Sasa hata kama wewe ukiwa spika au Dr Slaa awe Spika utashikilia midomo ya wabunge wote ili wasilopoke na kusema fungeni milango tupigane! Mimi naona ni tatizo la kupata wabunge wahuni ambao wanashindwa kuelewa hadhi ya bunge na kuona kama wako kijiweni!
..Swali hili alipaswa kuulizwa na waandishi wa habari waliokuwa wanamsikiliza. Tuna tatizo katika fani ya uanahabari Tanzania... Wengi ni wasikilizaji tu na kureport kama ilivyo....Dazu! CCM ni kundi kubwa kuliko tunavyolitazamia. Mbona hajasema kwa nini Spika alitaka kwenda kinyume na taratibu hizo za bunge anazosema wabunge hawana katika mikoba yao? kwani ndo ulikuwa mwanzo wa hayo yaliyotokea na kuyatolea mfano! Waingereza wanasema ''kama watu hawafikiri unavyofikiri wafanye wafanye unachofikiri''. Tutawapeleka kunakotakiwa.
Ahsante
hahahahaha hajatendewa haki kivipi? nafikiri mtu akiwa mbunge lazima ajijengee ustaarabu fulani: awe na hadhi fulani.
Lema ni Mbunge mzuri lakini bado ana mambo ya kijiweni sana, nimemshuhudia katika maeneo mengi pamoja na kwenye mijadala mbalimbali.
Katibu wa bunge bwana Kashillillah aliita waandishi wa habari kuelezea minyukano iliyojitokeza katika mkutano wa 3 wa bunge hili la 10, aliuleza umma kwamba kilichosababisha ni ugeni wa wabunge na sio udhaifu wa Spika. Alienda mbali zaidi kutolea mfano wa mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema kwamba kitendo chake cha kusema 'funga mlango tupigane' kinatokana na uchanga wake bungeni na kwamba hana wala hajasoma kanuni za bunge. Maoni yangu ni kwamba katibu hajamtendea haki Mhe. Lema kwa sababu
1. Ni wabunge wengi ambao walijibizana maneno wakiwemo wakongwe na mawaziri (tulisikia wengine wakisema 'atoke nje');
2. Si kweli kwamba mhe. Lema hana kanuni za bunge;
3. Kila bunge jipya huja na wabunge wapya lakini haya hajajitokeza huko nyuma;
Mtazamo wangu ni kwamba yaliyojitokeza ni mwanzo tu wa kuonesha dhahiri kwamba spika wa sasa hakuwa amewiva vya kutosha kuvaa viatu vya Sitta. Aidha kitendo cha ufafanuzi huu kutolewa na katibu wa bunge ni ushahidi mwingine kwamba Spika kashindwa. Naomba kuwasilisha.
Angemsamehe Lema bure kwani Lema ni form four, aliyepata division four points 29, sasa unategemea nini?
Acha kudanganya watu Lema hajamaliza form four alifukuzwa shule akiwa form two kwa wizi wa godoro form four ya points 29 kaipata wapi.Maneno yake mjengoni ni mwisho wa akili na upeo wake hana anachoweza zaidi ya kubwabwaja na kutoa mitusi hovyo.
Hivi haya ma-CCM lini yataacha kujidanganya?
Tunafahamu kabisa tatizo la bunge hili ni Spika ambaye hana uelewa wa sheria. Tumeona jinsi alivyochakachua tafasiri ya kambi ya upinzani bungeni.
Tumeona pia jinsi alivyokachuchua hoja ya Mh. Lema kuhusu uongo wa Mizengo Pinda PM. Nitamu quote Mh. Sita aliwahi kusema kwamba Anne Makinda ni Mtu wa kukurupuka hivyo asisimamie hoja ya Richmond.
Tatizo kubwa la Bunge letu ni kwamba Mi-Bunge mingi ya CCM ni mbumbumbu inayopitisha miswaada na hoja kwa wingi wa MIILI yao na sio kwa wingi wa AKILI zao. No wonder ni wabunge wachache sana wa CCM wanaweza wakasimama na Tundu Lissu na kutoa nguvu ya hoja ya kisheria labda Sita au Mwakyembe ndio maana hata Mwanasheria mkuu wa Serikali alitolewa nishai na Tundu Lissu eti hakuna utafiti wowote ambao amewahai kufanyika nchini kuonesha needs za mahakama (sics)
Mi-bunge ya CCM ilizoa kupitisha mambo kama bendera kufuata upepo wamekuja wabunge weledi wa sheria kama Tundu Lissu, Halima Mdee sasa yameanza kuweweseka.
Mbona wakati wa ufunguzi wa bunge wakati wabunge wa CDM walipotoka nje ya ukumbi tulisikia maneno mengi ya kejeli lakini hatukumuona huyui Dk fake akija na statements kama hizi za kipumbavu.
Huyu Kashilila ni sawa tu boss wake Anne Makinda wanaoamini kwamba kama umekaa bungeni mda mrefu basi unakuwa mweledi wa kanuni za bunge. Kwa lugha rahisi ni kwamba kama ukifanya kazi MOI mda mrefu basi siku moja utakuwa neuron surgeon one day bila kwenda shule. Shame on you CCM
Acha kudanganya watu Lema hajamaliza form four alifukuzwa shule akiwa form two kwa wizi wa godoro form four ya points 29 kaipata wapi.Maneno yake mjengoni ni mwisho wa akili na upeo wake hana anachoweza zaidi ya kubwabwaja na kutoa mitusi hovyo.
Ni hivi majuzi tumesoma kwenye baadhi ya magazeti kuwa Mwanasheria mkuu aliitwa kwenye vikao vya CCM kule Dodoma wakati inafanya madaliko katika safu ya uongozi. Na watu walihoji inakuwaje mwanasheria wa Serikali anashiriki kwenye vikao vya chama cha siasa?
Sasa Leo Katibu wa Bunge anaita waandishi wa habari na kuanza kuelezea 'upya' wa wabunge pamoja na madai kwamba baadhi yao hawazijui kanuni! Naomba kama kuna mtu mwenye job description ya katibu wa Bunge atuwekee hapa jamvini ili tujue katibu ana mamlaka gani na anawajibika kwa lipi?
Hizi kanuni za bunge zimekuwa zikiongelewa sana na Mama Makinda na sasa Katibu wa bunge kama some sort of holy gray! Na kuna uwezekano kabisa kuwa walipania kuzipindisha lakini kwa bahati mbaya hawa wabunge 'wapya' ambao wengi wao ni wanasheria wamewazidi 'maarifa' plus wameonesha kuwa kanuni za bunge ni taratibu na lazima zimesomwe pamoja na sheria mama ya nchi yaani katiba.
Mis-calculation ya kuweka Spika, naibu spika na katibu wa bunge ambao wote si wanasheria ndio mwanzo wa sokomoko bungeni. Kashilila aache kuhubiri porojo maana watanzania tumeona zomea zome na mipasho bungeni tofauti kabisa na kipindi kingine chochote hasa kipindi cha Spika Sitta. Kama taifa ni aibu kuona tuliyoona na nadhani ingekuwa busara kwa watu kama wakina Kashilila kuwa na different attitude wanapokaa kwenye viti vya uongozi badala ya kuja na excuses. Mbona kikao alichoongoza Mh. Jenista Mhagama kilikuwa na nidhamu nzuri? Fair play.