Ushirikiano wa kina na China unaweza kuwa suluhisho la changamoto kuu za nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1703057984978.png


Katika muda wa muongo mmoja uliopita, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika umekuwa ukiimarika, huku China ikifungua fursa nyingi za kiuchumi na kibiashara kwa nchi za Afrika. Wakati China ikifanya hivyo kwa matarajio ya kuziinua kiuchumi nchi za Afrika, changamoto mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kwa nchi za Afrika kushindwa kutumia fursa hizo ipasavyo.



Moja kati ya changamoto kubwa zilizopo katika kutafuta maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za Afrika, ni kwamba nchi za Afrika zinashindwa kutumia ipasavyo fursa za kujiendeleza kutokana na kukosa uwezo wa ndani wa kutumia fursa hizo. China imekuwa ikitoa fursa mbalimbali kwa nchi za Afrika ikiwemo soko, mitaji na hata ujuzi, lakini kutokana na kuwa na msingi dhaifu wa kutumia fursa hizo nchi za Afrika bado hazijanufaika vya kutosha na kuweza kupata maendeleo yanayohitajika.



Tunaweza kuchukulia mfano wa sekta ya kilimo, ambayo nguvu kazi nyingi ya Afrika inatumika, licha ya China kufungua soko lake kwa zaidi ya asilimia 95 ya mazao ya kilimo kutoka Afrika na kuweza kuingia bila ushuru, ni sehemu ndogo sana ya mazao hayo yanaingia kwenye soko la China. Sababu kubwa ni kuwa nchi za Afrika hazina uwezo wa kutosha wa kufanya uzalishaji kufikia viwango (quality) na kiasi (quantity) kinachokidhi mahitaji ya soko.



Uzuri ni kwamba kwenye mkutano wa majadiliano kati ya China na viongozi wa nchi za Afrika uliofanyika Agosti 25, 2023 mjini Johannesburg chini ya uenyekiti wa pamoja wa Rais Xi Jinping wa China na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Xi alitangaza mipango mitatu inayohusiana na maendeleo ya kilimo, maendeleo ya viwanda na maendeleo kuhusu ujuzi barani Afrika. Lengo mapendekezo hayo na mipango hiyo ni kuhakikisha Afrika inakuwa na uwezo halisi wa kutumia fursa zinazotolewa na China, na hata zinazoweza kupatikana sehemu nyingine.



China imepiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo ya viwanda, sekta ya kilimo na hata mafunzo ya ufundi stadi. Lakini pia hayo ni maeneo ambayo nchi za Afrika ziko nyuma zaidi ikilinganishwa na sehemu nyingine duniani, kama hakutakuwa na maendeleo thabiti kwenye maeneo hayo, sio tu kwamba nchi za Afrika zitashindwa kutumia vizuri fursa za kiuchumi zinazotolewa na China au dunia kwa ujumla, lakini pia itakuwa vigumu hata kwa nchi za Afrika zenyewe kuwa na mafungamano ya maana kiuchumi.

Lakini tukiangalia kwa undani zaidi tunaweza kuona kuwa ushirikiano kwenye sekta ya kilimo huenda ni muhimu zaidi kwa kuwa unatatua changamoto moto za moja kwa moja za sasa na hata za muda mrefu. Sekta ya kilimo ikiboreshwa ni wazi kwamba bara la Afrika zinaweza kuuza zaidi mazao ya kilimo, lakini pia tatizo la usalama wa chakula linalosumbua nchi mbalimbali za Afrika pia linaweza kutatuliwa. Tofauti na sekta ya viwanda yenye utatanishi mkubwa ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa wa fedha, teknolojia na hata watu wenye ujuzi, sekta ya kilimo ina mazingira ambayo hayahitaji nguvu kubwa ya kuipa msukumo kama ilivyo sekta ya viwanda.



Rais Xi alisema kwenye mkutano huo kuwa China itazindua mpango wa China kuhimiza maendeleo ya kilimo na itaisaidia kupanua mashamba ya nafaka na kuhimiza makampuni ya China kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo barani Afrika. Kwa kufanya hivi bara la Afrika litaweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja, yaani kukabiliana na tatizo la usalama wa chakula, na kuongeza mazao ya kilimo kwa ajili ya soko la nje.
 
Nchi za afrika Tume laaniwa kilakitu tunacho ila Viongozi wetu hawana ule uzalendo wa kweli, wao ni maneno matam tu ila kiutendaji ni sifuri, Nasisi WANA NCHI tume lala usingizi wa pono tukiamka tunatia kaunafki kidogo tuna lala tena Ee Mungu tusaidie
 
Back
Top Bottom