Polisi.....Polisi.....Polisi.....Jeshi la Polisi Tanzania!!!! Kero tupu, makashfa yao makubwamakubwa ya kikatili kwa raia!
Natamani siku moja tupate serikali mpya iliyo makini, hizi kero zitabaki historia.
Hii tuhuma ni nzito serikali ilifanyie kazi. Watuhumiwa ni jeshi la polisi sababu chuo cha polisi kilihusika kuwapokea na kuwapatia huduma za awali kwa malipo ya pesa taslim, sasa huyu msemaji anapowataka walalamikaji kutuma UJUMBE (yaani sms) kwa IGP inaleta picha gani? yaleyale ya tume ya .... kifo cha Mwangosi. Kama nakumbuka vizuri, mwaka 2001 pale Kituo cha polisi msimbazi mishahara ya polisi iliibiwa palepale ndani, yaani walijiibia wenyewe hatukusikia anafungwa mtu.
Sasa tatizo limekua, sasa ni janga la kitaifa. Kila intake inapoingia chuoni huwa ina taratibu zake, kama idadi,bajeti n.k. sasa hao watu zaidi ya 200 walipitaje getini pasi kuhakikiwa majina yao, na chakula walichopewa (naamini hawakulala na njaa) bajeti yake iliidhinishwa na nani? Mimi nafikiri kama shida ni ushahidi basi huyo mkuu wa chuo pamoja na Komba wanatosha.
Lakini pia huu ni udhaifu wa wazi wa mkuu wa jeshi la polisi. Kama Rais aliyemteua akimwacha, basi hili ni pigo jingine kwa seriksli yake. Mkuu wa chuo asisubiri kufukuzwa nashauri akabidhi tu ofisi aondoke zake lakini ashitakiwe pia