Kati ya Mkapa na Kikwete nani zaidi?

Kwa bado ni blabla mi nitamkumbuka kwa kutoa nafasi kwa wapinzani kuichallenge serikari yaani wapinzani wanaonekana wanaweza kabsa
 
kumbuka hizo sekondari zimejengwa kwa fedha ya msamaha wa madeni kazi ambayo Mkapa alipambana kuomba wafadhili wafute deni la Tanzania na nidhami aliyoionyesha ya kuanza kulipa madeni

Mkapa ndio aliye ruhusu Jengo la chimwaga liwe chuo kikuu cha Dodoma akaweka na budget ya ujenzi kwa kuanzia

Pamoja na mkapa kuwa mkali wa magazeti hakuwa mwoga wa yanayosemwa kama alivyo kikwete ndio maana akina Rai waliweza kuishi wakaishia baada ya wanamtandao kuingia madarakani

Kilimo kimekufa kabisa na hakuna bidii ya kutumia hata soko la agoa kwa bidhaa za kilimo miaka mitano imeshaisha kwa sababu hatuna hata jina la kumuita kwa mkampa kulikuwa na Ukapa,Ukaja ubinafsishaji,utandawazi mwisho ubabe ,sasa Twambie kwa Kikwete tuna majina gani zaidi ya vurugu zaakina dowans,richmond,epa nk.

Angekuwepo mpaka sasa angekuwa amejiwekea mgodi wa mchuchuma na kiwira lakini barabara ya dar -kigoma pia ingekuwa inazungumzwa
Ukisema hayo hata miradi ya daraja la Rufiji na barabara ya Dar-Mza hakuianza Mkapa.
 
Jamani muwe waangalifu vitu mnavyo-compare! mcheza ngoma za mdundiko na msoma novo wapi na wapi??
 
miaka 5 ya kwanza ya mkapa ilikuwa shughuli ukapa ulishamiri, challenge anazopata kikwete angekuwa mkapa angeshakufa na bp au angeua watu, kina mwanakijiji hatungekuwa nao leo...,
 
Mkapa tutamkumbuka kwa yafuatayo
1 Daraja la Mkapa la kuunganisha mikoa ya kusini
2 Uwanja wa michezo wa kisasa
3 Maji ya ziwa victoria kwenda Shinyanga na Kahama
4 Mabarabara mengi yalijengwa kwa kiwango cha rami
5 Uchumi uliimalika
6 Mfumuko wa bei ulipungua
7 Kodi ziliongezeka

Mh. Kikwete katika miaka 4 tumkumbuke kwa yapi? Orozesha hapa!!!

Misguided discussion; ones legacy has nothing to do with real people's needs derived development.

Chunga, avoid to be parrot drum-beating support to misguided leadership actions that have cost lives of your own people-wajomba, shangazi, kaka dada, mama, baba na jamaa wengine.
Si-Mkapa, Si-Kikwete both suffering poor leadership vision.
Ref. HDR 1998-2007
 
