Kati ya wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali yake, na wasifiaji nani wanamsaidia zaidi? Ijue nafasi ya JamiiForums

Wanabodi,

Hii ni thread ya Swali,
Kati ya Wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali Yake, Na Wasifiaji?, Nani Wanamsaidia Zaidi Rais Magufuli na Serikali yake?. Je kwa Ukosoaji unaofanyika humu JF, Je sisi JF, Tunamsaidia Rais Magufuli na Serikali yake au tunamdhalilisha?. Je ukosoaji wetu wa JF, tunalisaidia Taifa au tunajidhalilisha?

Umetunga mtihahani halafu unaufanya wewe mwenyewe. Angalia majibu yako hapo chini.

.Na kundi kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Magufuli na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watakosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika sio kwa lengo la kubeza, bali kwa ukosoaji unaofanyika kwa nia njema ya kusaidia. Ukosoaji wa aina hii ndio unaomsaidia Rais Magufuli na serikali yake kuliko wale wanaomsifia.

Mtihani umeujibu wewe uliyetunga, ila hujaridhika na majibu yako kisha unakuja kutuuliza tena. Maswali chini.

Namalizia kwa hili swali la msingi
Kati ya Wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali Yake, Na Wasifiaji?, Nani Wanamsaidia Zaidi Rais Magufuli na Serikali Yake?. Jee kwa Ukosoaji Unaofanyika Humu JF, Je Sisi JF, Tunamsaidia Rais Magufuli na Serikali yake au Tunamdhalilisha?. Jee Ukosoaji wetu wa JF, Tunalisaidia Taifa au Tunajidhalilisha?.

Long Live JF,
Long Live Maxence Mello.
Mungu Ibariki JF.
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Mimi Binafsi naamini kuwa Rais Magufuli ni mtu anayependa sifa/ kusifiwa sana. Hii ni tabia yake. Mtu yeyote mwenye tabia hii hafai kusifiwa hata kidogo.

Ukimsifu haumsaidii kwa kuwa atataka uendelee kumsifu hata kama sifa zitaisha. Mara nyingine tumemshuhudia JPM akisema uongo hadharani kabisa ili kutafuta sifa na pia akasaini sheria ya takwimu ili afanikishe malengo yake ya kutafuta sifa.

Kwa heshima na taadhima naomba turejee kauli zifuatazo:

Mimi Binafsi naamini kuwa Rais Magufuli ni mtu anayependa sifa/kusifiwa sana. Hii ni tabia yake. Mtu yeyote mwenye tabia hii hafai kusifiwa hata kidogo. Ukimsifu haumsaidii kwa kuwa atataka uendelee kumsifu hata kama sifa zitaisha. Mara nyingine tumemshuhudia JPM akisema uongo hadharani kabisa ili kutafuta sifa na pia akasaini sheria ya takwimu ili afanikishe malengo yake ya kutafuta sifa.

Kwa heshima na taadhima naomba turejee kauli zifuatazo:

1. Uchumi unakua kwa asilimia 6.7 na haijawahi kutokea toka tupate uhuru...(JK alituacha na asilimia 7)
2. Tunawadai ACACIA TSH Trilioni 400....(tukaishia kuahidiwa Bilioni 700)
3. ACACIA hawajasajiliwa na BRELLA....(Ila tukawaacha waendelee kuchimba madini huku tukisubiri kuongea na baba yao BARICK)
4. Nilipoingia madarakani sukari ilikuwa ikiuzwa TSH 5,000 lakini sasa imeshuka.
5. Eti kuna wengine wanasema sijui KINGEREZA wakati nimesoma na UINGEREZA kwenyewe nimekaa (lakini neno pekee tunalolisikia ni CATARYST)
6. Ndani ya miaka minne ya utawala wangu viwanda 4,000 vimejengwa


Haya ni baadhi tu ya anayoyasema mwenyewe ili kutafuta sifa/ kusifiwa, sasa wapo wale ambao vya kusifia vimeisha inabidi wajiongeze ili kumfurahisha mkulu. utasikia:
"Muheshimiwa Rais nakushukuru kwa mshahara mzuri unaonipa kwa kuwa sasa napata hata mshahara unaoniwezesha kukaa hata na kamchepuko kidogo" au "Inabidi hata Mungu amshukuru Magufuli"


itaendelea...
 
Wote ni muhimu kwa Rais. Wanaosifia wanamtia moyo, wanaokosoa wanamrekebisha, kwa mtazamo wangu ukosoaji mzuri uwe na alternative solution.
 
Rais hapaswi kusifiwa hata angelihamisha ziwa Nyasa akalipika kwao Chato!

Kwa kawaida mtu anapotekeleza wajibu wake wa msingi tena alioahidi kuutekeleza kwa kiapo unamsifia ili iweje.

