Katiba Mpya: Mimi ni CHADEMA lakini kwa hili nasema NO, tena Big No

Nashukuru kwa kuongeza nyama mkuu, lkn wasomi wengi kina Mabere Marando, prof Safari nk wameshakikimbia chama na waliobaki wameamua kukaa kando, baada ya kugundua kwamba viongozi wa juu kitaifa wameanza kuwatumia vijana walevi, wavuta bangi na vibaka kujenga hoja mfu mitandaoni na kukitetea chama kwa style ya matusi.
Ofcoz, wasomi waliokuwa wanaunga mkono chadema wameona either wakae pembeni au waingie CCM tu.

Unakaa unapoteza muda kuwashauri Ila wataishia kukutukana sana na kukukosea heshima. Hakina mtu mwenye akili atakubali upuuzi wa namna hiyo.

Mbowe ameshauriwa awaonye vijana wake na ajitahidi kutafuta seminar za uongozi kwa vijana wake, itawajenga kwa sababu heshima haiuzwi na ukiwa na heshima na staha jamii itakuona tu na utaheshimika. Ila kwa Hawa wanaorusha matusi humu aisee inakatisha tamaa sana better ukae pembeni usubiri uteuzi wako uchume chako ule na wanao Hawa wanywa double kick waendelee kupagawa.
 
No wonder watu wengi waliacha kuchangia mada za JF kipindi cha Magu sababu ya wapuuzi waliokuwa wanamsapoti ilikuwa ni matusi tu kuitana beberu, mwizi nk.

Sasa Magu hayupo wameibuka CHADEMA wanajiona kama ndio wameshinda uchaguzi na unapata picha je wakipewa nchi si itakuwa shida?

Tunahitaji upinzani mpya kabisa.
 
Hivi una hoja ya kujibiwa? Hivi Mfano Kabudi aliyekuwa kwenye tume ya warioba, Jana katoa hoja? Hiyo hoja yake unaijibuje?

Kabudi hana hoja kabisa.ana maslahi binafsi so tumpuuze tu,halafu soma mada yangu vizuri mimi sijapinga katiba mpya bali nimeandika jinsi ambavyo haiwezi kufanikiwa na sababu zake
 
Habari za usiku wanajukwaa. Ni muda mrefu sijachangia chochpte humu wala kuweka bandiko lolote humu zaidi tu ya kusoma mawazo yenu.

Naomba nieleweke kwamba mimi ni mfuasi mtiifu wa chadema na nitaendelea kukitii siku zote.na niweke wazi kwamba sijawahi kukihujumu chama wala sifikirii kufanya hivyo. Nije kwenye mada sasa. CHADEMA tunataka katiba mpya lakini kiukweli suala la katiba mpya haliwezekani.

Kwanini nasema haliwezekani? Kwasababu wakati wa kuitengeneza Rasimu ya pili ya warioba 2014 ili iwe the proposed constitution hawahawa viongozi wetu walikuwa ni wajumbe pale bungeni lakini walishindwa kuendelea kukaa pale bungeni na wenzao wengine kwa sababu tu ya suala la serikali mbili na serikali tatu. Wakabishana weeee hadi kufikia kuiambia serikali ilete hati ya muungano.

Ukiangalia hilo suala la muungano halikuwa na athari yoyote lakini wao wakasusa na kukimbia pale bungeni wakiongozwa na lipumba ambaye leo wanamuona sio mpinzani.ndani ya ile rasimu kuna mambo mengi ya muhimu sana wangeweza kuyapambania ambayo kama wangesusa kwa sababu ya hayo tungewaona ni mashujaa.

Mfano suala la Wabunge kuongoza miaka 10. Waziri na spika kutokuwa wabunge, matokeo ya raisi, wabunge na madiwani kuhojiwa mahakamani, tume huru ya uchaguzi, Mamlaka ya Rais kupunguzwa, mgombea binafsi, mbunge anapofariki basi aliyeshika nafasi ya pili wakati wa uchaguzi basi anakuwa mbunge na wananchi kuwawajibisha wabunge wavivu, mbunge akihama chama basi anahama na ubunge wake na sio mambo ya by election. Mengine nadhani kama ulibahatisha kuyaona kama ulisoma ile draft.

Sasa, ukiangalia kilichowafanya wakasusa ni kitu kidogo na kisicho na maana yoyote ile kwa wananchi.

Binafsi nahisi Rais Samia ameshagundua kwamba hata akisema mchakato urudi upya mambo yatakuwa ni yaleyale business as usual. Yaani CCM watataka serikali mbili huku CHADEMA wakitaka serikali tatu na mwisho hawataelewana na mchakato utakwama tena na hivyo kodi za wananchi zitakwenda bure Maana kumbuka walikuwa wanakula posho daily Tsh laki 3. Hivyo Rais sidhani kama atakubali huu mchakato urudiwe maana mambo yatajirudia ni yaleyale tu. Itakuwa ni uharibifu wa fedha..ni vizuri wang’ang’anie tu hii iliyopo ifanyiwe amendments baadhi ya vipengele lakini suala la katiba mpya hilo I’m sure halitafanikiwa.

Kitu kingine wanachohitaji viongozi wetu ni political rallies kuruhusiwa ni kweli hilo sio hisani bali ni takwa la kikatiba iliyopo lakini kuhusu hilo nadhani mheshimiwa Rais ashalitolea ufafanuzi tayari.kwamba tusubiri kwanza ajenge uchumi wawekezaji waje wakute nchi ikiwa tulivu haina labshalabsha zozote ndipo turudi majukwaani (angalau huyu katoa sababu zenye mashiko kidogo kuliko mwendazake).

Maana usisubiri hadi Raisi aongee direct kwamba “jamani utawala ulopita nilikuwa nikimshauri hiki na kile mwenzangu hakuwa akinisikiliza ndio Maana uchumi umeyumba”kwa sababu hakuna asiyejua kwamba Mzee alikuwa hashauriki.sasa Mama hawezi kuanza kumkandia na kuanza kujitetea.

Mimi nadhani tuwe watulivu tukisubiri huo uchumi unaojengwa then tukiona labda miaka miwili au mmoja unakata tunaweza kurudi kumkumbusha.lakini kwa style kama ya kuwapa vipaza watu kama mdude halafu kwa kauli kama zile kiukweli haipendezi na mwisho tutampa hasira Raisi asije akawa kama mwendazake tuanze kubambikiwa makesi na kufurushwa hata kwenye mikutano ya ndani.

Chadema chama langu waelewe tu upinzani upo ndani ya damu. Kumbuka Magufuli alipiga ban mikutano na kufunga wanasiasa na kununua wabunge na madiwani ila ilipofika wakati wa uchaguzi bado alisumbuka sana kuona nyomi la Chadema mwisho akapora uchaguzi kwa nguvu(nilisimamia uchaguzi so niliona ujinga uliofanyika) niwatakie siku njema na niwaase mfanye kazi kwa bidii na kama wewe ni mwanafunzi basi soma kwa bidiii.na msisahau kumuabudu mwenyezi Mungu.
Ajenda sio katiba, ya ndani tunayajua,
Msidhani wameshiba, njaa inawasumbua,
Wote hawa maswahiba, msone waziba pua,
Katiba huo ni mwiba, katu huwezi fumua.




Sent from #Kitale # Kenya
 
Mkuu umenena vizuri, hata hivyo binafsi naamini katiba mpya ni muhimu sana ukizingatia ulichokieleza kwenye hoja zako.

Tatizo kwa viongozi wetu ni approach ya jambo hili, wanataka liwe la haraka sana huku wakisahau kuwa tulikuwa chini ya Magu ambapo sauti zetu zilikuwa ni za kugugumia tena chini ya vitanda kinyume chake kesi ya uhujumu uchumi na uhamiaji haramu ingekuhusu ama KUTWALIWA na wasiojulikana.Ila Rais Samia amekubali kukosolewa kuonesha kwamba yuko tofauti na mwendazake tumpongeze kwa hilo.

Cha kufanya, approach her with soft tongue na siyo kusababisha kila mtanzania ajue kwamba mwadai katiba mpya naamini ataelewa mdogomdogo.Mwenyekiti Mbowe naamini una namba za simu za Rais, call and ask her for appointment right?

Zaidi ya hapo akina Mdude wapunguze kauli za kutweza kwa Rais kwa sababu hata na yeye (SSH) anaweza kuturudisha tulikotoka (naomba isiwe hivyo) kwa kuzingatia yeye ana dola na ni sababu ya Mdude kushinda kesi yake.Tukumbuke chini ya Magu Mdude asingekuwa uraiani kwa sasa.

Mwisho, kwa kuzingatia tulikopitia 2015-2020 namuomba Rais aongoze nchi yetu kwa kuzingatia matakwa ya katiba na sheria tulizojiwekea.Pia asione shida kukutana na kujadili na viongozi wa vyama vya wachache kuhusu mustakabali wa nchi yetu.

HII NI NCHI YETU SOTE TUPENDANE.
 
I beg to differ kidogo, CHADEMA wamewekeza kwa wasomi Ila wale ambao ni less privileged Wana hasira kama mama mjamzito aliyeachwa na mume.

