Kashilila hukumtendea haki Lema

Kashilila hukumtendea haki Lema

Katibu wa bunge bwana Kashillillah aliita waandishi wa habari kuelezea minyukano iliyojitokeza katika mkutano wa 3 wa bunge hili la 10, aliuleza umma kwamba kilichosababisha ni ugeni wa wabunge na sio udhaifu wa Spika. Alienda mbali zaidi kutolea mfano wa mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema kwamba kitendo chake cha kusema 'funga mlango tupigane' kinatokana na uchanga wake bungeni na kwamba hana wala hajasoma kanuni za bunge. Maoni yangu ni kwamba katibu hajamtendea haki Mhe. Lema kwa sababu
1. Ni wabunge wengi ambao walijibizana maneno wakiwemo wakongwe na mawaziri (tulisikia wengine wakisema 'atoke nje');
2. Si kweli kwamba mhe. Lema hana kanuni za bunge;
3. Kila bunge jipya huja na wabunge wapya lakini haya hajajitokeza huko nyuma;
Mtazamo wangu ni kwamba yaliyojitokeza ni mwanzo tu wa kuonesha dhahiri kwamba spika wa sasa hakuwa amewiva vya kutosha kuvaa viatu vya Sitta. Aidha kitendo cha ufafanuzi huu kutolewa na katibu wa bunge ni ushahidi mwingine kwamba Spika kashindwa. Naomba kuwasilisha.


Huyu Karani ameonesha dharau kubwa sana kwa Wabunge kutokana na haya aliyosema. Hivi kulikuwa kuna haja gani ya yeye kutoka na kuyasema haya yote? Kwanza Wabunge hata wakipigana au kutukanana Mjengoni ni haki yao na sheria inawalinda - wana imunity wakiwa humo.

Ushauri wangu ni kuwa Wabunge wamfukuze kazi katika kikao kijacho.
 
Sasa naamini Bunge halina uongozi. Katibu wa bunge na wasaidizi wake bomu. Spika Anna Makinda bomu. Kiongozi wa serikali bungeni na msaidizi wake bomu. Wenyeviti wengi wa kamati za kudumu bomu. Wote hawa fikra zao finyu hawana uwezo wa kujibu hoja bali wanalazimisha maneno yao yaheshimike na kuaminika hata kama ni mgando na uongo
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kukiwa na Spika dhaifu asejua kanuni za bunge unategemea nini kwa anaowaongoza? Pili ni afadhali kuwa na wabunge wahuni wanajua nini wanafanya kuliko kuwa na wabunge bogus na mafisadi yasiyojua lolote zaidi ya ushabiki usioenda shule.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Bwana Zulu ndiye PRO wa bunge letu. Sijamsikia akijibu hoja yoyote kwa wanahabari tangu bunge hili lianze.

Kama Kashilila aliwajibibka kutoa ufafanuzi kwa mambo yanayotokea bungeni, kwa nini amechelewa sana. Watu wamejadili hadi wamesahau yeye ndo anaibuka na kutudanganya tena. Je, ni mzembe?

Kwenye kikao cha February, kuna mdada mbunge mmoja alikuwa anagombea uwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu. Ofisi ya Kashilila ilikiuka kanuni na kumfanyia mizengwe huyu dada. Katika hotuba yake bungeni dada huyu alijitoa na kuitupia lawama ofisi ya Kashilila. Ilirushwa live na TBC na Star tv.

Kashilila hajajibu tuhuma za huyu dada hadi leo. Kama kuna ushahidi huu kwamba Kashilila AMA hazifahamu kanuni na au amezipindisha, je Kashilila ni mgeni bungeni? Je, hana elimu ya kutosha?
 
Bwana Zulu ndiye PRO wa bunge letu. Sijamsikia akijibu hoja yoyote kwa wanahabari tangu bunge hili lianze.

Kama Kashilila aliwajibibka kutoa ufafanuzi kwa mambo yanayotokea bungeni, kwa nini amechelewa sana. Watu wamejadili hadi wamesahau yeye ndo anaibuka na kutudanganya tena. Je, ni mzembe?