Ila anaposhindwa kutekeleza wajibu wake lazima akosolewe wanamkososa Rais ndio wamemfikisha hapo alipo!

Inashangaza inapotokea hata yeye mwenyewe Rais anajipongeza its absolutely nosense!
 
Wote wanasaidia kwa sababu wanawaakilisha mawazo ya kijamii. Katika jamii kuna mitazamo tofauti bila kujali anayejadiliwa anafanya vibaya au vizuri.
Uko sahihi kabisa ni kama kwenye ngalawa kuna mlengo wa kulia na mlengo wa kushoto kwa pamoja unaisaidia ngalawa kuelea vyema baharini
 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    24.2 KB · Views: 2
Pascal Mayalla,

RAIS kazungukwa na wanafiki ambao , wanapenda kumshauri anachotaka kusikia. Ukiwa na mshauri lazima awe tayari hata mara nyingine "kugombana" na bosi kwa kumshauri jambo, na bosi akilala akiamka anamuita na kumshukuru, ukiona mshauri kila siku mnacheka tu hamtofautiani na mambo yanaharibika hafai mshauri anatakiwa kuwa na mawazo ya ziada kwa boss wake na sio tu kupigia mstari mawazo ya boss.
 
Pascal Mayalla,

JF Iachwe kuwa JF,
Ni uwanja huru, andika, niandike, By the way nikiwa kama mkosoaji wa aina ya tatu. natamani idadi yetu iongezeke.
Pro wapinzani hupnga kila kitu, hata vile vya kupongezwa, hata vile vya kusikitika kama taifa kwa pamoja, wao hufurahia

Praise team ,wanaojiita mtandaoni MATAGA, Nao hupongeza kila kitu, hata yale ambayo yangehitaji kuboreshwa.

Daima ntasema kweli, uongo kwangu mwiko, hii ni ahadi ya MwanaTANU ambayo ntaishika daima, katika harakati hizi za ujenzi wa taifa letu, Nachagua kukosoa pale panapoitaji kukosoa na kusifia pale panapoitaji sifa. akili zangu sishikiwi na mtu.
 
Siasa ni uongo , vyama vya siasa ni viongo, wanasiasa waongo, wanaokosoa bila kutoa ushauri nini kifanyike waongo pia kiufupi muacheni Mzee wa Kazi apige kazi ukosoe usifie haiongezi wala kupunguza kitu, siasa ni jambo nadharia tu msilitilie maanani kiviile mwacheni Mzee Baba afanye yake.

Tena kwa hii speed ningewashauri wadau wa siasa mumuuongezee walau tumiaka 10 iwe 15. Asije akaingia mwingine ambaye ni 'kibaraka wa wazungu' akaturudisha Ukolonini, Uncle Magu jembe hataki mazoea na hao wazunguruku wanyonyaji wakubwa wanaowafadhili akina nanii
 
Kukosolewa kwa namna yoyote ile ukiwa na uwezo wakufanya tathimini lazima upate jambo la msingi la kukusaidia.

Tatizo, ni pale unapopenda nyimbo za sifa na kuabudu ikitokea umekosolewa hata kama kuna jambo chanya bado utaona unatukanwa, unaonewa n.k.

Tuendelee tu ivyo hivyo yaani hamna namna kwa makundi yote ila walio na jukumu tutachambua mazuri na baadaye tutayatumia kujenga nchi.
 
Mie ni mfuatiliaji mzuri sana kwa wote wanaosifia na wanaopinga. Kitu kikubwa hapa ni ushabiki wa kupitiliza mfano kutekwa na kupotea kwa watu na wengine kuumizwa au kuuwawa. Hapa wanaokosoa wako right bila chenga. Hakuna binadamu asiyetaka kuishi au kuwa na uhakika na kesho yake. Katiba yetu inatamka kuwa kila mtu anastahili kuishi na ni haki yake kufanya hivyo.

Kundi lingine kama watakosoa juhudi zozote za serikali kwa kubeza bila kutoa mbadala basi nao wanakosea sana. Kinachohitajika ni kukosoa na kuweka wazo mbadala ya namna gani shughuli hiyo ifanyike ukitaja na vyanzo vya mapato ya kukamilisha mradi. Kwa kifupi kama utasifia lakini Tina ikaonekana utakuwa sahihi lakini siyo kila tamko wewe udifie tu bila kujadili
 
Pascal Mayalla,

Hao wa tatu ulio waelezea wanao kosoa kwa constructive criticism hao ndio wajenzi wa Nchi, na ndio msaada wa maana kwa Rais. Sikuona bora lolote ulilosema ukijua wazi wasifiaji wakisifia hawana baya lolote ata kama wakisifia wakakesha haina ubaya ili mradi MSIFIWA ana ufahamu na anatambua uimara wa constructive criticism upo na utamsaidia kunyoosha pale atakapo pitiwa.