Vijana fulani 18-30 wapo hapo na hao wanahussle na maisha so hawajui namna ya kutafuta fursa kwa kutumia akili na sio mihemko.

Sisi wakati tunamaliza chuo na akina John Mrema na Mnyika na wengine akina Msando na Zitto vijana walikuwa na critical thinking yani ilikuwa wakisimama Nkrumah Hall enzi Ile Mzee Mkapa alikuwa anapenda kuja kuongea na wanafunzi wa chuo kikuu, walikuwa wanampa challenges mpaka Rais anatoka jasho kwa maswali na mawazo yaliyoshiba tena kwa staha sio matusi tu. Pale ilikuwa akitaka kuja anajipanga haswa maana alikuwa anakuwa challenged zile strategy zake za kiuchumi watu walikuwa wanampa challenges na inafika wakati anakubali kubadili strategy Ila angalia vijana wa sasa wanaishia kutukana na hakuna hoja. Yani hoja ni matusi.

Wakiwatumia vizuri Hawa ndio wenye ushawishi mkubwa sana kwakuwa ndio nguvu kazi ya taifa. Ila vijana wa kundi hili wamejikuta wanaishia kutukana kila mtu anayeshauri wafanyaje ili wapate public support kwa siasa zao.

Haiingii akilini mtu mzima umekaa unawapa ushauri unashangaa kijana anatukana tu, halafu umetoa mawazo mazuri tu ambayo angeweza sio lazima kuyakubali lakini akashukuru kwa ushauri, but utashangaa lundo la matusi tu.

Kwa namna hiyo, hakuna middle class atakayeona hiki ni chama madhubuti, hii iliwakuta NCCR maana ndio walikuwa chama kikubwa zaidi Ila Leo kinaelekea kufa.

Isingekuwa mlengo wa siasa flani za Zitto ACT wangekuwa juu sana kwa sasa na ingekuwa ndio mwisho wa CHADEMA.

Ila waendelee kutukana hata ambao sio CCM tutaona tu.

Yaani mkuu nilichokigundua hawa watu hawasomi article nzima.ni wavivu wa kusoma kabisa na hata wakisoma basi hawawezi kutumia akili zao vizuri namna ya kudadavua kujua mtoa mada alikuwa na lengo gani.kuna muda hadi unashamed kwa mtindo huu hata tukishinda ccm haiwezi kutoa nchi.yaani matusi ndio kitu wanachojua
 
No wonder watu wengi waliacha kuchangia mada za JF kipindi cha Magu sababu ya wapuuzi waliokuwa wanamsapoti ilikuwa ni matusi tu kuitana beberu, mwizi nk.

Sasa Magu hayupo wameibuka CHADEMA wanajiona kama ndio wameshinda uchaguzi na unapata picha je wakipewa nchi si itakuwa shida?

Tunahitaji upinzani mpya kabisa.

Ni kweli kabisa mkuu.then kipindi cha Magu watu wengi walikuwa waoga kuchangia kwa kuhofia mambo ya kutafutwa na kupotezwa kusikojulikana.kiukweli wanachama wengi wa chadema wa sasa sio critical thinkers kabisa.viongozi wana kazi ya kuwafunda wanachama sana
 
Mkuu umenena vizuri, hata hivyo binafsi naamini katiba mpya ni muhimu sana ukizingatia ulichokieleza kwenye hoja zako.

Tatizo kwa viongozi wetu ni approach ya jambo hili, wanataka liwe la haraka sana huku wakisahau kuwa tulikuwa chini ya Magu ambapo sauti zetu zilikuwa ni za kugugumia tena chini ya vitanda kinyume chake kesi ya uhujumu uchumi na uhamiaji haramu ingekuhusu ama KUTWALIWA na wasiojulikana.Ila Rais Samia amekubali kukosolewa kuonesha kwamba yuko tofauti na mwendazake tumpongeze kwa hilo.

Cha kufanya, approach her with soft tongue na siyo kusababisha kila mtanzania ajue kwamba mwadai katiba mpya naamini ataelewa mdogomdogo.Mwenyekiti Mbowe naamini una namba za simu za Rais, call and ask her for appointment right?

Zaidi ya hapo akina Mdude wapunguze kauli za kutweza kwa Rais kwa sababu hata na yeye (SSH) anaweza kuturudisha tulikotoka (naomba isiwe hivyo) kwa kuzingatia yeye ana dola na ni sababu ya Mdude kushinda kesi yake.Tukumbuke chini ya Magu Mdude asingekuwa uraiani kwa sasa.

Mwisho, kwa kuzingatia tulikopitia 2015-2020 namuomba Rais aongoze nchi yetu kwa kuzingatia matakwa ya katiba na sheria tulizojiwekea.Pia asione shida kukutana na kujadili na viongozi wa vyama vya wachache kuhusu mustakabali wa nchi yetu.

