JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Wakati Serikali inahamasisha Wananchi kujishughulisha na shughuli za Kilimo ili kujikwamia kimaisha, baadhi ya Wakulima katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamefyekewa Mahindi ikidaiwa ni kosa kupanda mazao marefu mjini.
Lucia Balizio ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Msasani na Nestori Kameme mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hoteli wamekerwa kwa kufyekewa mahindi yao ambapo wamedai kila mwaka wanapanda Mahindi katika mashamba hayo ambayo ndio mkombozi wa maisha yao.
Jovinari Deus ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Msasani na Christina Mshani Mwenyekiti wa Mtaa wa Mpanda Hoteli wamesema baadhi ya Wananchi hawahudhurii katika mikutano ya hadhara ambapo ndipo maelekezo ya Serikali hutolewa huku wakisisitiza mazao marefu kutopandwa katika mitaa yao.
Nao baadhi ya Wananchi katika Manispaa ya Mpanda wametoa maoni yao kwa kutoridhishwa na tukio hilo la kufyeka mahindi yaliyopandwa ndani ya Manispaa ya Mpanda lakini wanadai ni bora busara zingetumika ili kuzinusuru familia hizo kuziingiza katika maisha ya kuomba omba hasa katika mwaka huu wa 2023/2024 kwani tegemeo lao limeondolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amesema licha ya katazo la kupanda mazao marefu ndani ya viunga vya manispaa lakini amekerwa na kitendo hicho cha kufyeka mahindi ya wakulima hao.
Aidha, Jamila amesema viongozi wa Manispaa watakaa kikao ili kuona namna bora ya kuwalipa wakulima hao.