Katavi: Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ahimiza vipaumbele vya Bajeti ya 2024/2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Kikao cha Kamati ya Ushauri wilaya ya Mpanda (DCC) Mkoani Katavi kimepitisha rasimu ya Bajeti ya 2024/2025 kwa jumla ya zaidi ya Shilingi Bilioni 53 (Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zaidi ya Shilingi Bilioni 27 na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo zaidi ya Shilingi Bilioni 26).

Mbali na rasimu hiyo kupitishwa Afisa Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango na Uchumi Manispaa ya Mpanda, Leonald Kilamuhama amesema zipo changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha utekelezaji wa miradi kwa wakati sahihi ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara pamoja na baadhi ya Wananchi kutowiwa kujitolea katika shughuli za maendeleo huku Edger Mnyavanu.

ambaye ni Mkuu wa idara ya mipango na Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo amesema Halmashauri ya Nsimbo imeomba kupatiwa magari 3 ya kufika katika majukumu ya kiserikali pamoja na gari la idara ya afya.

Haidary Sumri ambaye ni Meya wa Manispaa ya Mpanda na Halawa Malendeja ambaye ni Mwenyekiti wa Halimashauri ya Nsimbo wamesema rasimu hiyo ya Bajeti ya 2024/2025 italeta utatuzi mbalimbali katika mahitaji ya miradi itakayotekelezwa.

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Lwamba akisikitishwa na baadhi ya wenyeviti wa mitaa hushiriki katika kulinda wafugaji wanaoharibu na kulisha mifugo yao katika vyanzo vya maji ambapo amesema chama hakitamfumbia macho mtumishi ambaye atashindwa kusimama vyema katika nafasi yake.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesema Halmashauri ya Nsimbo na Manispaa ya Mpanda zinatakiwa kuhakikisha Bajeti ya 2024/2025 inaleta mabadiliko makubwa katika miradi itakayopangwa na kutekelezwa ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo kwa wakati ulio sahihi ambapo amesisitiza uwajibikaji wenye tija na weledi kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom