale business as usual. Yaani CCM watataka serikali mbili huku CHADEMA wakitaka serikali tatu na mwisho hawataelewana na mchakato utakwama tena na hivyo kodi za wananchi zitakwenda bure Maana kumbuka walikuwa wanakula posho daily Tsh laki 3. Hivyo Rais sidhani kama atakubali huu mchakato urudiwe maana mambo yatajirudia ni yaleyale tu. Itakuwa ni uharibifu wa fedha..ni vizuri wang’ang’anie tu hii iliyopo ifanyiwe amendments baadhi ya vipengele lakini suala la katiba mpya hilo I’m sure halitafanikiwa.

Kitu kingine wanachohitaji viongozi wetu ni political rallies kuruhusiwa ni kweli hilo sio hisani bali ni takwa la kikatiba iliyopo lakini kuhusu hilo nadhani mheshimiwa Rais ashalitolea ufafanuzi tayari.kwamba tusubiri kwanza ajenge uchumi wawekezaji waje wakute nchi ikiwa tulivu haina labshalabsha zozote ndipo turudi majukwaani (angalau huyu katoa sababu zenye mashiko kidogo kuliko mwendazake).

Maana usisubiri hadi Raisi aongee direct kwamba “jamani utawala ulopita nilikuwa nikimshauri hiki na kile mwenzangu hakuwa akinisikiliza ndio Maana uchumi umeyumba”kwa sababu hakuna asiyejua kwamba Mzee alikuwa hashauriki.sasa Mama hawezi kuanza kumkandia na kuanza kujitetea.

Mimi nadhani tuwe watulivu tukisubiri huo uchumi unaojengwa then tukiona labda miaka miwili au mmoja unakata tunaweza kurudi kumkumbusha.lakini kwa style kama ya kuwapa vipaza watu kama mdude halafu kwa kauli kama zile kiukweli haipendezi na mwisho tutampa hasira Raisi asije akawa kama mwendazake tuanze kubambikiwa makesi na kufurushwa hata kwenye mikutano ya ndani.

Chadema chama langu waelewe tu upinzani upo ndani ya damu. Kumbuka Magufuli alipiga ban mikutano na kufunga wanasiasa na kununua wabunge na madiwani ila ilipofika wakati wa uchaguzi bado alisumbuka sana kuona nyomi la Chadema mwisho akapora uchaguzi kwa nguvu(nilisimamia uchaguzi so niliona ujinga uliofanyika) niwatakie siku njema na niwaase mfanye kazi kwa bidii na kama wewe ni mwanafunzi basi soma kwa bidiii.na msisahau kumuabudu mwenyezi Mungu.
 
Kumbe hata rasimu ya pili ya Warioba ilikuwa haifai.

Swala la mbunge kuhama chama na ubunge wake halifai. Hiyo rasimu ingepita nadhani kipindi kile cha hamahama cha wabunge wangeweza kuhama bila hata kununuliwa kwa bei kubwa, wangepozwa kwa hela kidogo tu ya mboga na kuhama chama.

So binafsi hiyo rasimu ya Warioba ilikuwa haifai pia, japo CHADEMA walisusia mchakato kwa hoja dhaifu ila kumbe subconciously walifanya la maana sana. Mambo gani ya mtu kuhama chama anahama na ubunge wake? Huko ni kuwasaliti wananchi. Wananchi walimpa ubunge kutokana na sera za chama chake hivyo anapohama chama anaenda kinyume na makubaliano ya wapiga kura wake.
 
Kwani nini faida na harasa ya serikali 3 na zipi faida na harasa za serikali 2? Wenda kila upande ulikuwa unajaribu kujitengenezea mazingira ya upataji kiurahis ndio maana hawakuona vitu vingne zaid ya hilo.
 
Mantiki ya andiko inakosa maana. Sioni umuhimu wa kuandika wewe ni CHADEMA au CCM.

Jenga hoja yako. Katiba tunayoongekea ni ya nchi. Siyo ya CCM wala CHADEMA. Kwa fikra zako unaamini kuwa CHADEMA wote wanataka katuba mpya, na CCM wote hawataki katiba mpya?

Wananchi walio wengi, webye vyama na wasio na vyama, wanataja katiba mpya. Hilo lilidhihirishwa kwa data, na tume ya Warioba. Kwa sasa, zaidi kinachogomba miongoni mwa wananchi, ni timing.
 
