Kati ya wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali yake, na wasifiaji nani wanamsaidia zaidi? Ijue nafasi ya JamiiForums

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Hii ni thread ya Swali,
Kati ya wakosoaji wa Rais Magufuli na serikali yake na wasifiaji, nani wanamsaidia zaidi Rais Magufuli na serikali yake?. Kwa ukosoaji unaofanyika humu JF, Je sisi JF, tunamsaidia Rais Magufuli na serikali yake au tunamdhalilisha? Je, ukosoaji wetu wa JF, tunalisaidia taifa letu Tanzania au tunamdhalilisha rais wetu, tunalidhalilisha taifa letu na hivyo kujidhalilisha wenyewe?.

Kwa kadri siku zinavyokwenda, Watanzania tunaanza kugawanyika katika kambi mbili kuu, kambi ya kusifia na kambi ya kupondea.

Kambi ya kusifia, wao kazi yao ni kusifia tuu, hata kukifanyika mabaya au maovu kiasi gani, wao watasifu tuu!. Mfano kama wa tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kupotea kwa watu kama kina Ben Saanane, Azory Gwanda, vifo vya kikatili kama cha kamanda Alfosi Mawazo au mambo tu kufanyika ndivyo sivyo, wao kazi yao ni kusifu tu kila kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wao ni kusifu tuu.

Kambi ya kuponda na kukosoa tuu, nao kazi yao ni kuponda, kupinga na kukashifu kila kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake, hata kiwe kizuri vipi, wao wataponda, watakosoa, watakashifu, wata tukana , watadhalilisha na kubagaza, hata ndege, walipinga ila wanazipanda, SGR wanapinga, Stiglers Gorge wanapinga, lolote litakalofanywa na Rais Magufuli na serikali yake, hata liwe zuri vipi, wao watalikashifu na kulipinga.

Na kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Magufuli na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watamkosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema, sio kwa lengo la kubeza, kukashifu, kudhalilisha au kubagaza, bali ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema kwa lengo la kusaidia, kutoa angalizo, kurekebisha na kutoa ushauri wa namna bora zaidi ya kufanya mambo. Ukosoaji wa aina hii, ni ukosoaji mzuri, na ndio unaomsaidia Rais Magufuli na serikali yake kuliko wale wanaomsifia tuu.

Katika makundi ya wasifiaji, wana mtazamo kuwa kumsifia tu Rais Magufuli na serikali yake ndio the right thing to do, na wote wanaokosoa jambo lolote ni wasaliti.

Hakuna yeyote anayeamini kuwa Rais Magufuli na Serikali yake ni malaika, they are perfect, hakuna kitu chochote wanaweza kukosea, hivyo kustahili nyimbo za sifa tu na mapambio tuu. Kwenye makundi yote mawili ya wasifiaji tu na wakosoaji tu, miongoni mwao kuna vichaa wengi tuu, ila kiukweli vichaa wengine hawajijui kuwa ni vichaa ila watu wenye akili, ukimsikiliza tu mtu anavyoongea, utambaini kwa urahisi kuwa huyo ni kichaa.

Mtandao huu wa JamiiForums, ni user generated content forum, kila mtu yuko huru kutoa mawazo yake yoyote kwa kuchangia jambo lolote kwa uhuru. Miongoni mwa wachangiaji hawa, wamo pia wasifiaji, wakosoaji na wale makini wanaosifu panapostahili sifa, na kukosoa kwenye makosa.

Leo nimemsiliza kichaa mmoja maarufu sana kwa kusifia tu. Naamini hata CCM na serikali wenyewe, wenye akili zao, wanajua kuwa Rais Magufuli na serikali yake sio malaika, na kuna makosa wanayaona, lakini hawawezi kuyasema, hivyo hawa wasifiaji tuu wa kusifia kila kitu as if ni malaika, watu wote wenye akili timamu wanawajua ni vichaa.