Tutamkumbuka Mkapa kwa yafuatayo:
1. Aliunda mipango ya kukuza uchumi: Mkukuta, Mkurabita, TASAF, SACCOS, n.k
2. Alisimamia matumizi ya serikali: Alibana matumizi ya hovyo ya serikali
3. Alituliza mfumuko wa bei
4. Alirudisha heshima ya Taifa (kwa wahisani na mataifa ya nje)
5. Alirudisha uwajibikaji: Mmesahau wasomi kukaa Salamander kwa kuwa ofisi hazilipi kabla hajaingia madarakani?
6. Aliachia uhuru wa habari: Japokuwa si kwa kiwango cha sasa. Ila ilikuwa bora kuliko miaka iliyotangulia
7. Alijenga miundombinu ya kudumu: Barabara za Dar na mikoani zilijengwa kwa kiwango cha lami
8. Alirudisha uwekezaji wa ndani na nje: Kwa mfano tu, Mmesahau kuwa Pugu Road (sasa Nyerere road) viwanda vyote vilishageuka magofu? Ukuaji wa kipato cha mfanyakazi wa kawaida. Nakumbuka awali wafanyakazi walikuwa wakilipwa peanuts. Kipindi chake hali ikiwa nafuu zaidi.
9. Aliinyanyua nchi kutoka kwenye uchumi uliokuwa umeporomoka kabisa. Nchi haikuwa ikikopesheka wala kuthaminika kwa namna yoyote
10. Alijenga shule nyingi: Awali ilionekana kuwa kujenga shule ni suala lisilowezekana kwa serikali. Shule nyingi zilikuwa hoi kabla hajashika madaraka
11. Alikarabati hospitali kubwa zote nchini. Muhimbili ilikuwa ikitisha siku za nyuma
12. Alipunguza migomo ya waalimu, madaktari na watumishi wengine. Kuna wakati hata jeshi lilibidi kutumia nguvu kupata mahitaji yake kabla hajashika madaraka
13. na mengineyo

Kikwete tutamkumbuka kwa yafuatayo:
1. Amekuza uhuru wa maoni: Watu wako huru kutoa maoni yao kuliko kipindi chochote cha uhuru wa nchi hii
2. Amepunguza urasimu kwa kiasi kidogo
3. Sheria imepunguzwa makali bila kubadilishwa kimaandishi
4. Vigogo wamepunguziwa uwezo wa kujiamulia watakavyo
5. Ametumia ziara zake nje ya nchi kuitangaza nchi zaidi
6. Amekuza michezo hasa soccer kwa kiasi kikubwa. Jitihada bado hazitoshi.
 
Watu wanaogopa sana kumsifia Mkapa hata pale alipofanya mambo mazuri kabisa,....tuache hizo haki yake tumpe kama tunavyo mpa lawama.

Mazuri ya Jk;
-Kutabasamu mfululizo...inasaidia sana kwa mwenye njaa kujisikia angalau anachekelewa!

n.k

...ha ha :D

wewe kweli ni mzizi wa mbuyu! :)
 
I think i would agree with Gelange, Kikwete will be building his LEGACY in the next 5years which i think will be the best and to use them as security for CCM to continue rulling after 2015.

To be honest Kikwete anakubalika sana nje ya nchi which means the next 5years he will mainly concentrate on local problems.
 
What is anakubalika nje? It is because of his weaknesses. No foreign element likes anybody but their interest. "Anakubalika" kwa sababu anawezesha kuimarisha na kusimamia maslahi yao, period!
Uliishawahi kujiuliza uhusiano baina ya James Synclair (the mining right baloon) na Kikwete inaigharimu Tanzania kiasi na kwa namna gani?
 
Mkapa tutamkumbuka kwa yafuatayo
1 Daraja la Mkapa la kuunganisha mikoa ya kusini
2 Uwanja wa michezo wa kisasa
3 Maji ya ziwa victoria kwenda Shinyanga na Kahama

Je alijenga hayo kwa pesa zake binafsi? Nadhani alikuwa anatimiza wajibu wake kama kiongozi, na kama sikosei, alikuwa akilipwa mshahara!

4 Mabarabara mengi yalijengwa kwa kiwango cha rami

Je ulifundishwa shule na kusomeshwa kiswahili wakati wa mkapa? Hiyo inaitwa LAMI!
Comment ni kama hapo juu, kuanzia 1 hadi 3.

5 Uchumi uliimalika
Nahisi una maana: ULIIMARIKA!

Je, umetumia vigezo gani!
Ninavyofahamu mimi ni kuwa uchumi ulianza kuimarika tangu pale Mzee Ruksa alipochukua madaraka, baada ya kuzorota sana miaka ya mwisho ya utawala wa anayelazimishiwa u "saint" (wakati huenda mwenyewe hakuutaka! 1985 Tanzania ilikuwa almost bankrupt! (Details IMF, WB, UN data)
Uchumi huo uliendelea kukua na unaendelea kukua (above 5% annually) hadi sasa chini ya Kikwete, ukitoa "credit crunch" iliyoanza muda si mrefu.

