Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Swila aomba ahirisho kuwa hajisikii vizuri; kuendelea na ushahidi 10/02/2022

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Habari Wakuu,

Leo 09/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki:Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Sostenes Swila kuendelea kutoa ushahidi wake Februari 9, 2022

Baki nami.

Updates:


Jaji ameingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
  • Wakili Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Mawakili Wa Serikali Waandamizi
  • Wakili Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na
  • Wakili Michael Mwangasa
  • Gaston Garubindi
  • Evaresta Kisanga
  • Maria Mushi
  • John Masoud kwa Niaba ya Nashon Nkungu
  • Clinton Kipengele Kwa niaba ya John Mallya
  • Fredrick Kihwelo
  • Dickson Matata
Jaji: anaandika, Kisha anaita Majina ya Mshitakiwa wote Wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili Kuendelea Kusikilizwa na tupo tayari Kuendelea

Peter Kibatala: Nasi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kuendelea

Shahidi anapanda kisha anasimama Kizimbani Jaji anaandika Kidogo

Jaji: Shahidi nakukumbusha Ulikuwa chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Shahidi: Sawa Mheshimiwa, Ila kuanzia Jana Jioni hali yangu haikuwa Nzuri lakini nitaendelea Kutoa Ushahidi

Kibatala: Good Morning Inspector

Shahidi: Morning

Kibatala: Nafikiri Unakumbuka Jana tulikuwa kwenye Swala la Mbowe Kuanzisha Ugaidi

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Tulijadili Mpaka Pale ambapo Washitakiwa Walikutana pale Morogoro na Luteni Denis Urio

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Upelelezi wako Uligundua hivyo

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na aliye Waita pale alikuwa ni Luteni Denis Urio

Kibatala: Na Utakubaliana na Mimi Kuwa Mpaka Mshitakiwa Wa Kwanza, Wapili na watatu anakutana na Denis Urio Mbowe alikuwa hawajui na hajawahi Kukutana nao

Shahidi: sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba kabla ya Kukutana Walikuwa wanafanya Shughuli zao halali

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Luteni Denis Urio aliwaita Morogoro Kwa sababu Yeye Makazi yake yalikuwa Morogoro

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwa namna yoyote Ile Freeman Mbowe Hakuwahi kuwa Morogoro kabla na baada ya hizo Tarehe walizokutana Morogoro

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Uliwahi Kugundua Kwa wewe Kuwa Pro Active au Kuhalifiwa na Luten Denis Urio Kwamba kabla ya Mohammed Ling'wenya Kuondoka Mtwara Kuja Morogoro, ilibidi awasiliane na Mzee Ling'wenya Kupata Ruhusa

Shahidi: Sikuwahi Kufahamu

Kibatala: Pia hufahamu Luteni Denis Urio alitoa Ushahidi Mahakamani akithibitisha

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo hata nikikwambia Kwamba Mzee Ling'wenya ilibidi aitishe Kikao cha Ukoo/Familia Kujadili suala la Mtoto wao Kwenda Kwa Luteni Denis Urio

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Pia ufahamu Kwamba Wakati Wanamtoa Walimtoa Kwa Uangalizi Kwamba Wanamkabidhi Kwa Luten Denis Urio na Kwa Freeman Mbowe, Kwa sababu ni watu wanao aminika

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Baada ya Kuwa wamekutana Luteni Denis Urio na Khalfani Bwire na Moses Lijenje na Baadae Kundi la Pili Adam Kasekwa Mbowe Hakuwahi Kutia Neno katika yale yaliyo kuwa yanajadiliwa pale

Shahidi: Fafanua tena

Kibatala: Ulikuwa unafahamu Kwamba Luteni Denis Urio, alikutana na Makundi Mawali Kwa wakati tofauti

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Baada ya Kuwa wamekutana Luteni Denis Urio na Khalfani Bwire na Moses Lijenje na Baadae Kundi la Pili Adam Kasekwa Mbowe Hakuwahi Kutia Neno katika yale yaliyo kuwa yanajadiliwa pale

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: aliyewaambia Bwire na Moses Lijenje na aliyewaambia Adamoo na Ling'wenya alikuwa ni Luteni Denis Urio, Je ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unaposema Kwamba alipo wasiliana na Mbowe aliwasiliana Meseji, Telegram au Simu

Shahidi: Kwa Njia ya Mdomo na Pia kwa Njia ya Mawasiliano ya Jumbe za Telegram

Kibatala: Walipoongea Denis Urio na Freeman Mbowe wewe Ulikuwepo

Shahidi: Sikuwepo

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Ulishawahi Kusikia Neno Maarufu la Kiupelelezi la "Your Word against Mine"