Kwenye kikao cha February, kuna mdada mbunge mmoja alikuwa anagombea uwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu. Ofisi ya Kashilila ilikiuka kanuni na kumfanyia mizengwe huyu dada. Katika hotuba yake bungeni dada huyu alijitoa na kuitupia lawama ofisi ya Kashilila. Ilirushwa live na TBC na Star tv.

Kashilila hajajibu tuhuma za huyu dada hadi leo. Kama kuna ushahidi huu kwamba Kashilila AMA hazifahamu kanuni na au amezipindisha, je Kashilila ni mgeni bungeni? Je, hana elimu ya kutosha?

Yaani ina maanisha kuwa Wabunge waogope kusema eti kwa sabau wanaogopa Karani wa Bunge atachukuliaje maneno wanayosema. Sijawahi ona bangi mbichi kuliko hii!!! Kazi ya Kashishila ni kupanga ratiba ya vikao na kuhakikisha Mjengo una-function. Yeye siyo Mbunge na wala siyo Spika.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Kashilila amejenga makazi mapya ya Spika Dodoma kwa gharama ya zaidi ya sh bilioni 3.7. Siyo kwamba spika hakuwa na makazi mazuri, ni njia tu ya kutafuna pesa.

Wakati Kashilila anatumia zaidi ya bilioni 3.7 kujenga residence moja tu, Bunge hilohilo lilishutushwa na kuchunguza kwa nini BoT walitumia bilioni 2.5 kujenga residence moja mpya ya gavana na kukarabati moja ya zamani.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Yaani ina maanisha kuwa Wabunge waogope kusema eti kwa sabau wanaogopa Karani wa Bunge atachukuliaje maneno wanayosema. Sijawahi ona bangi mbichi kuliko hii!!! Kazi ya Kashishila ni kupanga ratiba ya vikao na kuhakikisha Mjengo una-function. Yeye siyo Mbunge na wala siyo Spika.

Mkuu hata kupanga ratiba kumemshinda. Kikao kilichomalizika hakikuwa na ratiba maalum na wala hakuna ratiba iliyowekwa kwenye website ya bunge kama tulivyozoea. Kikao kikianza asubuhi ndo wabunge walikuwa wanatangaziwa shuhuli za siku hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Ni hivi majuzi tumesoma kwenye baadhi ya magazeti kuwa Mwanasheria mkuu aliitwa kwenye vikao vya CCM kule Dodoma wakati inafanya madaliko katika safu ya uongozi. Na watu walihoji inakuwaje mwanasheria wa Serikali anashiriki kwenye vikao vya chama cha siasa?

Sasa Leo Katibu wa Bunge anaita waandishi wa habari na kuanza kuelezea 'upya' wa wabunge pamoja na madai kwamba baadhi yao hawazijui kanuni! Naomba kama kuna mtu mwenye job description ya katibu wa Bunge atuwekee hapa jamvini ili tujue katibu ana mamlaka gani na anawajibika kwa lipi?

Hizi kanuni za bunge zimekuwa zikiongelewa sana na Mama Makinda na sasa Katibu wa bunge kama some sort of holy gray! Na kuna uwezekano kabisa kuwa walipania kuzipindisha lakini kwa bahati mbaya hawa wabunge 'wapya' ambao wengi wao ni wanasheria wamewazidi 'maarifa' plus wameonesha kuwa kanuni za bunge ni taratibu na lazima zimesomwe pamoja na sheria mama ya nchi yaani katiba.

