Kariakoo pako hovyo hapaeleweki kama sio soko kuu la nchi na majirani

ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
5,511
2,034
Nimepita leo kariakoo inasikitisha kweli hata pa kupita hamna kila sehemu chinga wamepanga vitu vyao.

Hivi hata kuwapanga chinga hatuwezi. Dar ni hub zaidi ya nchi 8 zinategemea pale hivi tumeshindwa kweli kutengeneza sehemu ya kuvutia iwe soko la kuwavutia wafanya biashara wa nchi zaidi ya nane na soko letu la ndani hadi tunakua na eneo la hovyo lisiloeleweka kama kariakoo.

Hivi sisi tunaweza nini
 
Hakuna tuwezacho zaidi ya Ulevi, Ngono, Umbea, Rushwa, wizi, uhujumu uchumi na kubishana Simba na Yanga.

Uafrika hasa utanzania ni laana.
 
Nimepita leo kariakoo inasikitisha kweli hata pa kupita hamna kila sehemu chinga wamepanga vitu vyao.

Hivi hata kuwapanga chinga hatuwezi. Dar ni hub zaidi ya nchi 8 zinategemea pale hivi tumeshindwa kweli kutengeneza sehemu ya kuvutia iwe soko la kuwavutia wafanya biashara wa nchi zaidi ya nane na soko letu la ndani hadi tunakua na eneo la hovyo lisiloeleweka kama kariakoo.

Hivi sisi tunaweza nini
Kariakoo kuna soko hapo, ila naona soko limeelemewa, na hatuna mipango ya kujiongeza.

Sasa hivi panatakiwa kujengwa soko jipya Kibaha uko, kubwa, mji utanuke kuelekea huko.
 
Fulsa ni kubwa sana ila tunaichezea
 
Sio hilo tu mkuu pia tunahitaji a single central hub ya kusafirishia mizigo ili kuwarahisishia wanunuzi wa bidhaa kutodhurula wanapotaka kusafirisha mizigo yao.
 
Nimepita leo kariakoo inasikitisha kweli hata pa kupita hamna kila sehemu chinga wamepanga vitu vyao.

Hivi hata kuwapanga chinga hatuwezi. Dar ni hub zaidi ya nchi 8 zinategemea pale hivi tumeshindwa kweli kutengeneza sehemu ya kuvutia iwe soko la kuwavutia wafanya biashara wa nchi zaidi ya nane na soko letu la ndani hadi tunakua na eneo la hovyo lisiloeleweka kama kariakoo.

Hivi sisi tunaweza nini
Si serikali ikitaka kuwapanga watu wanakuja juu wanaona serikali haiwapendi , last year walifanya kuwaondoa kando kando ya barabara raisi akatukanwa hana huruma na raia haya sasa ameacha

Ila kitendo ambacho sikukifurahia nilichukizwa ni kuwaondoa kimabavu watu wanavunjiwa meza zao, bidhaa zinaharibiwa kitu ambacho sio sahihi
 
Kariakoo kuna soko hapo, ila naona soko limeelemewa, na hatuna mipango ya kujiongeza.

Sasa hivi panatakiwa kujengwa soko jipya Kibaha uko, kubwa, mji utanuke kuelekea huko.

Ilitakiwa wagawe kariakoo kwa branches, kwa mfano hapo iliko kwa sasa ibakie kua sehemu ya nguo, mashuka, mapazia, halafu wajenge kariakoo nyingine kibaha huko sasa itakua sehemu ya vifaa vya kielektroniki, sijui simu, redio, tv, na vifaa vyote vya umeme hadi vifaa vya mifumo ya umeme, na tawi lingine la kariakoo lijengwe labda vikindu au kisarawe au bagamoyo na huko ndio wanaweka maduka makubwa ya madawa ya binadamu , mifugo na kilimo, na wangechagua tawi moja wapo hapo wakaweka vifaa vya ujenzi, na kote kukawa na barabara zinazofikika kirahisi na kote wangeruhusu design ya mahotel ili mfanyabiashara achague atalala wapi lakini pia kampuni za usafirishaji zingefungua maofisi huko kote ili mfanyabiashara ananunua anajua mzigo wake apeleke wapi, kikubwa miundombinu tu ya barabara iwepo vizuri na hizo mwendokasi zifike kote ambako kuna branches za matawi yote ya kariakoo, mji ungesambaa vizuri na kupangika vyema na ingesaidia sana kua na unafuu kua mtu anajua bidhaa fulani nitapata sehemu fulani lakini plan viongozi hawana kabisa hawaijui kesho ya nchi yao ni ipi na itakuaje baadae
 
Nimepita leo kariakoo inasikitisha kweli hata pa kupita hamna kila sehemu chinga wamepanga vitu vyao.

Hivi hata kuwapanga chinga hatuwezi. Dar ni hub zaidi ya nchi 8 zinategemea pale hivi tumeshindwa kweli kutengeneza sehemu ya kuvutia iwe soko la kuwavutia wafanya biashara wa nchi zaidi ya nane na soko letu la ndani hadi tunakua na eneo la hovyo lisiloeleweka kama kariakoo.

Hivi sisi tunaweza nini
TANZANIA KILA KITU SIASA
 
Back
Top Bottom