Kashfa ya kutisha jeshi la Polisi

Kashfa ya kutisha jeshi la Polisi

Na hao nao wakamatwe kwa kuwa ni watoa rushwa...unatafuta kazi kwa kutoa laki 8/milioni wakati kazi yenyewe ni maghumashi? Ama hakika Tanzania ni full mizengwe na huu utaratibu ni KAWAIDA saaaaaaaaaaaaaaaaaaaana na hata hawa wakubwa wenyewe wanakula hizi hela ama wanawapeleka watu kwa MEMO tu kibao ndo mfumo wa Tanzania. Hapa IGP kachezeshwa (hakulambishwa chake) ndo maana anashikilia kidedea..tsh
 
Mkuu kwa hali tuliofikia Tanzania leo bila ya kutoa rushwa iwe ya cash au ngono kupata kazi ni shughuli pevu..! Sio Polisi tu hata ajira kwenye sekta nyingine zinapatikana kwa mtindo huo wa rushwa au kujuana.. So kwa mtazamo wangu hauko sahihi kumuhukumu alielazimishwa na jamii iliomzunguka kutoa rushwa ili apate uwezo wa kujikimu..

Kwenye kulima ndio hakufai kabisa mkuu.. Umeona wakulima wa korosho wanavyolilia hela zao..? Umeona wakulima wa mahindi Rukwa walivyolalamika mahindi yao kuoza kwa kuwa hawana pa kuyaweka na wanalazimishwa kutokuuza mazao yao kwa wafanyabiashara wa kigeni ambao wanalipa hela nyingi..?

Umeona wakulima wengi huko mikoani wakilalamika kupata hasara kwa kuwa au wamecheleweshewa mbolea au wameuziwa mbolea fake ambayo ilipelekea kuharibu mazao yao..?

ndugu yangu uongo sasa mpaka police mahakamani bungeni na kote kwenye utawala ....umeme mgao utaambiwa matengenezo ya miundo mbinu......unanikumbusha no buku no koton by mr mapesa
 
Haya bwana Hoseya umepata mahali pakuanzia.hapa ndipo mahali pakumuvalisha paka kengere.onyesha vitu vyako baba.
 
Tumeshasema mara nyingi Mwema, Chagonja na wenzao waondolewe lakini kuna mtu anawalinda. Waacheni tu yaishe.
Hakika anayewalinda nae ana mgao wake hili deal si la kitoto...check hii watu 200 x 800,000 kila mmoja=zaidi ya 160,000,000/=milioni....ama kweli bongo maisha rahisi sana!!!Mwema.chagonja na wengineo endeleeni kufaidi nchi yenu hii.
 
Hayo Makampuni ya Mabasi si ndiyo yenye ushahidi wa majina ya waliotapeliwa. Kila risiti ina jina na contact
 
ndugu yangu uongo sasa mpaka police mahakamani bungeni na kote kwenye utawala ....umeme mgao utaambiwa matengenezo ya miundo mbinu......unanikumbusha no buku no koton by mr mapesa

Mkuu hilo la uongo mbona limekuwa dhahiri..! Wananchi wengi wanajua serikali ni waongo.. Wamepoteza credibility ya kuaminiwa na wananchi..
 
Polisi ni sehemu ya jamii yetu, jamii yetu yenyewe inaabudu rushwa kwa hiyo mi sishangai maana jamii yetu yote ndo ilivyo. Mbona hamshangai wajumbe wa NEC ya CCM kupatikana kwa rushwa wakati hiki chombo maamuzi yake ni makubwa kwa nchi yetu?

Umenena
 
Tatizo ni sisi wenyewe. Tunalalamika rushwa rushwa wakati ndio wakwanza kutoa. Vita ya rushwa ni ngumu sababu aliyemadarakani kaingia kwa rushwa pia.
 
Hivi najaribu kupiga picha maisha ya askari yalivyoduni halafu unakwenda kutoa rushwa ili upate hiyo kazi ya uaskari Tanzania?
 
Sasa kama hata Polisi wanaingizwa kwa rushwa au wanatoa Rushwa ili wapate hizo nafasi, hivi ni nani atayebaki kweli kwenye hii ishu ya rushwa?? Nadhani ni mimi tu

jibu ni M4C upepo wa kisulisuli na kimbunga cha CHADEMA 2015 utafagia uchafu wote huu na taifa litairudishia heshima yake ya enzi za mwalimu!
 
Utaratibu wa sasa mimi binafsi siuung mkono kabisa...
Kabla ya utaratibu huu wa sasa wa jinsi ya kujiunga na jesh la polisi... zamani watu walikuwa wakifanyiwa interview wilayan baada ya hapo wanakwenda mikoani.... Ukifanikiwa mkoan ndo hapo safar yako ya kwenda MpA...inakamilika.
 
Dawa ya upumbafu kama huo ni wetu sisi wananchi hasa walio zezeta katika kupambana na maisha yao, naomba adhabu kubwa ianzie kwa hao vijana ambao ni vilaza wanao amini uwezi fanikiwa bila hongo, na hao ndio watakuwa wa kwanza kuomba rushwa baada ya kumaliza mafunzo, nadhani elimu na uraia inatakiwa kwa vijana wote, huko wapi uzalendo wa nchi yao,je huko police kuna biashara gani hadi utoe laki nane, rushwa itakwisha siku watoa rushwa wataacha kutoa, waombaji wapo siku zote,
Amka vijana
Amka tanzania

Eeee watanzania naomba kwa heshima mnipatie nafasi ya kushika nchiii hii kwa siku sitini tu nikishindwa mnifukuze kazi nawajua hawa na ni saizi yangu
 
Tumeshasema mara nyingi Mwema, Chagonja na wenzao waondolewe lakini kuna mtu anawalinda. Waacheni tu yaishe.

kwa akili zangu ndogo mzee mwanakijiji nimekuelewa,waacheni tu yapite!teh teh aaahhaaaaaaaahhhhhaaaa nacheka kimaandishi kiuhalisia tofauti
 
Hakika anayewalinda nae ana mgao wake hili deal si la kitoto...check hii watu 200 x 800,000 kila mmoja=zaidi ya 160,000,000/=milioni....ama kweli bongo maisha rahisi sana!!!Mwema.chagonja na wengineo endeleeni kufaidi nchi yenu hii.

Na hiyo ni batch moja, kumbuka walifukuzwa ili wengine waingie, zamu yao wapigwe vipara, warushwe kichura then wana ambiwa hawafai.
 
Sasa kama hata Polisi wanaingizwa kwa rushwa au wanatoa Rushwa ili wapate hizo nafasi, hivi ni nani atayebaki kweli kwenye hii ishu ya rushwa?? Nadhani ni mimi tu

sasa mtu kafeli form four unategemea atafanya nini?
 
Back
Top Bottom