Mis-calculation ya kuweka Spika, naibu spika na katibu wa bunge ambao wote si wanasheria ndio mwanzo wa sokomoko bungeni. Kashilila aache kuhubiri porojo maana watanzania tumeona zomea zome na mipasho bungeni tofauti kabisa na kipindi kingine chochote hasa kipindi cha Spika Sitta. Kama taifa ni aibu kuona tuliyoona na nadhani ingekuwa busara kwa watu kama wakina Kashilila kuwa na different attitude wanapokaa kwenye viti vya uongozi badala ya kuja na excuses. Mbona kikao alichoongoza Mh. Jenista Mhagama kilikuwa na nidhamu nzuri? Fair play.
Yeah, I believe this woman (In bold red) could make the best Speaker than the current - Anna Makinda who unlike her predecessor Samuel Sitta has proved to be totally incompetent. The same is the case with her Deputy; Kashililla who fits more in the shoes of the propaganda platform of the worn out, exhausted and dilapidated CCM.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Exuper Kachenje

KATIBU wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, amemtetea Spika wa Bunge, Anna Makinda, kuwa kurushiana maneno kulikotokea kwenye mkutano wa tatu wa Bunge sio udhaifu wake, bali inatokana na wengi wa wabunge hao kutojua Kanuni za Bunge na Sheria.

Kauli ya Dk Kashilillah inaonekana kumkingia kifua bosi wake, Spika Makinda ambaye baadhi ya watu wameanza kuhoji uwezo wa utendaji wake katika kuliongoza Bunge."La pili, ni maandiko kuhusu uendeshaji Bunge, ninyi pia mmeandika. Katika mkutano wa Bunge uliopita wabunge kurushiana maneno


Ilitokea hivyo hata baadhi ya watu kuita Bunge shule ya msingi," alisema Dk Kashilillah na kuongeza:

"Asilimia 69 ya wabunge wa sasa ni wapya…hawajawahi kufanya kazi serikalini au kuajiriwa, kushiriki mijadala au makongamano."

Kuhusu umakini, Dk Kashilillah alisema kutokana na hali hiyo, uwapo wa wabunge hao unahitaji uvumilivu na msaada ili kuwawezesha kufanya kazi zao za Bunge."Uwapo wao unahitaji uvumilivu na msaada kuwawezesha kufanya kazi zao," alisema.


Alisema ofisi yake ilitoa semina kuelimisha wabunge kuhusu uendeshaji wa Bunge sanjari na vyama vikuu vya siasa nchini; CCM na Chadema kutoa semina kwa wabunge wake kuhusu masuala ya fedha, sheria na utawala zilizogharamiwa na ofisi yake.


Akijibu swali lililotaka kujua iwapo haoni kurushiana maneno kumetokana na Spika kutojua sheria na kanuni, hivyo kushindwa kuliongoza Bunge, Dk Kashilillah alisema madai hayo hayana ukweli.


Alisema Spika Makinda anajua sheria na Kanuni za Bunge, lakini anachofanya ni kuwalea kwa kufahamu kuwa bado wengi wao hawajui kanuni na taratibu za Bunge, ndio sababu hawafukuzi ndani ya Bunge.


Katika mkutano huo uliofanyika ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam, Dk Kashilillah alizungumzia pia Muswada wa Sheria wa Mapitio ya Katiba, ambao ulisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tatu wa Bunge, lakini ulirejeshwa kwa umma kupata fursa ya kuujadili zaidi.


Dk Kashilillah alisema kutopitishwa kwa muswada huo kutachelewesha hatua za kupatikana kwa katiba mpya, ambayo alisema wananchi ndio wataamua iwapo iandikwe katiba mpya au iliyopo ifanyiwe marekebisho.


Alisema ingawa muswada huo ulitambulika kama ni Muswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2011, lakini uhalisia utambulike kuwa ni Muswada wa Kuanzisha Kamisheni ya Kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba.


"..Kikubwa najua mngependa kujua kuhusu Muswada wa Katiba. Ulitammbulika kama Muswada wa Mapitio na Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011, lakini kimsingi utambulike kuwa ni Muswada wa Uundaji Kamisheni ya Ukusanyaji Maoni ya Wananchi kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba," alisema na kuongeza:


"Sisi tunaona muswada huu ungepita, ungesaidia kuipa muda wa kutosha kamisheni, tulitarajia sehemu ya hitaji la gharama zingeingia katika bajeti ijayo."

Alisema ingawa uliwasilishwa kwa hati ya dharura, lakini ulitangazwa katika gazeti la serikali Machi 11, hivyo ulifikia siku 21 na ungeweza kuwasilishwa kwa njia za kawaida.


SOURCE: Katibu wa Bunge amtetea Spika
 
Makinda kibaraka wa mafisadi lazima auone moto wa wanaharakati atake au asitake
 
makinda hajui sheria na anaongoza vikao vya bunge as if ni mwenyekiti wa kika cha kitcheparty au sendoff..hafai na hajui kanuni na sheria....
 
Job Description: Clerk of National Assembly.
===========================

1. Kufuta vumbi viti vya chumba cha Bunge
2. Ku-print ratiba za vikao na kuziposti kwa Wabunge
3. Kulinda Mjengo dhidhi ya ajali kama moto na vitendo vya jinai
4. Kuhakiksha bili zote za Tanesco na Maji za Mjengo zimelipwa kwa wakati
5. Kuratibu Protokali kwa Wabunge na wageni wa Bunge
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Hivi haya ma-CCM lini yataacha kujidanganya?

Tunafahamu kabisa tatizo la bunge hili ni Spika ambaye hana uelewa wa sheria. Tumeona jinsi alivyochakachua tafasiri ya kambi ya upinzani bungeni.

Tumeona pia jinsi alivyokachuchua hoja ya Mh. Lema kuhusu uongo wa Mizengo Pinda PM. Nitamu quote Mh. Sita aliwahi kusema kwamba Anne Makinda ni Mtu wa kukurupuka hivyo asisimamie hoja ya Richmond.

Tatizo kubwa la Bunge letu ni kwamba Mi-Bunge mingi ya CCM ni mbumbumbu inayopitisha miswaada na hoja kwa wingi wa MIILI yao na sio kwa wingi wa AKILI zao. No wonder ni wabunge wachache sana wa CCM wanaweza wakasimama na Tundu Lissu na kutoa nguvu ya hoja ya kisheria labda Sita au Mwakyembe ndio maana hata Mwanasheria mkuu wa Serikali alitolewa nishai na Tundu Lissu eti hakuna utafiti wowote ambao amewahai kufanyika nchini kuonesha needs za mahakama (sics)

Mi-bunge ya CCM ilizoa kupitisha mambo kama bendera kufuata upepo wamekuja wabunge weledi wa sheria kama Tundu Lissu, Halima Mdee sasa yameanza kuweweseka.

Mbona wakati wa ufunguzi wa bunge wakati wabunge wa CDM walipotoka nje ya ukumbi tulisikia maneno mengi ya kejeli lakini hatukumuona huyui Dk fake akija na statements kama hizi za kipumbavu.

Huyu Kashilila ni sawa tu boss wake Anne Makinda wanaoamini kwamba kama umekaa bungeni mda mrefu basi unakuwa mweledi wa kanuni za bunge. Kwa lugha rahisi ni kwamba kama ukifanya kazi MOI mda mrefu basi siku moja utakuwa neuron surgeon one day bila kwenda shule. Shame on you CCM
 