Ukiwa CHADEMA huwezi kupinga mpaka useme “mimi ni Chadema tena nakipenda chama” ndio unatoa Mawazo yako?
Anajihami kabla ya kuanza kushambuliwa na kuitwa mataga. Chadema wanaamini kwamba mtu yoyote mwenye mawazo tofauti na Mbowe ni msaliti au ni CCM, na yule anaekubaliana na mawazo au fikra za Mbowe ndio chadema kindaki ndaki hata kama mawazo au fikra hizo ni za kipuuzi inakubadi ukubaliane nazo tu ili kujinusuru na matusi. So usimshangae jamaa kujihami mapema japo najua na hiyo haitomsaidia kwa sababu tayar kimawazo kaishatofautiana na mwenyekiti.
 
Habari za usiku wanajukwaa.ni muda mrefu sijachangia chochpte humu wala kuweka bandiko lolote humu zaidi tu ya kusoma mawazo yenu.

Naomba nieleweke kwamba mimi ni mfuasi mtiifu wa chadema na nitaendelea kukitii siku zote.na niweke wazi kwamba sijawahi kukihujumu chama wala sifikirii kufanya hivyo.Nije kwenye mada sasa.chadema tunataka katiba mpya lakini kiukweli suala la katiba mpya haliwezekani...
Tupe andiko lako moja tu humu JF linaloonesha wewe ni CHADEMA.
 
Anajihami kabla ya kuanza kushambuliwa na kuitwa mataga. Chadema wanaamini kwamba mtu yoyote mwenye mawazo tofauti na Mbowe ni msaliti au ni CCM, na yule anaekubaliana na mawazo au fikra za Mbowe ndio chadema kindaki ndaki hata kama mawazo au fikra hizo ni za kipuuzi inakubadi ukubaliane nazo tu ili kujinusuru na matusi. So usimshangae jamaa kujihami mapema japo najua na hiyo haitomsaidia kwa sababu tayar kimawazo kaishatofautiana na mwenyekiti.

mkuu nimecheka sana.huo ndio ukweli wenyewe asante kwa kunisaidia.maana vyama vyetu ni vya ajabu sana.mtu akiwa na mawazo tofauti basi anaonekana sio mwenzao
 
Hayo ndio yalikuwa ya msingi sasa mkuu.walitakiwa wabaki wapambanie vitu kama hivyo
Ivi nyie kipindi hicho mlikuwa watoto? Chukua rasmu ya warioba ambayo ndio maoni ya wananchi halisi na chukua Katiba pendekezwa Soma between the lines utuambie hazifanani kwa kiasi gani na utuambie kilicho andikwa kwenye Katiba pendekezwa ni nini na walipata hizo baraka wapi? Ni wehu tu na waganga njaa wanaweza kukubali na kubaki bungeni kwa kilicho fanywa na bunge la katiba
 
Mimi ninakubaliana na wewe suala la katiba mpya ni la msingi sana kams alivyosema jaji Werema si la kupuuzwa jambo la muhimu hapa ni wakati gani mchakato uanze tena. Kabla ya hapo serikali iandae Roadmap kwa kushirikiana na makundi mengine ya kijamii. Tatu wapinzani na makundi mengine wasinganganie mambo yote ya rasimu ya katiba Warioba yakubaliwe kama yalivyo.

Wakumbuke Tume ya Warioba ilikusanya maoni ya wananchi kama yalivyo na kisha kupelekwa Bunge la Katiba kupitiwa na kupata baraka.

Na hapo ndipo wapinzani wafahamu kuwa kuna baadhi ya mambo yanayojenga msingi wa Taifa na ambayo yaliipasua bunge mfano Muundo wa serikali mbili.

Ninaamini iwapo mchakato utaanzishwa tena waelelewe kuwa hilo litaharibu tena mwafaka wa Katiba mpya. Wapinzani wawe strategic kwenye masuala nyeti kama haya yaliyoingizwa kwenye mapendekezo ya warioba iwapo itarejewa na wasikubali kususia kama walivyofanya awali wajue hawatapata katiba mpya. Waende na kanuni ya nipe nikupe.

Kuna suala lililofikiwa la kisheria la kupigia kura rasimu ya Sita je tupuuze? au inakuwaje? Au tuanze upya na rasimu ya Warioba au zote mbili?Kwa sasa wampe Rais muda pengine cha kumuomba ni time frame kwa tafakuri kwa vile kuna mkanganyiko mkubwa wa kuendeleza suala hili.

Mwisho wapinzani waache kuzificha ajenda zao binafsi kwenye mwavuli ya rasimu ya Warioba kuwa ni ya wananchi yaliyomo hayapaswi kuguswa watashindwa jumla.

Wakubali baadhi kuachwa kiporo kimkakati ili tupate kwanza katiba angalau mpya kwa kuanzia- step by step. Yako mengi tu mazito na yenye manufaa kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom