MUSHEKY
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 2,812
- 2,754
Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.
Imepita zaidi ya mwaka na ushee hivi toka Soko Kuu la Kariakoo ambalo ni kitovu cha biashara katika nchi yetu na nchi zinazotuzunguka kuteketea kwa moto.
Sikumbuki kama tuliambiwa sababu ya kuungua soko hili wala hatua zilizochukuliwa kwa yeyote aliyehusika hadi leo, ninachokumbuka iliundwa Tume na Waziri Mkuu kuchunguza undani wa sakata hili ila kwa kuwa mambo ni mengi labda uchunguzi bado unaendelea.
Bila kujali yote hayo niipongeze serikali yako kwa kulikarabati na kulitanua maradufu soko hili, bila shaka ni jambo la kupongezwa sana.
Lengo la uzi huu ni kukuomba kama ikikupendeza baada ya kukamilika soko hili kubwa lenye kubeba taswira na uchumi wa nchi yetu, basi wasije wakakuhadaa wenzetu wachache wakafanya udalali kwa wanaoitwa wawekezaji na kuwaacha mamia ya wazawa wakiendelea kukimbizana na mgambo kwenye kingo za barabara.
Nikukumbushe tu Rais, soko hili kabla ya kuungua lilikua limebeba wazalendo kwa asilimia mia moja, tena wale wasio na connection yoyote hivyo tunatarajia kuwaona wakirejea bila blabla na replacement yoyote.
Nimalzie tu kwa kusema sina taarifa yoyote inayosema soko hilo kubwa na la kisasa litapewa wawekezaji na kipande kidogo watapewa wazawa ili kuwafumba macho laahasha! Nimejaribu tu kukushauri kile ninachojisikia ili na mimi nitimize wajibu wangu.
Hao mabwana wakubwa wameshakula na kusaza, tafadhali watuachie makombo yetu.
Sent from my M100 using JamiiForums mobile app