Katavi: Mpanda yajipanga kukabiliana na magonjwa ya mlipuko

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imejipanga kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kulipuka katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.

Hayo yamesemwa katika kikao kazi maalumu kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kikiwa ni sehemu ya kuweka mikakati mahsusi ya kuhakikisha magonjwa ya mlipuko hayatokei.

Erick Kisaka na Mayunga Mabinda ni maafisa afya katika wilaya ya Mpanda wamesema magonjwa ya mlipuko yanapaswa kuwekewa mikakati mathubuti ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi ili kufuatilia suala la usafi wa mazingira katika sehemu mbalimbali ikiwemo makazi ya watu.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesisitiza kila kaya kuhakikisha inazingatia suala la usafi wa mazingira ikiwemo kunawa maji tiririka sanjari na kuwataka watumishi kuanzia ngazi ya serkali ya mtaa kuweka nguvu kazi katika kutunza mazingira ipasavyo katika hali ya usafi.

Mbali na hayo Jamila amewataka maafisa afya kufanya ukaguzi katika maeneo ya kutoa huduma ya chakula na usafiri ikiwemo maeneo ya mabucha ambapo amesisitiza kuzingatia suala la usafi ili kuzuia na kujikinga na magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kutokea ambapo mpaka hii leo hakuna mgonjwa ambaye ameripotiwa kupatwa na ugonjwa wowote wa mlipuko katika wilaya ya Mpanda.
 
Back
Top Bottom