6 Mfumuko wa bei ulipungua
7 Kodi ziliongezeka
Kuongezeka kodi kwa wananchi ni sifa kwa mkapa!?! Labda sijakuelewa na jaribu kutumia lugha nyingine ambayo unahisi ni nyepesi kwako ili ueleweke!Mh.

Kikwete katika miaka 4 tumkumbuke kwa yapi? Orozesha hapa!!!
Inabidi iwe Orodhesha

Kwa uchache tu:
1. Kwani sasa hivi barabara hazijengwi?
2. Kwani sasa hivi kodi hazikusanywi?
3. Kwani sasa hivi hakuna miradi yoyote ya maendeleo au ni jazba ya chuki kwa JK?
Mjadala utakuwa na mantiki pale JK atakapokuwa amemaliza awamu zake 2. Na hata kama atakuwa hajaleta maendeleo kama mkapa, (kwa mfano mgodi wa kiwira!), hakudai kwenye kampeni ya uchaguzi kuwa atashindana na
mkapa kwa kuleta maendeleo zaidi ya yale aliyoyafanya mkapa!

siku njema!
 
kumbuka hizo sekondari zimejengwa kwa fedha ya msamaha wa madeni kazi ambayo Mkapa alipambana kuomba wafadhili wafute deni la Tanzania na nidhami aliyoionyesha ya kuanza kulipa madeni

Mkapa ndio aliye ruhusu Jengo la chimwaga liwe chuo kikuu cha Dodoma akaweka na budget ya ujenzi kwa kuanzia

Pamoja na mkapa kuwa mkali wa magazeti hakuwa mwoga wa yanayosemwa kama alivyo kikwete ndio maana akina Rai waliweza kuishi wakaishia baada ya wanamtandao kuingia madarakani

Kilimo kimekufa kabisa na hakuna bidii ya kutumia hata soko la agoa kwa bidhaa za kilimo miaka mitano imeshaisha kwa sababu hatuna hata jina la kumuita kwa mkampa kulikuwa na Ukapa,Ukaja ubinafsishaji,utandawazi mwisho ubabe ,sasa Twambie kwa Kikwete tuna majina gani zaidi ya vurugu zaakina dowans,richmond,epa nk.

Angekuwepo mpaka sasa angekuwa amejiwekea mgodi wa mchuchuma na kiwira lakini barabara ya dar -kigoma pia ingekuwa inazungumzwa

Credit zingine zinatolewa bila kuzingatia kwamba miradi mingi mikubwa ya nchi huwa ni mwendelezo wa mipango iliyokuwepo, mingine tokea awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere.

Msamaha wa madeni, aliyelipigia kelele sana suala hilo alikuwa Mwalimu Nyerere tangu alipokuwa Rais na baada ya kustaafu alipokuwa anaongoza Tume ya Kusini. Mwalimu alipiga kelele na kugombana na viongozi wa World Bank, IMF na hata viongozi wa nchi kama Marekani na zingine za Kibepari kuhusu suala la madeni. Mkapa alikuwa akiendeleza tu sauti ya Mwalimu.

Miradi ya barabara pia nayo ilikuwa ni mipango iliyokuwepo tangu awamu ya kwanza na Rais Mwinyi anastahili pongezi kwa kuwa naye alianza utekelezaji wa baadhi ya miradi kama vile barabara.