HII NI NCHI YETU SOTE TUPENDANE.

Watu kama wewe ndio huwa tuma sema mmekomaa kisiasa na sio hawa wengine ambao akisoma tu heading basi anakimbilia kucomment bila kusoma article nzima
 
Yaani mkuu nilichokigundua hawa watu hawasomi article nzima.ni wavivu wa kusoma kabisa na hata wakisoma basi hawawezi kutumia akili zao vizuri namna ya kudadavua kujua mtoa mada alikuwa na lengo gani.kuna muda hadi unashamed kwa mtindo huu hata tukishinda ccm haiwezi kutoa nchi.yaani matusi ndio kitu wanachojua
Hata ikiwa wewe, yani mrithi wa mali unamuona ni mvuta mibangi na haeleweki utampa mali kweli? So atauza tu na atalewea hiyo pesa na kuwaacha ndugu zake bila kitu🤷
 
Kuna tatizo gani mtu akihama chama kuhama na ubunge wake?
Kama sera ya chama chake wakati anagombea ilikuwa kurejeshwa shule kwa watoto wa kike wanaopata mimba halafu baada ya ushindi chama chake kikabadilisha sera hiyo kuna tatizo gani akihama?
Kumbe hata rasimu ya pili ya Warioba ilikuwa haifai.

Swala la mbunge kuhama chama na ubunge wake halifai. Hiyo rasimu ingepita nadhani kipindi kile cha hamahama cha wabunge wangeweza kuhama bila hata kununuliwa kwa bei kubwa, wangepozwa kwa hela kidogo tu ya mboga na kuhama chama.

So binafsi hiyo rasimu ya Warioba ilikuwa haifai pia, japo CHADEMA walisusia mchakato kwa hoja dhaifu ila kumbe subconciously walifanya la maana sana. Mambo gani ya mtu kuhama chama anahama na ubunge wake? Huko ni kuwasaliti wananchi. Wananchi walimpa ubunge kutokana na sera za chama chake hivyo anapohama chama anaenda kinyume na makubaliano ya wapiga kura wake.
 
Upinzani mpya kabisa upo ACT
No wonder watu wengi waliacha kuchangia mada za JF kipindi cha Magu sababu ya wapuuzi waliokuwa wanamsapoti ilikuwa ni matusi tu kuitana beberu, mwizi nk.

Sasa Magu hayupo wameibuka CHADEMA wanajiona kama ndio wameshinda uchaguzi na unapata picha je wakipewa nchi si itakuwa shida?

Tunahitaji upinzani mpya kabisa.
 
ukisema mbunge akifa aliyeshika nafasi ya pili ndiye awe mbunge hilo siyo sahihi hata kidigo.kwanza wataanza kuuwana kwa kulogana au kuwindana.Pili kinachoshida ni chama kwa maana ya sera nzuri kukubarika na watu na siyo mtu.ndiyo maana mdhamini wa mgombea ni chama au wanachama husika.
 
Kwani nini faida na harasa ya serikali 3 na zipi faida na harasa za serikali 2? Wenda kila upande ulikuwa unajaribu kujitengenezea mazingira ya upataji kiurahis ndio maana hawakuona vitu vingne zaid ya hilo.
Tulia andika vizuri mkuu,unakimbilia wapi?
 
Bahati mbaya sana humu tunatumia fake ids.mwaka jana nilisimamia uchaguzi kiukweli kilichotokea ni ujinga yaani haukuwa uchaguzi ule japo chadema nao walifanya uzembe kiasi fulani.mkuu tuwe na tabia ya kukubali kutofautiana.nimekushangaa mtu kama wewe unareply comment ya mtu aliyetoa matusi badala ya hoja.huyo jamaa mimi nimempuuzia wala sijajibu coment yake hata moja ila wewe umemshangilia halafu sisi ndio makamanda wa jf dahbado sana hii safari Maana hakuna tofauti ya lumumba na bavicha
Chadema hakuna wapumbavu kama wewe. Mtu akishakuwa mpumbavu automatically anakuwa TAGA. So usitufanye wajinga. Upumbavu huu kawaambie mataga wenzio
 
Wangebaki bungeni hiyo rasimu yenye vipengele vya mbunge kuhama na ubunge wake ingepita. Hakuna kitu mpinzani anaweza kukizuia bungeni kwa sababu ya uchache wao. Hivyo kususia walifanya jambo la maana.
Unataka kusema hata hii katiba mpya pia haitawezekana kwa sababu huenda wanao itaka ni wachache?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom