MCHEZO HUU WA KITOTO
Mimi nimeiangalia clip ya Lwakatare ile iliyokuwa uploaded 11.03.2013 zaidi ya mara 5. Halafu nimeangalia na ile clipiliyokuwa uploaded 15.03.2013 ya maandishi aliyokuwa anaandika wakati wa akitoa maelekezo. Yafuatayo ni maoni yangu
1.Kuna uwezekano mkubwa sana tena sana kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kwa kumuahidi kitu Fulani au ujira Fulani kwamba bwana Lwakatare arekodiwe, ili baadae kuja kuipakaza matope CHADEMA. Mwaigulu Nchemba alitoa kauli kuwa ana video za kupanga mauaji za viongozi wa chadema mwishoni mwa 2012. Na ile clip BUKOBA boy ni ya 28.12.2012.
2. Ukiiangalia Clip kuna mtu anakuja na kuingia ndani ya sehemu wanapopanga hayo mabo kusema vip RICH. Ukimuangalia Lwakatare wala hakushituka ujio wa huyo mtu. Haingii akilini unapanga mauaji halafu mtu anakuja, nyie bila kushituka huku mkiendelea kupanga uhalifu.
3.Kama aliyemrekodi alirekodi kwa siri. Alirekodi vipi haya maandishi aliyokuwa anaandika Lwakatare kwa muonekano huo ?
4.Zile kelele za honi za magari, watu kupitapita(mdada) na mwanzoni kuwa eti HAPO TUTA NOTE vinaacha maswali kibao kama kweli they were serious.
5.Kwenye ile clip iliyokuwa uploaded 11.03.2013 inaonyesha kulikuwa na watu 2 mbele ya Lwakatare.Mmoja alikuwa kimyaa kabisa ANGALIA MACHO YA LWAKATARE VIZURIUTAGUNDUA.
Lakini cha ajabu utamsikia Lwakatare anasema Umenielewa! mara baada ya muda tena Umenielewa! kwanini asiseme mmenielewa? Huku ni kujikanganya.
KWA YEYOTE ANAYESOMA UJUMBE HUU NA AJUE kuwa huu ni mchezo wa kitoto kabisa wa kutusahaulisha kwenye mambo ya msingi kama
1.Wadogo zetu zaidi ya 200,000 waliopata sifuri
2.Mijadala ya bunge kuwa edited kabla ya kurushwa
3.Kuzivunjavunja kamati za bunge na kuacha maswali mengi
4.Katika katika ya umeme hasa jiji la DSM.
5.Mauaji ya padre mushi na ujio wa FBI
6. Sheik kuvamiwa Zanzibar
7.Mhariri Kibanda kuvamiwa
9.Padre ambrose kupigwa risasi.
10.KUWA HAMISHA CHADEMA KWENYE SEHEMU MUHIMU YA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA HASA KWENYE KUUNDA MABARAZA ILI HATIMAYE MAONI YA TOLEWE NA DEADLINE NI 20.03.2013.Wanataka CDM waendelee na Lwakatare huku katiba ikiendelea sehemu muhimu.
11.Hii ya kumuunganisha na Joseph Ludovick siijui sana ila utakuwa ni mwendelezo wa usanii wa MCHEZO WOTE.
12.Kusema kuwa alilishwa maneno haina nguvu baada ya wacheza mchezo kuleta ile karatasi aliyokuwa anaandika wakati wa kutoa maelezo.LABDA SASA KAMA KUNA TECHNOLOGIA YA KUIGILIZIA HADI MWANDIKO NA UNACHOKISEMA.KAMA IPO HIYO BAASI NANYOSHA MIKONO .
WITO KWA CHADEMA
1.Kwa nia njema kabisa wamsimamishe cheo bwana Lwakatare.Ili apate muda mzuri wa kushughulikia ishu yake.
2 .Mawakili wanaomtetea hata kama ni wana CDM wasijali waendelee kumtetea kwani ni mteja wao na ni sehemu ya kazi yao.
3.CDM iueleze umma juu ya huu MCHEZO MCHAFU wa mwanachama kukubali kutumika, kukubali kurekodiwa kwa ahadi ya hela au nyumba au kitu chochote cha dhamani sana ni kudumaza demokrasia.
NB.MWIGULU Nchemba alipata kiburi cha kusema ana clips za Chadema kwa kuwa walikuwa wameshafanya mpango mzima. Na polisi isingeweza kumuuliza kwani mdio wanaotumika kufanikisha mpango mzima.
4.sasa hivi M4C iendelee kwa kasi
5.Kuhimiza vijana na watu wote kuwa na vitambulisho vya kitaifa
6.kuhimiza vijana na watu wote kufuatilia mchakato wa katiba hatua kwa hatua.
7.Viongozi chonde msije andaa maandamano ya kutaka kumtoa Lwakatare kwa nguvu. Hapo tutanasa tena kwenye mtego wa kusema chadema chama cha fujo. Mtego ambao CUF walinasa.Kwani kamwe hawatatoa kibali cha kuandamana kitakachofuata kuandamana bila kibali then mabomu, risasi, na mauaji. Nasema hivi kwa bado na doubt na ile clip kuwa MTOA MAELKEZO YA KIHALIFU ALIJUA KUWA ANAREKODIWA NA WALIOKUWA WANAMREKODI WALIJUA NINI WANAKIFANYA TENA BILA KIFICHO .NA NDIO MAANA SASA HIVI WATALETA CLIP ZINGINE 4 ZILIZOBAKI.
Ila tushukuru kwani wanatuonyesha mbinu zao kuelekea 2015 mapema. WAMETUSAIDIA na TUNASHUKURU MUNGU
Poleni sana kwa kusoma ujumbe huu mrefu .