Naweza kukubali kwamba Mkapa alisaidia kuiondoa ile 'ruksa' iliyokuwepo wakati wa Mwinyi. Lakini, aliboronga kwenye zoezi la ubinafsishaji kwa kuuza NBC bila sababu za msingi. Pia aliboronga sana alipoingia tamaa ya kutaka kutajirika. Sasa hivi ni wazi anaona soni kuwaangalia Watanzania usoni kwa sababu ya mambo aliyoyafanya kwa manufaa yake na majumba yasiyo na sababu aliyoyajenga akiwa Ikulu kwa kutumia fedha za walipa kodi.

Aibu nyingine ni pale alipoonyesha wazi udhaifu wake. Pamoja na elimu yote aliyokuwanayo na kuwa kiongozi katika wizara ya Mambo ya Nje kwa muda mrefu alishindwa kuhilimili vishindo vya kukosolewa na marafiki zake walioonekana kuwa na mtazamo tofauti ya wake. Sakata la Jenerali Ulimwengu kuvuliwa uraia ni doa jeusi kwa upande wa Mkapa.

Ubabe wake usio na sababu katika kipindi cha uongozi wake Mkapa umemshushia hadhi.
 
Zaidi nitamkumbuka kwa maagizo yake ambayo hayatekelezwi na wasaidizi wake na yeye kukaa kimya mfano Elimu: Aliagiza wanaosomea udaktari na Ualimu wapate mkopo 100%, Haikufanyika[/QUOTE]
 
Huko nyuma nshawahi kunukuu na ninarudia nukuu hiyo:'ALL POLITICAL CAREERS ENDS UP IN FAILURE'. Anayebisha achunguze historia na atuonyeshe mwanasiasa MMOJA tu aliyefanikiwa.
 
Mimi nadhani JK amerithi matatizo na anaangalia aanzie wapi kuyafumua. Alianzia na plate chafu kabisa ambapo ni vigumu kuendeleza ya kwake katika hali hii.
 
Boramaisha said:
Msamaha wa madeni, aliyelipigia kelele sana suala hilo alikuwa Mwalimu Nyerere tangu alipokuwa Rais na baada ya kustaafu alipokuwa anaongoza Tume ya Kusini. Mwalimu alipiga kelele na kugombana na viongozi wa World Bank, IMF na hata viongozi wa nchi kama Marekani na zingine za Kibepari kuhusu suala la madeni. Mkapa alikuwa akiendeleza tu sauti ya Mwalimu.

Miradi ya barabara pia nayo ilikuwa ni mipango iliyokuwepo tangu awamu ya kwanza na Rais Mwinyi anastahili pongezi kwa kuwa naye alianza utekelezaji wa baadhi ya miradi kama vile barabara.

Boramaisha,

..wakati Mwinyi anaondoka madarakani Tanzania haikuwa na mahusiano mazuri na WB na IMF.

..juhudi za Mkapa na serikali yake ndiyo ziliwezesha kurejesha mahusiano hayo na Tanzania ku-qualify kuingia katika mpango wa HIPC.

..pesa zinazotokana na HIPC ndiyo zinasaidia mipango mikubwa kama MKUKUTA, MKURABITA, na ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu.

..Uganda wali-qualify kuingia HIPC wakati Tanzania tunaongozwa na Raisi Mwinyi. binafsi naamini kama Mwinyi angekuwa na nidhamu na asingeharibu mahusiano yake na IMF/WB basi Tanzania ingeingia kwenye HIPC miaka ya 90.

..nadhani kila Raisi anawajibika kuja na mambo mapya bila kuathiri yale mazuri yaliyoachwa na waliomtangulia.

NB:

..nilitegemea Kikwete atafanya mambo makubwa kuliko Mwinyi na Mkapa. Kikwete amepokea nchi ikiwa na hali nzuri KIUCHUMI kuliko hao wawili waliomtangulia.
 
Huko nyuma nshawahi kunukuu na ninarudia nukuu hiyo:'ALL POLITICAL CAREERS ENDS UP IN FAILURE'. Anayebisha achunguze historia na atuonyeshe mwanasiasa MMOJA tu aliyefanikiwa.

