Kashilila hukumtendea haki Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashilila hukumtendea haki Lema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dazu, Apr 27, 2011.

 1. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Katibu wa bunge bwana Kashillillah aliita waandishi wa habari kuelezea minyukano iliyojitokeza katika mkutano wa 3 wa bunge hili la 10, aliuleza umma kwamba kilichosababisha ni ugeni wa wabunge na sio udhaifu wa Spika. Alienda mbali zaidi kutolea mfano wa mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema kwamba kitendo chake cha kusema 'funga mlango tupigane' kinatokana na uchanga wake bungeni na kwamba hana wala hajasoma kanuni za bunge. Maoni yangu ni kwamba katibu hajamtendea haki Mhe. Lema kwa sababu
  1. Ni wabunge wengi ambao walijibizana maneno wakiwemo wakongwe na mawaziri (tulisikia wengine wakisema 'atoke nje');
  2. Si kweli kwamba mhe. Lema hana kanuni za bunge;
  3. Kila bunge jipya huja na wabunge wapya lakini haya hajajitokeza huko nyuma;
  Mtazamo wangu ni kwamba yaliyojitokeza ni mwanzo tu wa kuonesha dhahiri kwamba spika wa sasa hakuwa amewiva vya kutosha kuvaa viatu vya Sitta. Aidha kitendo cha ufafanuzi huu kutolewa na katibu wa bunge ni ushahidi mwingine kwamba Spika kashindwa. Naomba kuwasilisha.
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na hoja zako. Katibu wa bunge naye anaanza kucheza karata ya ushabiki, shame on him. Udhaifu wa spika anaupelekea kwa wabunge kadhaaaaaaaaaa kiushabiki.
   
 3. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sasa hata kama wewe ukiwa spika au Dr Slaa awe Spika utashikilia midomo ya wabunge wote ili wasilopoke na kusema fungeni milango tupigane! Mimi naona ni tatizo la kupata wabunge wahuni ambao wanashindwa kuelewa hadhi ya bunge na kuona kama wako kijiweni!
   
 4. Mwathirika

  Mwathirika JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35

  Dazu! CCM ni kundi kubwa kuliko tunavyolitazamia. Mbona hajasema kwa nini Spika alitaka kwenda kinyume na taratibu hizo za bunge anazosema wabunge hawana katika mikoba yao? kwani ndo ulikuwa mwanzo wa hayo yaliyotokea na kuyatolea mfano! Waingereza wanasema ''kama watu hawafikiri unavyofikiri wafanye wafanye unachofikiri''. Tutawapeleka kunakotakiwa.
  Ahsante
   
 5. Mwathirika

  Mwathirika JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Lugha ya uungwana inatokana na mazingira ya uungwana, hao jamaa zako hawana uungwana. Huwezi kucheza lizombe unapopigwa mdumange!
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nina shaka na uhalisia wa udaktari wa Dr Thomas Kashilila. Anasema asilimia sabini ya wabunge ni wapya bungeni na wengi ni vijana hivyo hawajui au hawajazoea kanuni. Sioni mantiki ya kuwa mgeni na kutokukua kanuni ikiwa zimeandikwa kwa Kiswahili na wabunge wanajua kusoma.

  Kwa maoni yangu wabunge wapya na hasa wa Chadema wameonesha uelewa na matumizi makubwa ya kanuni kuliko wa zamani na hata kuliko Spika aliyekaa bungeni muda mrefu kuliko wabunge wote.

  Yaani, kuna wabunge wakongwe na wapya ambao hawazijui kanuni, na kinyume chake. Pia kuna sisi wengine ambao hata siyo wabunge lakini tunazijua kanuni hizo kuliko wabunge.

  Kashilila arejee namna kanuni zilivyokiukwa wakati wa chaguzi mbalimbali ndani ya bunge. Pia athibitishie umma kwamba wote wanaozomea bungeni na kupiga makofi kwa mkumbo kwamba ni wabunge wapya
   
 7. J

  JABEZ Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza nadhani aliyetamka maneno 'funga milango tupigane' sio Lema, ni mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe Haule. Sielewi kwanini lema anahusishwa na ile kauli
   
 8. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijui lini tutaacha unafiki!lema amekisema kilichokuwa moyoni bila unafiki,matukio kama haya sio mageni duniani,hata bunge la israel panachafuka hadi wabunge hutolewa nje na maafisa usalama.
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  gharrrri nini wahuni hata mafisadi wamo hilo ndio tatizo la ****** kwenda kuwapgia kampeni Chg RA,EL
   
 10. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijui lini tutaacha unafiki!lema amekisema kilichokuwa moyoni bila unafiki,matukio kama haya sio mageni duniani,hata bunge la israel panachafuka hadi wabunge hutolewa nje na maafisa usalama.
   
 11. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hahahahahaha! Kweli chadema mnachekesha mnatetea hadi ujinga!
   
 12. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huyo mdigi kakurupuka. Kama ni uzoefu mbona siku ya kufungua bunge tulisikia maneno kitao ya kijingajinga tena kwa hao wabunge wa ccm? Alwayz wanaongea mipasho. KASHILILA TUNAONA NA KUSIKIA WENYEWE SPIKA AMEPWAYAAAA USIJIFANYE KUWA MSEMAJI WAKE KABWAYA
   
 13. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  hahahahaha hajatendewa haki kivipi? nafikiri mtu akiwa mbunge lazima ajijengee ustaarabu fulani: awe na hadhi fulani.
  Lema ni Mbunge mzuri lakini bado ana mambo ya kijiweni sana, nimemshuhudia katika maeneo mengi pamoja na kwenye mijadala mbalimbali.
   
 14. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Je PhD yake inafanyakazi yake hapo bungeni! Basi ndo kumkuta mtu kama huyu kugeuka kama kada wa ccm kwani yuko underemployed! Nashauri wampeleke UDOM akatoe lecture halafu wanafunzi watatupa feedback!
   
 15. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijui lini tutaacha unafiki!lema amekisema kilichokuwa moyoni bila unafiki,matukio kama haya sio mageni duniani,hata bunge la israel panachafuka hadi wabunge hutolewa nje na maafisa usalama.
   
 16. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Come to think of it!!!! .........hivi huyu jamaa ni daktari wa masuala gani?
   
 17. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tulikua na makatibu wa bunge akina George Mlawa, Kipenka Musa, nk. Hatukuwasikia kulisemea bunge. Hivi Katibu ni msemaji wa bunge?
   
 18. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Daktari! My poor foot!
   
 19. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katibu wa bunge ni MBWA na spika nimfugaji MBWA japo naye ni MBWA kwani anao wanaomfuga hivyo hawana budi kuteteana kwani Wabunge wanao ongea ujinga na ushabiki kikada pia kuzomea kama Mh Sophia Simba wao ni wageni ama walitaka Mh Lema aseme ndio mzee.
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Ni hivi majuzi tumesoma kwenye baadhi ya magazeti kuwa Mwanasheria mkuu aliitwa kwenye vikao vya CCM kule Dodoma wakati inafanya madaliko katika safu ya uongozi. Na watu walihoji inakuwaje mwanasheria wa Serikali anashiriki kwenye vikao vya chama cha siasa?

  Sasa Leo Katibu wa Bunge anaita waandishi wa habari na kuanza kuelezea 'upya' wa wabunge pamoja na madai kwamba baadhi yao hawazijui kanuni! Naomba kama kuna mtu mwenye job description ya katibu wa Bunge atuwekee hapa jamvini ili tujue katibu ana mamlaka gani na anawajibika kwa lipi?

  Hizi kanuni za bunge zimekuwa zikiongelewa sana na Mama Makinda na sasa Katibu wa bunge kama some sort of holy gray! Na kuna uwezekano kabisa kuwa walipania kuzipindisha lakini kwa bahati mbaya hawa wabunge 'wapya' ambao wengi wao ni wanasheria wamewazidi 'maarifa' plus wameonesha kuwa kanuni za bunge ni taratibu na lazima zimesomwe pamoja na sheria mama ya nchi yaani katiba.

  Mis-calculation ya kuweka Spika, naibu spika na katibu wa bunge ambao wote si wanasheria ndio mwanzo wa sokomoko bungeni. Kashilila aache kuhubiri porojo maana watanzania tumeona zomea zome na mipasho bungeni tofauti kabisa na kipindi kingine chochote hasa kipindi cha Spika Sitta. Kama taifa ni aibu kuona tuliyoona na nadhani ingekuwa busara kwa watu kama wakina Kashilila kuwa na different attitude wanapokaa kwenye viti vya uongozi badala ya kuja na excuses. Mbona kikao alichoongoza Mh. Jenista Mhagama kilikuwa na nidhamu nzuri? Fair play.
   
Loading...