Watanzania hatujasahau na hatutasahau yaliyotokea katika tetemeko la Kagera

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
1. Rais uhuru kenyata alichangia wahanga million 200.

2. Serikali ya korea iliwachangia wahanga million 108.

3. Serikali ya uingereza iliwachangia wahanga billion 6

4. Askofu mkuu wa EAGT dkt brown mwakipesile alichangia million 10.

5. Mh Freeman Mbowe million 5.

6. Waziri mkuu wa india NARENDRA MODI na serikali yake walichangia million 545.

7. Mchungaji king james wa kanisa la P.AG. kahororo kyamaizi bukoba alichangia million 3.

8. United States of America ilichangia billion 6.

9. Jasem al - najeola barozi wa Kuwait alichangia dora za marekani elfu 33.

10. Rais yoweli Kaguta museveni wa Uganda alichangia million 430 kupitia serikali yake.

11. Said salimu bakhalesa alichangia million 100.

12. Reginald mengi alichangia million 110.

13. Baraza la wawakilishi zanzibar lilichangia milioni 30.

14. Caspian omid kalambech alichangia million 190.

15. Kiongozi wa madhehebu ya bohora alichangia dora za marekani elfu 33.

16. Umoja wa vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema BAVICHA walichangia million 7.

17. Barozi kagasheki milioni 5.

18. Uvccm mwanza milioni 3.

19 .Mch. Dr geturuda rwakatale million 10.

Kwa mujibu wa ripoti ya maafa iliyo tolewa na mkuu wa mkoa wa kagera Mh Kijuu wakati ule nikwamba nyumba zaidi ya 1200 ziliadhilika na tetemeko hilo.
Ukilinganisha na kiasi hicho cha fedha kilicho changwa na wadau mbalibali niwazi kila Mhathirika angeweza kujengewa nyumba nzuri na ya kisasa tena yenye vigae kwa kila muhanga na umeme juu.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli aliwajibu wanakagera mwafa serikali haina fedha za kuwajengea nyumba na hakuna serikali yoyote duniani iliyowai kuwajengea wahanga wa matetemeko nyumba!
Magufuli alienda mbali zaidi nakusema fedha zilozo changwa zitajenga miundominu ya serikali iliyo alibiwa na tetemeko hilo.

Sasa watanzania tunahoji mbona miundombinu iliyo karabatiwa mbona haiendani na kiasi cha fedha lizizo changwa Fedha zingine zimepelekwa wapi?

WATANZANIA TUMETUNZA MAFILE KWA KUMBUKUMBU NZURI ZA KUSAIDIA KWA AMBAO HAWAKUREKODI KUMBUKUMBU.

kwa wale tulioweka Kumbukumbu naomba tukumbane kwa kuongeza mengine na kuonyesha jinsi gani hatutaki kudanganywa wala kuunga hoja zisizo na Mantiki.

TUUNGANE NA KUKEMEA UNYANYASAJI UNAOENDELEA KULIGAWA TAIFA LETU BILA KUANGALIA ITIKADI ZETU BALI TUWEKE MBELE MSTAKABARI WA MAENDELEO KWA WANANCHI WA TANZANIA NA UTANZANIA WETU. (Tusibaguane kwa Matatizo tuliyonayo #SisiniWamoja Tanzania Moja kwa Umoja WETU.)
 
Huu Ni urojo wa Cha Domo na Wala hazita wasaidia kuwapa kura hamna sera zaidi ya kuwa vibaraka wa mabeberu, Viva magufuli Viva CCM
 
Ndugu tatizo la Wa Tz wengi Ukiwapa tui chai washasahau yote yalopita na hajua hata shida ya zinazokuja.
Usione sisiemu ina jitahidi kutumia wasanii kwenye kampeni zao au unaskia wengine wana honga au sijui kisheree flani , hizi ndo hizo mbinu kuwasaulisha na kwa Tz hii wanasahau kabisa.

Ukianza taja mambo yaloumiza watu ni mengi sana ila mtu kapewa buku 10 ,kashasahau shida zote na yuko tayari hata kupigia kampeni.

Watu walioumizwa ni wengi sana na utawalau KAMA kuwafukuzisha watoto wawatu pale Udom tena ndan ya sa 24. Aisee iliniuma sana hi kitu kwani nilikuwa na mdogo wangu wa kike pale daah acha yan acha si bora wangetoa hata wiki jamani. Utadhani madogo walikosea wao kuwa pale au walileta vurugu.
 
Jiseemee weweeee, usitujumulishe na sisi wanabukoba tunao kaaaa hapa hamgembe bukoba mjini. Sisi tunasema magufuli anatosha na kura zote ni zakeeee, kwahiyo uchonganishiii, na propaganda ondoa hapaa
 
Chadema mbona uchaguzi huu amna helcopter?.
Jitahidini mpate helcopter huwa inasaidia kujaza watu kwenye uwanja wanapokuja kuishangaa.
 
Ndugu tatizo la Wa Tz wengi Ukiwapa tui chai washasahau yote yalopita na hajua hata shida ya zinazokuja.
Usione sisiemu ina jitahidi kutumia wasanii kwenye kampeni zao au unaskia wengine wana honga au sijui kisheree flani , hizi ndo hizo mbinu kuwasaulisha na kwa Tz hii wanasahau kabisa.

Ukianza taja mambo yaloumiza watu ni mengi sana ila mtu kapewa buku 10 ,kashasahau shida zote na yuko tayari hata kupigia kampeni.

Watu walioumizwa ni wengi sana na utawalau KAMA kuwafukuzisha watoto wawatu pale Udom tena ndan ya sa 24. Aisee iliniuma sana hi kitu kwani nilikuwa na mdogo wangu wa kike pale daah acha yan acha si bora wangetoa hata wiki jamani. Utadhani madogo walikosea wao kuwa pale au walileta vurugu.
Hili la Udom acha kabisa, nilikua pale huo mwaka, wale watoto waliletewa mitutu na kufukuzwa usiku kama mbwa. Wengi wao waliharibu kabisa system zao za elimu lakini ndio hao na wazazi wao leo hii utawakuta wanasema habari za ndege na flyovers.
 
Chadema mbona uchaguzi huu amna helcopter?.
Jitahidini mpate helcopter huwa inasaidia kujaza watu kwenye uwanja wanapokuja kuishangaa.
Wale wenye malori na matrekta waliosomba watu kuwapeleka kwenye fiestra yenu kule Dodoma jana wameshalipwa kwani?
 
Back
Top Bottom