Karamagi Na Kikao Cha Wanakagera

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
60
Jumatano tarehe 27.11.2007 pale diamond Jubilee kulikuwa na kikao cha wanakagera.

Dhumuni la kikao lilikuwa ni kuchangia maendeleo ya mkoa wa Kagera na mgeni rasmi alikuwa awe mh Rais Kikwete ila hakuweza kuhudhulia na akawakilishwa na Mh Edward Lowasa.

Mh. KARAMAGI ALICHANGIA kiasi cha Tshs 50,000,0000/= kama sijakosea.

SWALI JE YEYE KAMA WAZIRI kiasi hicho cha hela anakitoa wapi?????? Je ni mshahara wake wa muda gani.

Watu wengi walihudhulia akiwemo Ritta ambaye alimuwakilisha Mh. Reginald Mengi.

Mimi ambalo limenichanganya na naomba hoja zenu ni Mh. KARAMAGI KUCHANGIA KIASI KIKUBWA HIVYO CHA PESA WAKATI KUNA TUME YA KUCHUNGUZA MKATABA WA MADINI NA UNAMUHUSU YEYE HASWA.
 
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha wakwetu zinasema kwamba. Karamangi alikuwa ametoa milioni 10, lakini PM lowassa akamuomba na kumsihi aongoeze nyingine 10. Kwa hiyo karamangi alitoa milioni 20. Aliyesema milioni 50 ni mzushi kwa hilo. Bilioni 1.4 zilikusanywa siku hiyo ikiwa ni wadau wengi kuchangia pamoja na kununua mabag mengi ya senene kwa mamilioni ya fedha.
 
Karamagi ni mfanyabiashara mkubwa sana hata kabla ya kuwa mbunge na Waziri. Pesa zake ndizo zilizomwingiza kwenye siasa, kwa hiyo wala sishangai kusikia kachangia kiasi hicho kikubwa cha fedha!

Wanasiasa wetu wa siku hizi wote ni wafanyabiashara. Yale maadili ya viongozi ya enzi za Nyerere ya kiongozi kutoruhusiwa kuwa hata na nyumba ya kupangisha hayapo tena na yameshapitwa na wakati.
 
karamagi ni tajiri mkubwa sana mwenye TICTS NA VERTEX ...hata angetoa milioni 100 singeshangaa..kwani hamjui pamoja na nazir kuwa waziri hakosekani kwenye ofisi yake binafsi ya biashara kila siku kupiga mzigo ..anatumikia biashara zake na serikali at the same time ..na ndio hasra ya kuwa na watu kama nazir na rostam kwenye serikali..

ehee na huyo RITTA alimuwakilisha MENGI kama nani....yaani watu wameshabariki VIMADA kwenye jamii ...HIYO NI AIBU KWA WATU WALIOOA NA KUOLEWA WAALIOKUWA PALE!!!
 
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha wakwetu zinasema kwamba. Karamangi alikuwa ametoa milioni 10, lakini PM lowassa akamuomba na kumsihi aongoeze nyingine 10. Kwa hiyo karamangi alitoa milioni 20. Aliyesema milioni 50 ni mzushi kwa hilo. Bilioni 1.4 zilikusanywa siku hiyo ikiwa ni wadau wengi kuchangia pamoja na kununua mabag mengi ya senene kwa mamilioni ya fedha.

Sorry inawezekana sikuipata vizuri, ila haijarishi kachangia kiasi gani tatizo je hizo 20m zinatoka wapi??????????
 
Sorry inawezekana sikuipata vizuri, ila haijarishi kachangia kiasi gani tatizo je hizo 20m zinatoka wapi??????????

MAFISADI WANAANZA KUCHOMOA MAKUCHA YAO TENA BILA AIBU MBELE ZA WATU-MAKUCHA CHOMOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Karamagi ni mfanyabiashara mkubwa sana hata kabla ya kuwa mbunge na Waziri. Pesa zake ndizo zilizomwingiza kwenye siasa, kwa hiyo wala sishangai kusikia kachangia kiasi hicho kikubwa cha fedha!

Wanasiasa wetu wa siku hizi wote ni wafanyabiashara. Yale maadili ya viongozi ya enzi za Nyerere ya kiongozi kutoruhusiwa kuwa hata na nyumba ya kupangisha hayapo tena na yameshapitwa na wakati.

Hivi analipa kodi kwa mwaka kiasi gani kwenye biashara zake zote?
 
1.4 Bil ilikuwa ni mchango wa kuchangia maendeleo ya Kagera katika eneo gani? kama ni mambo ya kijamii ni bora wachangie ili kupunguza maumivu wanayotulete! Tumpongeze kwa mchango ili next time atoe zaidi, ni style ya kuuma na kupuliza!
 
Sasa kuna ubaya gani Karamangi kuchangia hizo 20 milioni? Hata akichangia 50M ni sawa tu ili mradi ni pesa zake.

Sisi muhimu ni kumbana Karamangi kwenye mambo ambayo tunaamini
ametuibia kama watanzania.

Yeye ni tajiri hata kabla hajaingia kwenye siasa kwahiyo kutoa hiyo 20M si jambo la ajabu.

Inabidi tuwasifu wana Kagera kwa kuweza kuchangia pesa zote hizo. Muhimu pia ni kuhakikishia zinatumiwa vyema kwa maendeleo ya mkoa wao.