This is more general than the word general itself. Success is a relative concept and everyone especially politicians (I mean real politicians) has their own objectives therefore to say that every politician in history has been a failure is utterly and completely wrong. Infact I think that in any career one is bound to have some successes and some failures. The question is which side is to be the majority that is all.

K out.
 
Safari nyingi za nje

Kupendwa na Marekani (kumbuka ndiye Rais wa Kwanza wa Africa kumtembelea Obama Ikulu ya Merekani; kumbuka mambo ya Sullivan etc)

Kuwashitaki kina Mramba kwa ufisadi lakini kuwakataza kina Mengi wasiwataje mafisadi maana kufanya hivyo ni kuwagawa watanzania
 
Boramaisha,

..wakati Mwinyi anaondoka madarakani Tanzania haikuwa na mahusiano mazuri na WB na IMF.

..juhudi za Mkapa na serikali yake ndiyo ziliwezesha kurejesha mahusiano hayo na Tanzania ku-qualify kuingia katika mpango wa HIPC.

..pesa zinazotokana na HIPC ndiyo zinasaidia mipango mikubwa kama MKUKUTA, MKURABITA, na ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu.

..Uganda wali-qualify kuingia HIPC wakati Tanzania tunaongozwa na Raisi Mwinyi. binafsi naamini kama Mwinyi angekuwa na nidhamu na asingeharibu mahusiano yake na IMF/WB basi Tanzania ingeingia kwenye HIPC miaka ya 90.

..nadhani kila Raisi anawajibika kuja na mambo mapya bila kuathiri yale mazuri yaliyoachwa na waliomtangulia.

NB:

..nilitegemea Kikwete atafanya mambo makubwa kuliko Mwinyi na Mkapa. Kikwete amepokea nchi ikiwa na hali nzuri KIUCHUMI kuliko hao wawili waliomtangulia.

Jokakuu:

Mkuu itabidi u-check facts zako. HIPC ilianzishwa 1996 na Mwinyi alikuwa tayari amestaafu. Hivyo isingewezekana Uganda kujiunga HIPC wakati Mwinyi yuko Madarakani.
 
Zakumi said:
Jokakuu:

Mkuu itabidi u-check facts zako. HIPC ilianzishwa 1996 na Mwinyi alikuwa tayari amestaafu. Hivyo isingewezekana Uganda kujiunga HIPC wakati Mwinyi yuko Madarakani.

Zakumi,

..I am tied up right now...besides, I dont think you would come here and purposely[sp?] mislead us. kwa hiyo tukubaliane kuwa HIPC ilianzishwa 1996.

..bado naamini kwamba mahusiano mabaya kati ya serikali ya Ali Hassan Mwinyi na vyombo vya fedha vya kimataifa yalisababisha Tanzania kuchelewa ku-qualify for HIPC.

..kwa mtizamo wangu kama serikali ya Mzee Mwinyi isingekosa nidhamu ya kusimamia economic reforms, ukusanyaji kodi, na udhibiti wa mapato, basi Tanzania ingeweza kuingia HIPC kabla hata ya Uganda.
 
Nadhani tulikuwa na mjadala kuhusu misaada na madeni. Katika picha kubwa tunaweza kumlaumu Mwinyi tunavyotaka.

Lakini kutokana na literature zilizokuwepo sasa kuhusu failure ya misaada na madeni kuna uwezekano mkubwa tulikuwa tu-deal na phenomena nyingine kabisa.

Nchi mbili za mwanzo za kiAfrica kujiunga na HIPC zilikuwa ni Ghana na Uganda. Coincidently, nchi hizi zilikuwa za utawala wa kijeshi-jeshi.

HIPC ilianzishwa kwa sababu program za mwanzo za WB/IMF za kuinua uchumi wa nchi masikini zikiwemo Uganda na Ghana zili-fail. Na prescription ikawa inatakiwa.
 
Back
Top Bottom