Kati ya Rais Samia na Hayati Magufuli nani aliona vizuri kuhusu idadi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM?

JPM alikuwa na akili ya kijanja janja sana. Aligundua ni vigumu sana kuwadanganya/ kuteka akili ya watu wengi kwa pamoja, alichokifanya kwa sababu alikuwa na agenda zake za Siri ili aweze kupitisha maamuzi yake kwenye halmashauri kuu ni rahisi sana kufanikiwa ukiwa na wajumbe 150 kuliko wakiwa 300. Ni rahisi kuhonga wajumbe 80 kati ya 150 kuliko wajumbe 160 kati ya 300. Tena baada ya kuwapunguza akaanza kuchagua watu wake mf mtoto wa pinda, makongoro Nyerere nk. JPM alikuwa na mikakati yake tushukuru tu Mungu ni wa huruma
 
JPM alikuwa na akili ya kijanja janja sana. Aligundua ni vigumu sana kuwadanganya/ kuteka akili ya watu wengi kwa pamoja, alichokifanya kwa sababu alikuwa na agenda zake za Siri ili aweze kupitisha maamuzi yake kwenye halmashauri kuu ni rahisi sana kufanikiwa ukiwa na wajumbe 150 kuliko wakiwa 300. Ni rahisi kuhonga wajumbe 80 kati ya 150 kuliko wajumbe 160 kati ya 300. Tena baada ya kuwapunguza akaanza kuchagua watu wake mf mtoto wa pinda, makongoro Nyerere nk. JPM alikuwa na mikakati yake tushukuru tu Mungu ni wa huruma
Kwamba alikuwa anahonga wajumbe?
Dah.
 
Huyo daktari aliyetokewa yeye alikuwa na integrity yeyote? Mbona unaangalia upande moja tu wa coin? Kwa ubinafsi ule wa wafanyakazi wa sekta ya umma, uzembe, uvivu na ubadhirifu uliochagizwa na rushwa kila mahali, ungerekebishaje hizo attitudes? Ofcourse kuna ma sycophants ambao wali take advantage, but in general dhamira yake ilikuwa imelenga nini? Watanzania tujifunze kuwa critical na open minded...Sisi siyo honest wala hatupo objective tunapenda sana mob psychology!
Reading your articles between the lines. Thumb up.
 
Johnny Sack post: 44681522, member: 410952"]Itabidi tukaongee na Gwajima amfufue[/QUOTE]Johnny Sack wewe ni sehemu ya wapumbavu mliotemwa na JPM!

Muda mwingi mnaupoteza kugombana na Marehemu!

Kitu hamjui ni kwamba lolote litaweza tokea siku si nyingi ni suala la Muda tu!
 
Mimi moja wao...I was proud of chama changu, hivi sasa nakiteteaje kwa mfano?

Infact before, sikuwahi kuwa mwanachama wa chama cha siasa japo nimezaliwa na waasisi wa chama. I did join the party actively because of the expectations I had, ya maendeleo ya kweli ya nchi na watu wake na siyo yale ya mwanzo ya kisiasa na yasiyo na economic values wala hayakuleta spcial gains zenye impacts kwa jamii pana zaidi ya individuals tena wenyewe wakiwa wanabadilika kila wanapoachia nafasi nakubakiwa kuwa fukara hata miradi yao kufa; hata sasa bado sijakata tamaa but will never bless what is not right, my integrity goes first before anything else!

As for me sincerely, JPM aliniathiri sana in person kwa maendeleo ya carrier yangu kupitia wapambe wake ambao wali take advantage ya kuaminiwa (few ambao to me are just sycophants) na pia kuvuruga biashara zangu nyingi tu; yet I had nothing in person na nilikubali kwa moyo moja bila kisasi wala grudge kwakua alionyesha kubeba national agenda, ambayo ni muhimu kuliko my personal gains....Sasa hivi gharama yote ile naibebaje kisha eti nisi simame kuusema ukweli?

Mungu na asimame kuona dhamira yangu, I wont compromise my integrity a minute for material gains!
Na kwasababu hiyo ninaujasiri sana wa kumwendea Mungu na kumwambia look here God, do what is unexpected and righteous, naye atajibu hakika, very sure indeed, this wont last long kabla Mungu hajatu reward tuliobeba gharama za kweli kwa taifa letu!
Watu mnaoandika KISWANGLISH huwa ninawadharau mno. Mnatia kinyaa
 
Hayati Magu alipunguza wajumbe wa NEC wa CCM, Samia kaongeza idadi, nani aliyeona kwa jicho la makengeza kati ya hawa Wenyeviti wawili?
Mama anaenda na upepo tu hana umakini wala haangalii tija. Yeye ni wale ulaji ndio lengo. Magufuli aliondoa watendaji au tuseme waajiriwa ccm wasihudhurie vikao na kupiga kura ila wawakilishi tu ndio wahudhurie vikao na kuweza kupiga kura.
Sasa makatibu wanafuata nini kwenye vikao na kupiga kura. Hio demokrasia gani ya chama.
 
Hoja iliyoko mbele yetu nani alitazama kea jicho la makengeza kati ya Mwenyekiti aliyepita na huyu aliyepo sasa!!

Magu alipunguza idadi ya wajumbe wa NEC,kupunguza kule kulikuwa na tija kwa chama?

Mama kaongeza idadi ya wajumbe tena bdani ya kipindi kifupi toka kupunguzwa kwa wajumbe na mtangulizi wake,je ni kigezo gani Mwenyekiti wa sasa amekitumia kuongeza tena idadi ya wajumbe ukizingatia yeye alikuwa mjumbe wa sekretarieti kuu,hakuona hilo kipindi mwenzake anapunguza na kushauri?

Maamuzi ya chama yanajengwa na utashi wa Mwenyekiti aliyeko au yanajengwa kutokana na falsafa, itikadi na misingi ya chama?

Ikiwa kuna wajumbe wa sekretarieti kuu ambao kazi yao kubwa ni kusukuma mambo yaende mbele yenye tija hawakuliona hili linaweza kuzua kizungumkuti?
 
CCM ya JPM ilikuwa imara kwa sababu watu wallipenda toka moyoni. Heshima ilikuwepo kwa wenye nacho na wasionacho.
Ukitaka kujua waulize wauza kadi na wauza sare za chama.

Wakati wa JP watu walijivunia chama.
Waliunda umoja bila shuruti!
Lakini sasa hivi kimekuwa ni chama cha mammbuzi, yanakula tu kwa urefu wa kamba!
Punguani mkuwa wakati wa chizi hakuna wa kumshika shurubu chizi
 
CCM ya JPM ilikuwa imara kwa sababu watu wallipenda toka moyoni. Heshima ilikuwepo kwa wenye nacho na wasionacho.
Ukitaka kujua waulize wauza kadi na wauza sare za chama.

Wakati wa JP watu walijivunia chama.
Waliunda umoja bila shuruti!
Lakini sasa hivi kimekuwa ni chama cha mammbuzi, yanakula tu kwa urefu wa kamba!
Watu waliipenda kutoka moyoni? Kwa kipimo kipi hicho? Hawa watu ndio mbuzi sads hivi au waliletwa wengine?
 
Hayati Magu alipunguza wajumbe wa NEC wa CCM, Samia kaongeza idadi, nani aliyeona kwa jicho la makengeza kati ya hawa Wenyeviti wawili?
Ninachojua CCM ni chama ambacho kiko flexible kujihuisha kutokana na nyakati ndiyo maana kiko strong. Ni lazima ukubali mabadiliko na uende na nyakati vinginevyo mabadiliko yatakusomba. #JPM was right kwa alichokifanya kwa analysis ya wakati wake anachukua Chama na Mhe. Rais Dk. Samia yuko sahihi, kwa wakati na analysis ya kitaasisi katika kuendesha Chama. 🙏🙏🙏
 
Huu
Enzi za Dkt Magufuli wajumbe wa NEC na Kamati kuu walikuwa bata balaa. Sasa hivi Rais Samia hawamuelewi kabisa. Kibaya kabisa kibaya kuna vijanaa vinamzunguka Rais Samia
Kuwafanyia mbaya wajumbe ndiyo Maana JK alitoa ile kauli. Kwa ufupi Rais Samia 2025 kama ana chake basi ni 25% maana wajumbe wapo mguu pande wakisubiri muda wowote kumtosa. Na siku akitoswa aisee Rais Samia atatukanwa zaidi kuliko kiongozi yeyote kuwahi kutokea. Anachopaswa kufanya sasa ni kuzia matusi kwa Dkt Magufuli na vijembe, yaani kadri anavyoendeleza vijembe ndiyo anazidi kujiumbua. Huwezi kusema eti wajumbe walikuwa hawashirikishwi kutembelea miradi hahahaha so shameful sijui nani kamuandalia hiyo hotuba na waliomfanyia hivyo ni hao wabaya wake wakiwa na lengo la kumfanya aonekane Rais Samia hajui.
Uzushi na uzandiki mpelekee mamako
 
Hayati Magu alipunguza wajumbe wa NEC wa CCM, Samia kaongeza idadi, nani aliyeona kwa jicho la makengeza kati ya hawa Wenyeviti wawili?
Vijana wa sasa hivi hawajui CCM imetoka wapi, iko wapi na inaelekea wapi.