Maendeleo ya nchi yetu yatatokana na sisi wenyewe kuchangia maendeleo ya huko tunakotoka. Hii ni changamoto kwa mikoa mingine pia.

Kwa hili namsifu Karamangi na wengine wote waliochangia.
 
MAFISADI WANAANZA KUCHOMOA MAKUCHA YAO TENA BILA AIBU MBELE ZA WATU-MAKUCHA CHOMOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Yaani we acha tu BM,
Kuna mtu aliniambia kwamba wengi ya walio enda kwenye hicho kikao chao ni wafanya biashara wakubwa.
Ningekua boss wa TRA ningezikata kodi hizo pesa zote kwanza alafu ndio mwende mkajenge huko kwenu!
Alafu,haya mambo si ndio kama ya Bwana Ben Mkapa?kufanya biashara Ikuru?
Sasa embu wana JF nielewesheni hapa kuna Fair Competition kwenye biashara!?
Wewe waziri tena mfanyabiashara ile nyeti!?Aaah..jamani ss wafanyabiahara wadogo tutatoka kweli?
Niliona watu kwenye Tv jana wana lalamika kuhusu ucheleweshaji wa mizigo bandari ya DSM,wanailaumu hiyo TICS sijui...!!!?
sasa kama hiyo kitu ni ya muheshimiwa sana.....KALAMAGI tunaweza kumuwajibisha ikiwa Rais hawezi hata kumuweka benchi kwenye baraza la mawaziri!
Hivi Wana JF wenzangu TUTAFIKA KWENYE HAKI SAWA!?
 
Mkuu,

Kwanza kodi haikatwi mara mbili, kama hizo pesa zilishakatwa kodi
basi sasa inabidi uvizie hiyo miradi ya maendeleo Kagera ndio ukaikate kodi. Kikawaida kisheria hiyo miradi haikatwi kodi, kwahiyo hapo ungetoka kapa.

Sina uhakika sheria zetu zinasemaje lakini sidhani kama Karamangi
anaweza kuwa executive kwenye hizo biashara zake. Huenda uendeshaji kauacha mikononi mwa watu wengine.
Pamoja na mambo ya Karamangi, lakini tuangalie pia kwamba huwezi kutunga sheria tu kwa ajili ya kumbana mtu mmoja. Kwenye siasa kuna kila aina ya profession, kuanzia wafanyabiashara, walimu mpaka hata changudoa. Sasa unachoweza kufanya ni kuweka njia za kuzuia conflict of interest na sio kuwazuia kabisa maana ukizuia hapo unaweza kujikuta ukawa umemzuia hata mwalimu wa mlimani asirudi kufundisha anapokuwa mbunge. Ndio maana kunakuwa na mambo ya conflict of interest, lakini je TZ yanafuatwa? labda hilo ndilo tatizo.

Inabidi kupata utaratibu mzuri lakini pia hatuwezi kurudi kwenye enzi za Mwalimu ambako hata kufuga kuku ilikuwa ni makosa kama wewe ni kiongozi. Matokeo yake watu wakalemaa ile mbaya!
 
Karamagi ni mfanyabiashara mkubwa sana hata kabla ya kuwa mbunge na Waziri. Pesa zake ndizo zilizomwingiza kwenye siasa, kwa hiyo wala sishangai kusikia kachangia kiasi hicho kikubwa cha fedha!

Wanasiasa wetu wa siku hizi wote ni wafanyabiashara. Yale maadili ya viongozi ya enzi za Nyerere ya kiongozi kutoruhusiwa kuwa hata na nyumba ya kupangisha hayapo tena na yameshapitwa na wakati.

MASAKI

its good to see you around JF
 
By th way nashangaa watu wanalalamika kuhusu KARAMAGI na pesa zake

huyu mtu ni mfanyabiashara mkubwa tuuu na pesa anazo tangu zamani ndio maana yeye anabank na COUTTS BANK ambayo ni benki ya QUEEN ELIZABETH II
coutts.gif

sasa hivi kwa akilizenu mnataka kuniambia kuwa KARAMAGI na account yake kule COUTTS atakuwa hana hizo milioni 29 za madafu?

The man has good credit ratings and thats what matters na mabenki haya

By the way kuwa na account kule COUTTS inabidi na LAZIMA uwe na mambo yafuatayo:

1)minimum of £500,000 investable assets (kama cash au shares)

2)£5,000,000 net assets (kama vile property, jewellery, artwork etc)

baada ya kuwa na hizo kama minimum requirement ndio unaweza kupewa appointment na bank clerk wao

vile vile hiyo haimaanishi kuwa utapewa account kwani wao wanapenda OLDMONEY na jinsi Karamagi alivyofanikiwa kufungua account pale is another story ambayo itahitaji separate thread.

kwa COUTTS BANK kuwa na pesa pekeyake siyo kigezo cha kufungua account na watakuweka kwenye waiting list zaidi ya miezi 12 huku wanakufanyia background checks and so on

zaidi soma hapa:

[media]http://www.rbs.com/content/about_us/our_heritage/our_history/our_banking_family/present_day/downloads/Coutts_%26_Co.pdf[/media]
 
Back
Top Bottom