Mbowe akizungumza kuhusu Mdee na wenzake kwenye kikao cha Baraza Kuu

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
795
1,635
Kama ni kweli anayoyasema Mh. Freeman A. Mbowe kwenye video hii wakati wa kikao cha Baraza Kuu kuhusu Halima Mdee na wenzake maarufu kama COVID-19 ni kweli, basi huyu mtu IS REALLY A TRUE and A GOOD LEADER of this millenium in Tanzania..!!

Mimi kwa 99% naweza kuamini kuwa ni kweli maana hata baada ya maelezo hayo na kila mmoja kupewa nafasi ya kusema lolote ikiwemo aidha kukanusha maelezo ya mwenyekiti au kuyakubali, HAKUNA ALIYESIMAMA.



Ningependa kumuita ndugu yangu Pascal Mayalla kwa heshima na taadhima aje aseme neno hadharani hapa kuhusu hili...

Ni kwa sababu, amekuwa akisisitiza mara kwa mara juu ya ile iitwayo kwa kimombo kama "Natural Justice" yaani "haki ya kusikilizwa" na kwamba, hawakupata nafasi hiyo huko KK [Kamati Juu] na kwenye BK [Baraza Kuu] ...

Je, ndugu Pascal Mayalla hii sio ya haki yao ya waliyoipata ili wasikilizwe na yet, wakaiachia ikapaa hewani na kupotea mithili ya mvuke..?

Ndugu Pascal Mayalla, je kuna namna nyingine labda ya kumpa mtu nafasi ya kujitetea anapokuwa ameshitakiwa na si kwa namna hii..?

Asanteni wote kwa kusoma.
 
" amekaa na halima Nairobi wiki moja, na wakati mwingine walikuwa wanatoka" mhhhh, mbona hasemi yote, naona uhuni mtupu, unakaaje na mtu si mkeo kwa wiki nzima
 
Back
Top Bottom