Wadau wa jamvi hili, tunapomjadili huyu Katibu wa Bunge Bw. Kashililah inabidi kwanza tumjue yeye ni nani? Kwa utafiti wangu mdogo sana, bwana huyu si lolote si chochote! Kwanza udaktari wake ni wa mashaka achilia mbali uwezo wake wa kazi. Phd yake nasikia ya mtandaoni, wengine wanadai ni ya south Africa lakini bado maswali ni mengi kuliko majibu. Uwezo wake kulisaidia Bunge na kumsaidia Spika wake ni zero. Kwanza atamsaidiaje yule mama wakati yeye mwenyewe alikuwa kibaraka wa mzee Sitta? Ufisadi wao na wizi wa fedha za bunge ndio uliowaunganisha na kuwafanya maswahiba. Sitta alimtaka Kashilila kwa udi na uvumba, alifanya njia zote bwana huyo ateuliwe kuwa Katibu wa Bunge.
Utafiti unaonyesha kuwa Kashilila hakuteuliwa kwa uwezo wake maana waliachwa Wenye uwezo wao na waliokuwa tishio kwa uwezo wa kazi yasemekana walifanyiwa mizengwe na kuhamishwa Bunge. Baada ya Katibu wa Bunge Bw. Foka kustaafu vita ya ukatibu wa Bunge ilianza. Sitta kwa kutafuta mtu atakayelinda maslahi yake alimpigia debe Kashilila aliyekuwa Mkurugenzi ktk mojawapo ya Idara za Bunge kwa muda wa chini ya miaka 2 tu na kuwa Katibu wa Bunge. Ni vema kama angekuwa na uwezo kuliko wengine lakini ni bomu kuliko walioachwa. Natamani ningemuona anatoa lecture siku moja pale UDSM au UDOM na hiyo Phd yake feki kama watu wasingezimia! Nimewahi kumsikia akiongea lugha ya kwa malkia mahali fulani, niliona aibu sana kwa mtu mwenye Phd. Afadhali hata huyo Lema anayedaiwa kuwa ni form four na alipata Div four ya pointi 29, lkn shughuli yake tunaiona!
Kashilila ana ubavu gani wa kuita waandishi wa habari leo na kujifanya kuwakosoa Wabunge? Ni dhihaka kudhani kuwa Wabunge hawazijuwi Kanuni za Bunge, wanazijua vizuri, tena Wabunge wa kambi ya upinzani wanazijua vema kuliko hata hao wa chama tawala! Kwanini Kashilila hasemi kweli nini kilichojiri siku Wabunge walipozozana bungeni? Watanzania ni mashahidi, wana akili, wanaelewa na wanafuatilia mambo. Watendaji wabovu wakiongozwa na Kashilila mwenyewe pengine kwa makusudi na kwa kumhujumu Spika wa sasa aonekane hafai kuvaa viatu vya Sitta hawamshauri vema na pengine hutoa taarifa za kupotosha. Mfano mzuri siku ya tukio, issue ilikuwa ni uchaguzi wa wenyeviti wa Bunge ambapo Kanuni zilipindishwa. Lengo lilikuwa zuri lkn utaratibu ulitaka hilo liweze kufanyika Kanuni ilibidi zitenguliwe. Msaidizi wa Kashilila aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi wakati akitoa maelezo ya taratibu za uchaguzi huo ilibidi atoe maelezo ya ziada kwanini Kanuni zitenguliwe kuruhusu maazimio ya Kamati ya Uongozi kupitisha majina 3 tu na si 6 kama Kanuni zinavyotaka. Hapo ndipo mchezo ulipoanza, mara oh...Kamati ya Uongozi ilitengua Kanuni, mara oh....Wabunge makini wakataka kujua Kanuni zinasemaje? Mie nimebahatika kuzipitia Kanuni kwa sana tu, jamani hakuna mwenye mamlaka ya kutengua Kanuni za Bunge isipokuwa Bunge lenyewe, hata Kamati ya Uongozi wala Tume ya Bunge haina mamlaka hayo. Kuna wakati Msimamizi wa uchaguzi alijaribu kutetea kuwa Kanuni hazijakiukwa na kutaka kuonyesha Wabunge hawazijuwi Kanuni, wote tuiloangalia TV siku ile tuliona Mhe. Halima Mdee akimshushua Katibu huyo wa Bunge kuwa asome Kanuni vizuri na asisome nusunusu, loh ilikuwa aibu! Mhe. Lukuvi kwa haraka alitambua kosa na akaomba sasa Bunge litengue Kanuni ili uchaguzi huo na hayo majina 3 yaliyowasilishwa na Kamati ya uongozi yapigiwe kura.
Bw. Kashilila awe mkweli, amechemka! Kwanza siku ya tukio hakuwa Bungeni wala hakuwa Dodoma, kwa macho yangu nilimuona Dsm akiwa Shoppers plaza kwenye kliniki ya macho. Kama anabisha akanushe maneno yangu! Kwanza wabunge walioanza kuzomea walikuwa wa CCM tena wengi wao ni mawaziri. Atasemaje aliyesema funga mlango tupigane alikuwa Lema? Kashilila kuita waandishi wa habari anataka kutuambia nini? Ana lipi jipya? Avunje makundi yake Bunge, akae chini afanye kazi na amsaidie Spika! Tangu yule mama kaingia madarakani yasemekana Kashilila hakai ofisini na hampi mama wa watu ushirikiano, kisa swahiba wake Sitta kaikosa nafasi hiyo. Wanachotaka ijengeke picha kuwa Spika kashindwa kazi. Wa-TZ tunazo data za Kashilila asifikiri hatujuwi yanayoendelea huko mjengoni kwao. Asiwe mnafiki wa kujifanya hajuwi kitu. Hivi karibuni alipoulizwa kuhusu ujenzi wa nyumba ya Spika huko Dodoma, eti alijifanya hajuwi kitu, kivipi? Maana yeye ndiye aliyetoa idhini kwa CDA kuendelea na ujenzi wa nyumba hiyo na hata upatikanaji wa mkandarasi etc, inakuwaje anasema hajuwi? Huyu ndiye Kashilila anayetaka kuaminisha watu kuwa yupo makini na kazi yake.
Kashilila kudai kuwa Wabunge wengi ni wapya na ni vijana sio justification ya fujo zinazotokea Bungeni wakati huu. Uzuri ni kwamba pamoja na wengi kuwa wapya na vijana uelewa wao ni mkubwa kuliko wa wakati mwingine wowote. Lazima tukubali kuwa Wabunge wa upinzani pia wameongezeka kulinganisha na bunge lililopita, wasomi ni wengi pia na changamoto zilizopo sasa kama za ufisadi, kupanda kwa gharama za maisha, umasikini wa Wa-TZ unaokua kila uchao ndio sababu za kuongezeka kwa udadisi, ufuatiliaji na uelewa wa wananchi maana hawadanganyiki tena. Watu wanataka kujua A-Z ya hatima ya maisha yao na mustakabali wa nchi hii. Ndio maana wanahoji Bungeni, wanahoji vijiweni, wanahoji magazetini, wanahoji kila mahali....hao ndio Wa-TZ wa leo! Wanataka majibu kwa maswali yao magumu na si blah blah za watu kama akina Kashilila. Kwanza sijuwi kwa nini havuliwi hilo gamba lake hapo Bungeni kama walivyoasisi watu wa chama chake na wateule wake?
Kashilila jivue gamba mwenyewe, maana umeshindwa kuongoza safu ya watendaji wako wa Bunge kumsaidia Spika na kulisaidia Bunge!