Siku ya jana nilishtuka sana nilipokuwa nikimsikiliza katibu wa bunge Ndugu Thomas Kashilila katika moja ya vipindi vya taarifa ya habari ya Star tv.Huyu bwana alizungumzia mambo mawili makubwa moja likiwa ni zomea zomea bungeni na suala zima la katiba mpya.
Katika zomea zomea katibu huyo wa bunge alisema kuwa kitendo hicho kinasababishwa na ugeni wa wabunge na kutojua kanuni za bunge vizuri,ambapo kwa maoni yangu naona alipotoka kwa kiasi kikubwa katika kuliongelea suala hili na jinsi alivyolipa mtazamo wake.Zomea zomea bungeni haikuanza leo huo ni mtindo ulioasisiwa na wabunge wa CCM ambao kwa kiasi kikubwa ni wengi na sote tulishuhudia bunge lililopita hata la Msekwa ambapo zomea zomea ilikuwa business as usual,sasa je nalo lilisababishwa na ugeni wa wabunge na huo ugeni wao ulidumu kwa kipindi gani?.Bunge lililopita lilikuwa na wabunge wengi wazee tofauti na bunge la sasa ambalo vijana ni wengi lakini bado zomea zomea ilikuwepo kama kawaida je nalo lilisababishwa na kutojua kanuni au ugeni?na kama ni kanuni je kanuni hizo zinasemaje kuhusu zomea zomea?na je zile semina elekezi za wabunge pale Ubungo-Plaza zilikuwa na manufaa gani katika kuwaelewesha wabunge kuzijua kanuni?.Ukweli ni kuwa vitendo vya zomea zomea bungeni linasababishwa na udhaifu mkubwa sana wa kanuni za bunge ambazo haziwabani wabunge katika hili ndo maana wanazomea zomea hovyo kitu ambacho katibu huyu wa bunge sijui hakijui au alikuwa anajaribu kupotosha kwa makusudi ukweli.
Suala la pili alilozungumzia ni mchakato wa katiba mpya ambapo alidai kuwa suala la katiba mpya kupitia mswada wa marejeo ya katiba unapotoshwa au umepotoshwa lakini hasemi kwa hoja kwamba kinachopotoshwa ni kipi.Katibu huyu wa bunge ametoa kauli sawia kabisa na Waziri Kombani,Waziri Wassira na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh.Jaji Werema ambao wote kwa nyakati tofauti wametoa msimamo huohuo kuwa kilichopo kwenye muswada kinapotoshwa ambapo wote hao hawatuelezi kinachopotoshwa ni kipi na sahihi ni kipi.Watu hawa kwa maoni yao wanafikiri kuwa watu hawaelewi kinachoendelea katika mchakato mzima.Tatizo la watu hawa ambao kwa kiasi kikubwa ni watetezi wakubwa wa serikali wanataka waaminike kwa kile wanachoongea lakini cha wale wanaowapinga kwa hoja kionekane si kitu.Hivyo basi ingekuwa vyema Mh.Thomasi Kashilila aeleze ukweli tena kwa hoja yeye kama katibu wa bunge kuhusu zomea zomea bungeni na katika suala la muswada wa katiba kipi hicho kinachopotoshwa badala ya kuleta hoja zisizokuwa na mashiko hata kidogo.
 
Katika hali ya kushangaza jana katibu wa bunge dr.kashilila amekuwa mwanasheria wa serikali kwa kutolea ufafanuzi muswada wa katiba na kusema ulikosewa kichwa cha habari na kuendelea kutolea ufafanuzi ambapo kimsingi hiyo ni kazi ya mwanasheria mkuu na waziri wa sheria na katiba.

Wakati akifanya hivyo wahusika wenyewe hawajawahi kuona shida yeyote wala tafasiri inayohitajika, vile vile aligeuka kuwa wakili wa kujitegemea kwa boss wake spika dhaifu anne makinda
 
naona kashilila anafanyia kazi magazeti ya ccm ndio yalioandika kuwa lema ndiye aliyeongea siye aliyeongea hivyo ni moses machali mbunge wa kasulu mjini-Nccr wanamuonea tu huyo jamaa na bungeni viti vyao viko vitatu vinafuatana pamoja anaanza moses halaf mnyika baadaye lema.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Dr.Kashilila ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kujifanya mwansheria wa kujitegemea wa spika dhaifu AnneMakinda na kujipa hadhi ya mwansheria mkuu wa serikali na waziriwa katiba na sheria alipokuwa anatoa tafasiri ya muswada wa katiba uliowasilishwa kwa hati ya dharura.

anaposema wabunge wengi ni wapya mbona bunge latisa halikuwa hivyo wakati badi lilikuwa na wabunge wengi wapya?Mnyika ni mpya bungeni ila ndio aliyeongoza kuomba muongozo wa spika pale kanuni zilipokuwa zinakiukwa, atatueleza nini kashilila kwa hapa?Makinda mwenyewe alikuwa anaendesha bunge kishabiki na kama mwalimu asiyejua kitu na hataki mwanafunzi amkoseo hadharani
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Back
Top Bottom