Katavi: Malalamiko ya waliofyekewa Mahindi yatua kwa Mkuu wa Wilaya

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Jamila Yusuf ameeleza kuwa amekerwa kwa tukio la baadhi ya wakulima katika Manispaa ya Mpanda kufyekewa mahindi yao ambapo amesema kitendo hicho si cha uungwana katika mstakabali wa maisha ya wananchi.

Jamila amesisitiza viongozi wa mtaa na kata kuhakikisha wanatekeleza sheria kwa wakati sahihi na sio kuchukua maamuzi kwa kuviziana.

Aidha, Jamila amewasihi wakulima waliofyekewa mahindi kuwa watulivu uongozi wa Wilaya unafanyia kazi malalamiko hayo kuona namna bora ya kumaliza tatizo hili kwa njia nzuri zaidi.

Wananchi wa Mpanda walifyekewa mahindi kwa sababu ilizuiwa kupanda mazao marefu katikati mji.

Soma zaidi >>> Zaidi ya heka 6 za Mahindi zimefyekwa Mjini Mpanda
 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Jamila Yusuf ameeleza kuwa amekerwa kwa tukio la baadhi ya wakulima katika Manispaa ya Mpanda kufyekewa mahindi yao ambapo amesema kitendo hicho si cha uungwana katika mstakabali wa maisha ya wananchi.

Jamila amesisitiza viongozi wa mtaa na kata kuhakikisha wanatekeleza sheria kwa wakati sahihi na sio kuchukua maamuzi kwa kuviziana.

Aidha, Jamila amewasihi wakulima waliofyekewa mahindi kuwa watulivu uongozi wa Wilaya unafanyia kazi malalamiko hayo kuona namna bora ya kumaliza tatizo hili kwa njia nzuri zaidi.

Chanzo: Bugoma Wa Bugoma
Amri ilitoka kwake, kaona wakubwa zake wameliona awaruka Watendaji wa chini.
 
Eti Mahindi mjini ni kichaka cha wezi!? Huyo kiongozi aliyetoa agizo hilo siku akihamishiwa Dar,ina maana atakata Minazi yote kisa hataki mazao marefu kwa eneo lake!!??
Pia watuambie urefu walikubaliana kuanzia meter ngapi!!
 
Eti Mahindi mjini ni kichaka cha wezi!? Huyo kiongozi aliyetoa agizo hilo siku akihamishiwa Dar,ina maana atakata Minazi yote kisa hataki mazao marefu kwa eneo lake!!??
Hapana kufyeka mazao haikubaliki, nia yake ni njema lakini angesubiri wavune then ndio sheria kali iwekwe
 
"Jovinari Deus ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani na Christina Mshani Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpanda Hoteli wamesema baadhi ya Wananchi hawahudhurii katika mikutano ya hadhara ambapo ndipo maelekezo ya Serikali hutolewa huku wakisisitiza mazao marefu kutopandwa katika mitaa yao."
 
Mafi yao popote walipo hawastahili kuwa viongozi hao kwa nn wasibuni mbinu za kupambana na wahalifu?
 
Eti Mahindi mjini ni kichaka cha wezi!? Huyo kiongozi aliyetoa agizo hilo siku akihamishiwa Dar,ina maana atakata Minazi yote kisa hataki mazao marefu kwa eneo lake!!??
Kuna muda huwa nawaza hii elimu tunayoipata mashuleni pamoja na vyuoni huwa inatusaidia nini.

Kweli unatoa amri ya kufyeka chakula kwasababu ya urefu wa mashina yake!🙆‍♀️

Vetting haina maana
 
Sheria za Mipango Miji zinakataza kupanda mazao marefu eneo la Mji
Mkuu hivi kwenye hizo sheria kuna baadhi huwa zinachaguliwa zifuatwe na nyingine zisifuatwe?

Mbona sheria nyingi tu tunaona zinavunjwa tena ambazo zinahatarisha uhai pamoja na maendeleo ya taifa?

Chakula ni uhai. Kuna vitu vingine tujaribu kuwa na fikra kidogo.

Japo una point!
 
Sheria zipo na zikivunjwa bila hatua kuchuliwa haina maana kwamba hazipo au zimesimama.

Cha msingi wakati wa kuchukua hatua, mamlaka ya usimamizi wa sheria inapaswa kueleza imechukua hatua kwa sheria ipi.

Huwezi kuilaumu Mamlaka kwamba kwanini imekuacha ukavunja sheria halafu ndiyo ikaja kukuadhibu.

Mwananchi ana haki ya kufanya lolote atakalo ilimradi havunji sheria, ila serikali kwa kila inalofanya ina wajibu wa kueleza ni kwa mujibu wa sheria ipi.

Mfano hapa wananchi wa Mpanda wana haki ya kulima eneo la Manispaa lakini hawatakiwi kulima mazao marefu.

Manispaa nayo imechukua hatua ya kuyafyeka mazao na ikaeleza sababu ya kufyeka kwamba ni marefu na ni kinyume na Sheria za Mipango Miji.
 
Back
Top Bottom