Lipumba yuko sahihi kwa kiasi kikubwa. Katika kipindi chake cha kwanza, Raisi Mkapa aliongoza nchi vizuri sana; mara nyingi nimekuwa nachukulia kuwa huenda alikuwa anaogopa kufanya madudu asije kukemewa na Nyerere. Baada ya Nyerere kufariki, ndipo Mkapa akawa kichwa ngumu katika kipindi chake cha pili na kuanza kuboronga. Mabaya yote yaliyofanbywa na Mkapa ambayo ndiyo wananchi wengi wanakumbuka ni yale aliyofanya katika kipindi cha pili; alipoanza kuwa mjasiliamali basi akauza nchi yote kwa mabavu hata pale ambapo ilikuwa ni wazi kabisa kuwa uamuzi wake haukuwa na faida kwa nchi; alichjali zaidi ni msalahi yake binafsi kuliko yale ya taifa. Unfortunately, historria huwa inajua kuadhibu watu wa aina hiyo kwa sababu huwa inakumbuka zaidi mabaya yao kuliko mema yao.
Kwa upande wa Kikwete, siyo kweli kuwa hajafanya mazuri. Kikwete amefanya mambo kadhaa yanayoheshimika kimataifa; kwa mfano alikuwa msitari wa mbele katika kutatua migogoro ya kisiasa ya Kenya na Zimbabwe, amesaidia sana kujenga amani katika eneo la maziwa makubwa, na mengineyo mengi katika bara la Afrika. Utawala wake pia umeimarisha urafiki na nchi za nje hasa Marekani ambapo siku hizi tu watalii wengi wa Kimarekani wanakwenda Tanzania kuliko Kenya, kinyume na zamani. Ameiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa mwenyeji wa mkutano wa WEF ambao umekuwa ukifanyikia Davos miaka yote. Kwa hiyo ana mambo mazuri aliyofanya ingawa yote hayo hayamsaidii raia wa kawaida aliyepiga kura na kumpangisha Kikwte kwenye lile kasri la Magogoni.