Kwa wasiyoijua CCM wanahoji na kupima uwezo wa uongozi wa Marais katika Awamu mbalimbali. Lakini ukweli hawaujui au kama wanaujua wanaifunika kwa sababu zao binafsi.

CCM imepita katika nyakati mbalimbali na muhimu kulingana na kundi linaloongoza chama, kama ifuatavyo:

1) Kabla ya Uhuru: Viongozi wa TAA (1929) ikiongozwa na Ali Saidi, ikabadilishwa kuwa TANU (1954) na Nyerere, walishughulikia Uhuru na kufanikiwa. Hawa viongozi, chini ya Mwl Nyerere, Kawawa nk walisukumwa na uzalendo.

2) Baada ya Uhuru: Viongozi walioanzisha TANU, walijenga jumuiya za chama ikiwemo ya Vijana (TANU Youth League) kwa madhumuni ya kuandaa viongozi wa kesho. Hawa vijana walipelekwa Jeshini kupata mafunzo ya uongozi na ushupavu. Baadhi yao ni Marehemu Moses Nnauye, Yusuf Makamba, Kinana, na wengine walifuatia km Jakaya kikwete.

Kundi hili la vijana lilitaka utawala wa Dola baada ya Mwl Nyerere, lakini kwa Awamu 2 (ya Mwinyi na Mkapa) halikufanikiwa. Hivyo lilibaki na kinyongo. Hili kundi dhamira yake kuu ni kujitajirisha kupitia "political power". Ni kundi la watu linaloamini siasa ndio mtaji mkuu wa mafanikio.

Kwa sababu hiyo, juhudi zikafanyika hadi likafanikiwa kumweka JMK kutawala ambapo pia kulikuwa na makubaliano ya siri ya kurithishana. Haikutokea hivyo kwa kuwa uchu wao wa madaraka ulimwezesha Magufuli kupata fursa ya kuwa Rais.

Matarajio ya kundi hilo la vijana wa TANU kuendelea kutawala Chama na Serikali kulizimwa kwenye Utawala wa Magufuli. Hivyo zikafanyika kila njama kumwondoa Magufuli. Hivyo basi, kuondoka kwa Magufuli, hatima ya Chama imerudi mikononi mwa waliokuwa Vijana wa TANU. Kwa kuwa tayari umri wao umeenda, wanachokifanya ni kuhakikisha watoto wao wako madarakani, katika chama na Serikali.

Kujibu swali la mada kuu, ni dhahiri Chama na Serikali, kwa sasa, uongozi wake uko kwa Watoto wa Vijana wa TANU. Vijana wa CCM wamewekwa kando kwa sababu hawana msingi kichama.
 
CCM ilikuwa imara zaidi wakati wa JPM, siyo sasa.
Watu tuliipenda CCM kwa moyo thabiti kabisa kwani JPM alituheshimisha hata sisi wa kipato cha chini.
Saa hizi MAFISI, MAKENGE NA MANYONYA DAMU YOTE YAMEJAA CCM.
 
Samia amerudi enzi ya Kikwete, Magufuli aliondoka enzi ya Kikwete.

CCM ya Kikwete na CCM ya Magufuli ipi ilikuwa imara zaidi?? Jibu unalo mwenyewe.
Uimara wa ccm unaupimaje wewe?
CCM ya Magufuli wabunge na madiwani walinunuliwa kwa kilichoitwa kuunga Mkono juhudi za chizi. kisha wakarudishwa kwenye nafasi zao na majimbo yao kwa gharama zilizotokana na kodi zetu. Ya Kikwete wala Mkapa haikufanya upuuzi huu. huo umara ukowapi?
CCM ya Kikwete watu waliruhusiwa Kufanya Siasa na walijibiwa na wanasiasa. CCM ya Magufuli shughuli za siasa kwa vyama vya upinzani zilipigwa marufuku. Ndiyo uimara unaouzungumzia?
CCM ya Magufuli iliiba na kuharibu kabisa Uchaguzi ule wa serikali za mitaa na ule uchaguzi mkuu.
NI MTU MPUMBAVU TU AWEZAYE KUSEMA CCM YA MAGUFULI/NYAPARA ILIKUWA IMARA
LABDA UIMARA WA KUPIGA WATU RISASI
 
Kwa mantiki hii chama kimeacha falsafa na itikadi yake,wahuni wameachiwa kukipeleka chama wanapotaka ilimradi familia zao zinakuwa sehemu ya kuendeleza uhuni huo.

Ideology ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi imeondoka na kukifanya chama kuwa chama - dola. Malengo ya kuwa chama cha siasa hayapo ndiyo maana CCM ya sasa inaogopa hoja,kwa kuwa imekuwa mufilisi wa fikra
 
Back
Top Bottom