Leo huyo kichaa nimemsikia akimshutumu mmiliki wa Jamii Forums, Mkuu Maxence Melo kuwa yuko kwenye mtandao wa watu wanaolipwa kumdhoofisha Rais Magufuli na serikali yake. Kichaa huyo anaamini watu wote tunaomkosoa Rais Magufuli na serikali yake humu jf, tunatumwa na Max!.

Nakuomba Mkuu Maxence, mpuuze kichaa huyo, si wengi wanaojua kuwa mtandao wa JamiiForums unaisaidia sana serikali, vichaa hawa na wajinga kama hawa, wanadhani Rais Magufuli anapenda sana kusifiwa sifa za kijinga!. Wanadhani anapenda kusifiwa tuu, na kuwa hapendi kukosolewa. Mimi nafahamu Rais Magufuli ni mtu anayependa challenge ili to prove them wrong na nilimsikia mwenyewe akisema anapenda kukosolewa anapenda challenge.

Na katika wakosoaji pia nako kuna vichaa, kwa kudhani kuwa Rais Magufuli na Serikali yake hawapendi kukosolewa, hivyo madhila yoyote yanayowakuta wakosoaji wote akiwemo Tundu Lissu na kupotea kwa mkosoaji wetu mkuu humu JF, Ben Saanane, wanakuhusisha na serikali. Huu nao ni ukichaa tuu!. Huwezi kumtuhumu mtu kwa kumnyooshea kidole bila ushahidi. Hakuna ubishi ni kweli Ben Saanane ametoweka, hakuna ajuaye ni nini kilichomtokea, pia ni kweli Tundu Lissu ameshambuliwa, ila waliopanga na kufanya shambulio hilo ni watu wasiojulikana, mtu yeyote anayemnyooshea kidole mtu mwingine yeyote na kumhusianisha na matukio haya bila ushahidi naye ni kichaa tu. Ingekuwa ni serikali imehusika kwenye shambulio la Lissu kwasababu ya ukosoaji wake, then mtu wa kwanza kushughulikiwa angekuwa ni Zitto, kwasababu Zitto ni mkosoaji mkubwa kuliko hata Tundu Lissu.

Sisi wana JF, tuendelee kuwa wana mtandao responsible, kwanza tuendelee kusimama na JF Management yote, kwa kuiunga mkono JF kuruhusu free flow of information and opinions. Hakuna mtandao mwingine wowote wa kiTanzania ambao watu wako free kujimwaga watakavyo kama JF. Kwa sisi baadhi yetu, tuliojaaliwa kauwezo kadogo ka kusoma in between the lines, na wakati viongozi wakihutubia, kuwasikiliza sio tu kile wanachosema, bali pia kusikia vile ambavyo hawajavisema ambavyo ndio huwa the motive behind ya hivyo wanavyosema, kiukweli JF inamsaidia sana Rais Magufuli na Serikali yake kuliko hata hao vichaa wanaoshinda kutwa kucha wakisifu kwa nyimbo za shangwe na mapambio, au wale wakosoaji waliofilisika, wasio ona zuri lolote. Sisi tuendelee na ukosoaji wetu, very objectively kama nilivyo shauri hapa
Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli - JamiiForums

Hii dhana ya kumuona kila mkosoaji kama ni msaliti is wrong notion, tena kuna uwezekano kuna wakosoaji wanaomkosoa Rais Magufuli na serikali yake, kwa sababu wanampenda, kama vile baba anavyomrudi mwanae aliyekosea, kwa sababu anampenda anataka asikosee tena, vivyo hivyo, kuna baadhi ya wakosoaji wa Rais Magufuli na serikali yake, sio wanamkosoa ili kumbeza kwasababu hawampendi, bali wanamkosoa kwa sababu wanampenda, wanatamani awe perfect, tunatamani kuona kuwa not only he does the right thing at the right time, but he got to do things right.

Mfano kufuatia lile swali langu kwa Rais Magufuli pale Ikulu, kuna mambo ya ajabu ambayo nayapitia, nikielezwa ni kwa mujibu wa maelekezo kutoka juu, hao watekelezaji hawasemi ni maelekezo kutoka juu kwa nani, bali just suggesting ni maelekezo ya kutoka juu kule kileleni!. To be honest, I don't believe kuwa hayo ni maelekezo kutoka huko ninakoelezwa, na kuna siku ikitokea, hata nikikutana naye popote hata kwa bahati mbaya tuu, baada tuu ya kumsalimia, swali langu la kwanza, nitamuuliza kama kweli ni yeye!.

Namalizia kwa hili swali la msingi: Kati ya wakosoaji wa Rais Magufuli na serikali yake, na wasifiaji - nani wanamsaidia zaidi Rais Magufuli na serikali yake?. Je, kwa ukosoaji unaofanyika humu JF, Je sisi JF, tunamsaidia Rais Magufuli na serikali yake au tunamdhalilisha?. Jee ukosoaji wetu wa JF, tunalisaidia taifa letu Tanzania au tunajidhalilisha?.

Long Live JF,
Long Live Maxence Melo.
Mungu Ibariki JF.
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea kuhusu ukosoaji na usifiaji
Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli - JamiiForums
 
Nadhani na Bilashaka jibu la Swali lako liko hapa.

Na kundi kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Magufuli na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watakosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika sio kwa lengo la kubeza, bali kwa ukosoaji unaofanyika kwa nia njema ya kusaidia.

Ukosoaji wa aina hii ndio unaomsaidia Rais Magufuli na serikali yake kuliko wale wanaomsifia.
 
Wote wanahoja za msingi na zenye mashiko kulingana na jinsi wanavyoyachambua mambo katika angle wanayoamini wako sahihi.

Kwa upande wangu nakujibu katika vipengee viwili.

1) Wanaomkosoa Rais wanamsaidia kuyaona mapungufu na kuyarekebisha inapobidi kwa sabab rais siyo malaika,,,,kundi hili linakosea pale linapokosoa kila kitu hata pale panapostahili pongezi,kwa kufanya hivi kukosoa kwao kunachukuliwa kama destructive na wanakuwa kama hawamsaidii.

2) Wanaomsifia rais wanamsaidia rais kumwongezea ari na morali ya kufanya makubwa zaidi maana anaona kuwa anachokifanya kinakuwa recognized na jamii. Kundi hili linakosea pale linapo sifia kila kitu hata pale panapohitajika ukosoaji na kushauri,kwa kufanya hivi Rais anaweza akapotoshwa na kundi hili na sifa zao kwa rais zikawa destructive!

huu ni wangu mtazamo
 
Swali lako ni gumu kulijibu bila ya kufikiria katiba yetu na utekelezaji wa yaliyomo ndani yake. Je ni kweli kuwa yaliyomo yanatekelezwa kulingana na viapo vitolewavyo wakati wa kupanda ngazi au kupitia mlango mwingine?,au yanatekelezwa kulingana na Hali iliyopo?.
 
Binafsi napenda changamoto pale ninapofanya jambo hata kama ni zuri lakini wakatokea mtu kuni challenge huwa ninajitahidi kufanya vizuri zaidi ya vile nilivofanya mwanzo.

Lakini kusifiwa kuna bwetesha mno unaweza ukajiona wewe ni mmoja uliyezaliwa sahihi hakuna mwingine kumbe sivyo.
 
Nadhani inahitajika ukosoaji wa kistaarabu na kujenga na usifiaji wa panapostahili

Jee yeye naye angependa tumkosoe kwa namna hii?

Mbona hata yeye keshafanya makosa mengine makubwa sana kuliko huyu anayemtukana hadharani? Tena mtu familia na mwenye umri unaorandana naye?

Unadhani kama huyo mhandisi ni member wa JF akipata nafasi ya kukosoa ataremba maneno kweli?
Tumfikishie ujumbe Rais kuwa lugha zake ndizo zinazaa mashambulizi kwake yasiyo na staha.

Hana haki yeyote mbinguni au duniani kuwatweza wengine kwa sababu yeye ni Rais. Kwanza mwananchi ndiye bosi wake amlipaye mshahara na marupurupu, kujimwambafai hakuta msaidia
 
kundi la kwanza ni CCM kindakindaki ambao hawamsaiidii sana

kundi la pili ni CHADEMA yaani wenyewe hadi mafisadi wanawatetea kwamba Rais alivyowaambia warudishe pesa zile anawaonea yaani wamechanganyikiwa ni kama kakundi flani kakihuni ujinga ujinga wanautetea na kukosoa juhudi zooote za Magufuli.

kundi la tatu linatakiwa likuzwe na litakua tu taratibu maana Rais anafanya kazi kubwa.
 
Kundi la kusifia tu ni baya sana. Wanawafanya hata ninyi mnaosifu kwa nyakati na kushauri kwa nyakati kuonekana hamfai. Kusifia tu nayo sio vizuri kabisa na haijengi.

Ila nilichoelewa kwa Rais Magufuli na kikosi chake kwa ujumla ni kwamba wametuelewa tunaobaki katikati. Wanawajua wanaosifia tu vizuri sana na hata wale wanaokosoa wanawajua vizuri sana.

Timu sifia tuu inamchukia kila anayeshauri au kosoa lakini Rais Magufuli na timu yake hupamabana na wahujumu sio wakososoaji.
 
Serikali sikivu inapokosolewa pale inapofanya makosa hujirekebisha.Watu kukosoa serikali ndio picha kamili ya namna utendaji wa serikali unavyofanyika. Kama kuna makosa kweli ni vyema kukosoa ila kwa lugha ya staha.

Gazeti la mwanahalisi na sakata la richmond ulikuwa ukosoaji na ulipuaji wa madili ambao nafikiri kwa maoni yangu serikali ilikuwa sikivu. Sasa hii awamu ya tano hakuna ukosoaji ,ni matusi tu na chuki hasa kwa wale vibaraka wa wapiga dili na mafisadi ambao wamedhibitiwa.

Awamu hii ya tano ni kweli kuna mapungufu ambayo kuyaona kwa macho ni ngumu sana. Kwani hata wateule wa serikali hii hawalali usingizi maana wanajua anytime watatumbuliwa. Mfano utamkosoa vipi rais ambaye amefanya ziara mtwara na kusaidia wakulima waliokuwa wameibiwa bil 1.2! Na hapo kuna wateule waliliwa vichwa!

Serikali sikivu inapokosolewa pale inapofanya makosa hujirekebisha.Watu kukosoa serikali ndio picha kamili ya namna utendaji wa serikali unavyofanyika. Kama kuna makosa kweli ni vyema kukosoa ila kwa lugha ya staha. Gazeti la mwanahalisi na sakata la richmond ulikuwa ukosoaji na ulipuaji wa madili ambao nafikiri kwa maoni yangu serikali ilikuwa sikivu.

Sasa hii awamu ya tano hakuna ukosoaji ,ni matusi tu na chuki hasa kwa wale vibaraka wa wapiga dili na mafisadi ambao wamedhibitiwa.

Awamu hii ya tano ni kweli kuna mapungufu ambayo kuyaona kwa macho ni ngumu sana. Kwani hata wateule wa serikali hii hawalali usingizi maana wanajua anytime watatumbuliwa. Mfano utamkosoa vipi rais ambaye amefanya ziara mtwara na kusaidia wakulima waliokuwa wameibiwa bil 1.2! Na hapo kuna wateule waliliwa vichwa!
 
Kwa sababu Rais Magufuli anafanya vizuri na tunayafurahia. Kumkosoa ni kumvunja moyo na kumsifia ni kumpa moyo na nguvu ya kukaza.

Forward ever, backward never.
 
Back
Top Bottom