So kuna faida gani ya kuwa na BORA KUKOSOA na sio KUKOSOA BORA why to have them,wana msaada gani zaidi ya kuwa KICHAKA cha MAADUI kujifichia ili kutimiza ajenda zake kwa nia OVU. ili daraja la watu wema [constructive criticism] waonekane nao MANCHE GA NYANZA HAWAFAI ATA KWA KULUMANGIA sababu ya Ushenzi wa Wakosoaji ovyo aka Utumbo.

Ukuryani, Umasaini na Usukumani ukiwa na mdomo mdomo Wakurya wanakupta jina utaitwa RWAMBE na Wasukuma WILOMOLOMO manake mbele za Wanaume wenzio HUFAI ATA KUSHIKA FIMBO za Wanaume na ni dharau kubwa sana kwa wewe kusimama na kuongea na Wanaume wenzio.

So sikuona sababu ya Wewe Mayala kutaka kutuaminisha kuwa Maradaraja hayo Mawili wasifiaji kupitiliza [Utoto- Na ngoma ya Watoto AIKESHI] na Constructive Crtisim -[Matual People-Who deserve Mijadala ya kujenga] wanaweza kulinganishwa dhidi ya Wapingaji [Haiters -ambao ni tabia za Kishriki -Watu wasio Mtakiwa Mema Binadamu yoyote yule ata kama ni wewe mwenyewe Pasco] ,

Saikolojia na na mfumo wa Kiroho zinamtaka binadamu kukaaa mbali na ROHO HASI [NEGATIVITY] ambazo UKIZI ISHI LAZIMA ZIKUPELEKE KUZIMU WHY HOST THEM.

Kwani kuaccomodate Roho za WASHANGILIA KILA JAMBO KWENYE MAISHA YAKO KUNA UBAYA GANI [POSITIVITY} wakati ukijua ndani ya akili yako kiwango cha SIFA unachostahiki kupokea na zingine kuziacha zikipita kama Makelele ya Watoto kwa ''Baba huyooo karudi toka kazini zina athari gani na uchovu wa mihangaiko ya kutwa nzima kazini'',

So usilinganishe WAKOSOAJI OVYO [MAGUGU KONDENI] na madaraja yale mawili ya Wakosaji wajenzi na Washangiliaji dhidI ya Wakosaji [Maadui] wasiostahiki kupewa nafasi, japo kusikilizwa na wanapaswa kufutwa ili wapishe njia njema zistawi, kwani magugu uondolewa ili mmea Upate Kustwai vyema Kondeni
 
Pascal Mayalla,

Taifa lolote duniani haliwezi kuendelea kwa wananchi wake kumsifia Raisi tu, lazima wananchi wajenge utamaduni wa kukataa yale ambayo wanaona hayawezi kulipeleka taifa mbele.

sasa kwa mfano ubaya wa baadhi ya wananchi wa kawaida na viongozi waliopo kwenye system wanasifia hata yale ya hovyo. Huo unageuka kuwa ni unafiki na kujipendekeza na mwisho ni kifo.Yaani ni kifo kwa wananchi lakini pia ni kifo wa taifa.Kwa hiyo ni afya kumkososa raisi.
 
Nadhani na Bilashaka jibu la Swali lako liko hapa.
Na kundi kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao rais magufuli na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watakosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika sio kwa lengo la kubeza, bali kwa ukosoaji unaofanyika kwa nia njema ya kusaidia. Ukosoaji wa aina hii ndio unaomsaidia rais Magufuli na serikali yake kuliko wale wanaomsifia.
Yeye mwenyewe huwasema watu kwa vijembe, matusi na lugha za kubeza, kebehi, Kwahiyo na ukosoaji wake utakuwa wa lugha hiyo hiyo anayoitumia yeye.
 

Jee yeye naye angependa tumkosoe kwa namna hii?
Mbona hata yeye kesha fanya makosa mengine makubwa sana kuliko huyu anayemtukana hadharani? Tena mtu family man na mwenye umri unaorandana naye?
Unadhani kama huyo mhandisi ni member wa JF akipata nafasi ya kukosoa ataremba maneno kweli?
Tumfikishie ujumbe rais kuwa lugha zake ndizo zinazaa mashambulizi kwake yasiyo na staha.
Hana haki yeyote mbinguni au duniani kuwatweza wengine kwa sababu yeye ni rais. Kwanza mwananchi ndiye bosi wake amlipaye mshahara na marupurupu, kujimwambafai hakuta msaidia

Very perfect 100%.
 
Back
Top Bottom