kichwa kikubwa
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 2,275
- 1,698
Wanabodi,
Hii ni thread ya Swali,
Kati ya Wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali Yake, Na Wasifiaji?, Nani Wanamsaidia Zaidi Rais Magufuli na Serikali yake?. Je kwa Ukosoaji unaofanyika humu JF, Je sisi JF, Tunamsaidia Rais Magufuli na Serikali yake au tunamdhalilisha?. Je ukosoaji wetu wa JF, tunalisaidia Taifa au tunajidhalilisha?
Umetunga mtihahani halafu unaufanya wewe mwenyewe. Angalia majibu yako hapo chini.
.Na kundi kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Magufuli na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watakosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika sio kwa lengo la kubeza, bali kwa ukosoaji unaofanyika kwa nia njema ya kusaidia. Ukosoaji wa aina hii ndio unaomsaidia Rais Magufuli na serikali yake kuliko wale wanaomsifia.
Mtihani umeujibu wewe uliyetunga, ila hujaridhika na majibu yako kisha unakuja kutuuliza tena. Maswali chini.
Namalizia kwa hili swali la msingi
Kati ya Wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali Yake, Na Wasifiaji?, Nani Wanamsaidia Zaidi Rais Magufuli na Serikali Yake?. Jee kwa Ukosoaji Unaofanyika Humu JF, Je Sisi JF, Tunamsaidia Rais Magufuli na Serikali yake au Tunamdhalilisha?. Jee Ukosoaji wetu wa JF, Tunalisaidia Taifa au Tunajidhalilisha?.
Long Live JF,
Long Live Maxence Mello.
Mungu Ibariki JF.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali