Barabaraya18,
Kumbe wewe kigeugeu kweli aisee; hivi kweli unapoandika huwa unajua unachoandika? Tulianzia kwenye talaka tatu ukasema upewe reference, tukakupa ukakimbia. Sasa unakataa kukubali uliyoandika mwenyewe eti hadi tukupe reference. Siyo wewe ulieandika hivi?
halafu leo unadai hivi:
Huoni kabisa kuwa unatudanganya hapa. Kama una maana yako nyingine moyoni iwe njema au mbaya sina haja ya kuijua lakini usitufanye kama watoto wadogo hapa.
Nimeongezea sehemu hii makusudi: Swala la kujua dhehebu la mtu siyo muhimu kabisa katika jamii yetu. Tunaweza kujua kuwa ni mwislamu au mkiristo lakini hatuna haja ya kujua dhehebu ndani ya uislamu au ukristo wa mtu. Ni kama ambavyo huwa hatuhitaji kujua makabila ya watu.