Hiki chama cha kijani kitakua kimewapumbaza wengi sana nchini. Tena cha ajabu hata wanaojiita eti ma-great thinkers nao wanapumbazwa na hiki Chama. Hii inasababisha hata maendeleo kuchukua muda sana nchini kwa vile tu kuna watu wanashabikia uozo uliopo nchini, hawataki mabadiliko.
Eti mtu anatokea na kudai haiwezekaniki kulisha maneno clip ya dakika 5. Hawafahamu kama watu wanaangalia tamthilia za kina MARA & CLARA zimerekodiwa Ki-philipine na kulishwa maneno ya Kiengereza zinafikia mpaka Episodes zaidi ya 30 na zote huwezi kujua kama ni maneno ya kulishwa, sembuse vidakika 20 vya Bukoba Boy?
Funguka akili Ndugu, hata kama unalipwa lakini jaribu ku-act basi ki-great thinker japo kwa muda tu.
Yaani kwa mfano uliotoa tu tayari unadhihirisha wala hufahamu kinachoongelewa....yaani mwenyewe umeona umetoa bonge la ushuhuda?! Nani amebisha kwamba video clip hailishwi maneno?! Mie nimeshafunguka, ila wewe ndie unahitaji kufunguka macho!!
KInachozungumzwa hapa sio kulishwa maneno....kinachozungumzwa au ninachozungumza ni kufanya voice match; umenielewa?! Kwamba, leo hii uchukue video ya Obama, kisha umlishe maneno ambayo kimsingi hakutamka yeye, lakini sauti iwe ile ile ya Obama..UMEELEWA BANDUGU?!
Na ndio maana, nikakuambia wazi kwamba ku-fake sauti si kazi ndogo na video/audio zote ambazo zimekuwa faked but with perfect voice match zinakuwa ni fupi….in most cases zinakuwa less than 5 minutes. Ugumu ni kwavile ili uweze kufanya hicho kitu effectively, ni lazima uwe unaunganisha various audio clips za muhusika and not otherwise unless awepo mtu anayeweza kuigiza sauti yake kwa 100%. So how do you join those audio clips….Kwa mfano, mathalani mtu alitaka Lwakatare atamke
"Hakikisha ukishamtia mikononi yule Msacky, basi hapo hapo mpige risasi!" So, kupata mtiririko kama huo ni lazima upate audio clips za Lwakatare ambazo ndani yake ametamka maneno kama hayo na kisha uunganishe hizo clips. Kwa mfano labda kuwe na audio files zenye sentensi zifuatazo:
1. Mpeleke mtoto stendi na
hakikisha ukishamtia kwenye gari tu wewe rudi……
2. Baada ya kufika polisi nikakuta ametiwa
mikononi yule mwizi anayetususumbua hapa…..
3. Amini usiamini, kati ya wahariri hodari,
Msacky ni mmoja wao
4. Baada ya kuhangaika sana, nikaona
basi hapo hapo ni bure nipumzike….
5. Kama kuna nguruwe anaharibu mazao,
mpige risasi tu asije akazidi kukutia hasara….
Hivyo basi, ili kuweza kumlisha maneno sawa na BLUE COLORED sentensi with exact voice match, ni lazima uwe ume-review different audio files za (say)Lwakatare ambazo ziwe zinafananafana sawa na sentence 1 to 5 hapo juu. Utakachofanya wewe, una-copy hayo maneno in RED kisha unatumia maujanja ya kiteknolojia na kutengeneza sentensi moja itakayosikika
"Hakikisha ukishamtia mikononi Yule Msacky, basi hapo hapo mpige risasi!" Sentensi kama hiyo, mtu unaweza kuingizwa mkenge na kuzani ndicho alichokisema Lwakatare kumbe kimsingi, hakuna uhusiano wowote na kilichofanyika was just combination of different audio clip files na kuunda one complete and logical sentence! Na kwa kuwa ni kazi sana mtu kupata mtiririko kama huo, ndio maana utakuta manipulated videos/audios with perfect voice match zinakuwa fupi sana….na sio kama ile ya Lwakatare ambayo ni zaidi ya robo saa!!
However, mtu unaweza kum-set up kwa leading questions ili upate majibu yatakayotoa desired audio clips….Na kama ulivyoona, katika sentensi ya maneno kumi, unaweza kujikuta unachukua neon moja tu. So, kwa clip ambayo imeenda beyond robo saa itakuwaje?!
So, hapa issue sio kumtia mtu maneno kama ambavyo unadai, issue ni kumtia maneno lakini sauti iwe yake yeye mwenyewe na sio mfano wako wa Tamthilia za Kifilipino simply because, wale zinazosikika sio sauti zao!