Kashfa ya kutisha jeshi la Polisi

Na hiyo ni batch moja, kumbuka walifukuzwa ili wengine waingie, zamu yao wapigwe vipara, warushwe kichura then wana ambiwa hawafai.
Haki ya nani inatia uchungu na sometime inachekesha hapo kwenye red...mwema ni shemeji yake prezidaa,chagonja yeye ni nani?mbona wanafaidi sana haya madeal bila hofu yoyote?
 
Hii bado ni ishu ndogo sana..... Kuna madudu mengine makubwa lakini hawashughulikii.
Anyway, Mwema asibakie kutoa namba, bali akafanye mchakato wa kuhakikisha vijana hao wanarudishiwa fedha zao.
Na hao vijana nao hawafai kabisa kuwa wana usalama...... Kwa kitendo kutoa rushwa ili wawe mapolisi. Wanajua wakishavaa gwanda watazirudisha vipi
 
Mwema anza na polisi wa hapo chuoni waliokuwa geitini siku hiyo wanatakiwa wahojiwe, ilikuwaje wakaruhusu mabasi matatu yaingie chuoni, huo ni udhaifu. Waliowapokea na kuwapa sehemu ya kulala, waliotoa chakula wote wanahusika. Ni nani alihidhinisha yote hayo yafanyike?
 
Wewe unashangaa, polisi wanatapeliwa kituoni kwake pa kazi. OCD wa Ilala aliwahi kutapeliwa ofisini kwake na mjanja tena polisi mwenzake. Jamaa alitayarisha Tsh 2million Cash akakabidhi nyuma akaachiwa dhaabu feki. Chezeya Bongo
 
Tumeshasema mara nyingi Mwema, Chagonja na wenzao waondolewe lakini kuna mtu anawalinda. Waacheni tu yaishe.
Hata wakiondolewa haitasaidia lolote!Sanasana wengine wataona ndiyo nafasi yao ya kula!

Kwa taarifa yako hapo ni mwanzo tu,bado kuna hongo ya kupangiwa kwenye ulaji zaidi.Kuna mikoa ambayo haupangiwi hadi uhonge!Na si mikoa tu,mfano askari wanapenda pia kupangiwa sehemu ambazo zinahusisha uvushaji wa magendo na maliasili,ama usafirishaji wa magendo na madawa ya kulevya nk.Pia hata wengine hupenda kupangiwa mikoa yenye ulaji wa kutosha kwenye traffic police.The system is rotten!

Namna ya kudeal na tatizo hili si kubadilisha hao kina Mwema na Chagonja,tatizo ni ccm na mfumo tulionao(chini ya ccm),period!

Huwezi kuwa na rushwa ndani ya chama chenye nguvu kuliko serikali halafu utegemee eti rushwa itaisha serikalini kwa kufuta viongozi hapa na pale.
 
Hata wakiondolewa haitasaidia lolote!Sanasana wengine wataona ndiyo nafasi yao ya kula!

Kwa taarifa yako hapo ni mwanzo tu,bado kuna hongo ya kupangiwa kwenye ulaji zaidi.Kuna mikoa ambayo haupangiwi hadi uhonge!Na si mikoa tu,mfano askari wanapenda pia kupangiwa sehemu ambazo zinahusisha uvushaji wa magendo na maliasili,ama usafirishaji wa magendo na madawa ya kulevya nk.Pia hata wengine hupenda kupangiwa mikoa yenye ulaji wa kutosha kwenye traffic police.The system is rotten!

Namna ya kudeal na tatizo hili si kubadilisha hao kina Mwema na Chagonja,tatizo ni ccm na mfumo tulionao(chini ya ccm),period!

Huwezi kuwa na rushwa ndani ya chama chenye nguvu kuliko serikali halafu utegemee eti rushwa itaisha serikalini kwa kufuta viongozi hapa na pale.


Unafikiri mfumo wa jeshi la polisi utakuwaje CCM ikiondolewa madarakani?
 
Unafikiri mfumo wa jeshi la polisi utakuwaje CCM ikiondolewa madarakani?
Sijui itakuwaje,inabidi wanaotaka kuingia madarakani wali address hilo.Inawezekana utaratibu uko sawa tu sema rushwa imekuwa kama utamaduni wetu.Chama kinachotaka madaraka ni lazima wa address hizi issue na kueleza kiunagaubaga kuwa ni kwa kivipi wata deal nazo.

Mfano labda wazungumzie kuhusu sheria kali za kukabiliana na rushwa.Mifumo ninayoiuzungumiza mimi ni ya rushwa,mifumo ya kiutendaji(as it is supposed to),inawezekana kuwa ni mizuri tu,lakini rushwa ni mfumo mbaya unaoweza kuharibu mfumo wowote ule ambao uko perceived kwamba ni mzuri.

La muhimu ni wanaotaka kuingia madarakani kusema wazi ni kivipi watadhibiti rushwa!
 
Niliwahi kushuhudia mwanamama aliyeenda kituo cha polisi huku akilia na kulalamika mwanaye mdogo amebakwa, na mbakaji wala hayupo mbali na sehemu hiyo hivyo anahitaji askari wa kwenda kumkamata mtuhumiwa. Kilichonishangaza ni pale askari aliyekuwa mapokezi bila aibu wala kujali watu tuliokuwa pale na shida zetu alimuuliza yule mama,una bei gani tukusaidie mama..??Nilishikwa na hasira na kujiuliza maswali mengi ambayo sikuwa na majibu mpaka leo ndio nimepata jibu kwa nini yule askari alisema vile..
 
Nchi yetu inasubiri masiha 2015,MAIGIZO YA SERIKALI YA CCM KAMWE HAYAVUMILIWA TENA KWA MTINDO WA FUNIKA KOMBE MWANAHARAM APITE.
 
Hiii kweli hii! mbona napata kigugumizi kuamini. Kama kweli:
Mwanafunzi: Hivi polisi aliyeingia mafunzo kwa kutoa rushwa kwa polisi na kufundishwa na polisi hao hao waliochukua rushwa kwao watatoa product ya aina gani kuhudumia umma? nzuri or mbaya?

Haya nimekutafunia jawabu na ukishindwa kujibu wewe mjinga na kwa ujinga huu hata wewe hujui kuwa umjinga hivyo.
 
Kama M/Kiti wa CCM aliwaambia wajumbe kwenye mkutano mkuu kwamba sasa wasitegemee Polisi kuwasaidia katika harakati za M4Change, sasa ulitegemea hao Polisi watapata wapi pesa walizokuwa wanapata hapo awali? Lazima watafute njia nyingine za kupata mlo na zingine zinakuja zipo njiani tele tuwe waangalifu zaidi.:israel:
Bye.
 
mtu anahonga laki 8 ajiunge polisi wakati akishakua polisi kamili hatapata hiyo laki 8 mshahara kwa mwezi....huo ni ujinga
 
Tusisahau hili SHORT-CUTS WILL ALWAYS CUT YOU SHORT!Kama chuo kikuu uliingia kwa merit kwa nini wataka utoe hongo uingie CCP wakati mshahara wa Polisi hata GRADUATE ni kiduchu?Ni ili uje urejeshe pesa yako kwa kuchukua rushwa
Kwa kila aliyetapeliwa sitoi pole nasema IT SERVES YOU RIGHT!
Njia za panya zitatumaliza!Lakini ninyi ni wa BABA YENU ibilisi-CCM, baba wa RUSHWA,UFISADI,NA UCHAFU SYSTEMIC!
 
Yaliyopo Polisi ni zaidi ya haya ongea na polisi wenyewe uone HOW ARE THEY PINCHED katika ruhusa za likizo, masomo, katika kuomba mikopo kwenye mabenk.

Ushauri wa bure! Polisi wamo ktk jamii ambayo rushwa ni style ya maisha ya kila siku, si rahisi kukwepa kumezwa na jamii ingawa wao ni Crime specialists

Nini kifanyike; tutalaumu, tutahukumu sababu hatufikirii kuwa Taifa liko katika transitional period from SOCIALISM TO CAPITALISM.Hivyo kila mmoja si kutoka chama tawala wala Upinzani wanajaribu kupunguza gap la aliyenacho na asiye nacho.

Wazalindo waliobaki baada ya Baba wa Taifa ni wachache( Almost negligible till you collect them by MAGNETIC)
 
Polisi ni sehemu ya jamii yetu, jamii yetu yenyewe inaabudu rushwa kwa hiyo mi sishangai maana jamii yetu yote ndo ilivyo. Mbona hamshangai wajumbe wa NEC ya CCM kupatikana kwa rushwa wakati hiki chombo maamuzi yake ni makubwa kwa nchi yetu?

Viongozi wa Jeshi la polisi wanateuliwa na Mwenyekiti wa wala rushwa;
Lipi la kushangaza?
Kwa ujumla jeshi la polisi na CCM yake vyote vimeoza; mahakama ndo kidogo bado kuna aibu lakini nao sijui tunakokwenda.

Jeshi pekee hapa nchini ni Jeshi la wananchi tu!
 
Back
Top Bottom