Shahidi: Sijui

Kibatala: Kwa kuwa Wewe, Kingai, DCI hamkuwepo Wakati Mbowe anaongea na Urio

Shahidi: Hatukwepo lakini tulifanya Upelelezi

Kibatala: Watu Wawili wamezungumza, Na DCI hakuwepo, Kingai hakuwepo, na wewe hukuwepo Je si lazima sasa Tupime Maneno ya Denis Urio na Freeman Mbowe

Shahidi: Siyo lazima, Unaweza Kufanyia Kazi Maneno ya Denis Urio

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Wakati Denis Urio anakutajia Kuwa Kuna Cassa Motel, Je Uliwahi Kwenda hata Kuthibitisha

Shahidi: Sijawahi Kwenda

Kibatala: Mgahawa ambao Denis Urio alitaja Wamekutana na Mbowe Wewe Kama Mpelelezi Uliwahi Kwenda

Shahidi: Sikwenda

Kibatala: Je Urio aliwahi Kukwambia Kwamba alipanda Tax Mgulani

Shahidi: sikwenda

Kibatala: Je aliwahi Kukwambia Kwamba alikuwa Mjini alipanda bodaboda

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Uliwahi Kufika Kuona Kama Kuna Kituo cha Bodaboda

Shahidi: Sikwenda

Kibatala: Je Uliwahi Kwenda Cassa Motel Kuthibitisha Kama Gari ya Denis Urio lilifika pale

Shahidi: Sikwenda

Kibatala: Uliwahi Kwenda Mgulani Kuthibitisha Kwamba Denis Urio aliwahi Kufika na Kuishi Pale

Shahidi: Sikwenda

Kibatala: Nyie Kama Polisi mkipata Taarifa Mnairekodi au Kufanyia kazi

Shahidi: Tunafanya kazi

Kibatala: Je wewe Kama Mpelelezi Uliwahi Kwenda 14 July 2020 Kule Ngerengere 92 KJ Ka kweli alikuwa kazini

Shahidi: Sikwenda

Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Baada tu ya Kurejea Kutoka Darfur alikamatwa Kikosini baada ya Kutajwa na Adam Kasekwa

Shahidi: Sifahamu nilifanya Uchunguzi

Kibatala: Kwakuwa umechunguza Kule 92 KJ uliongea na nani

Shahidi: Nisha sema Sikwenda

Kibatala: Kwa hiyo wewe hata 92KJ hufahamu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kwamba Makampuni ya Simu yanatunza Kumbukumbu za Mawasiliano

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je Yanatunza Kwa Muda gani

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Je Wewe Kama Mpelelezi Uliomba Taarifa za Call Recordings katika Makampuni ya Simu Kati ya Freeman Mbowe na Denis Urio

Shahidi: Ndiyo Niliomba

Kibatala: Kwa Barua ya Tarehe Ngapi

Shahidi: Kwa Barua ya 13 August 2020

Kibatala: kwenda Kampuni gani

Shahidi: Kwenda Kwenye Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao

Kibatala: Kwa Inspector Ndowo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa hiyo wewe Uliomba Taarifa Kwa Inspector Ndowo, Je yeye ndiye Mwenye Kuhifadhi

Shahidi: Yeye Ndiye aandike Barua kwenda Tigo na Airtel

Kibatala: kwa hiyo wewe Pamoja na Mambo yote Uli Mwomba Na Rekodi za Mawasiliano ya simu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je wewe Uliona Katika Barua yake kutoka Kwenu Terms of reference suala la Call Recordings lipo

Shahidi: Halipo

Kibatala: kwa hiyo Mliomba au Hamkuomba

Shahidi: Hatukuomba

Kibatala: Uwe sasa inasililiza kwa Makini.. Haya Unafahamu Kuhusu Sheria ya EPOCA

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo ufahamu Kwamba Sheria hiyo nakupa Mamlaka Ya Kuomba Voice Recordings

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo Wewe Wakati DCI na Kingai Wanakuteua waliluteua Kwa sababu ya Uwezo au Sababu ya Kitengo X

Shahidi: Sababu ya Uwezo

Kibatala: Hivi una Elimu gani

Shahidi: Kidato cha 6

Kibatala: Sekondari gani

Shahidi: Moshi

Kibatala: Ulipata Division ngapi

Shahidi: Division 3 Point 13

Kibatala: ulifaulu Kwenda Chuo

Shahidi: Hapana, CCP Moshi

Kibatala: Ok! Ndiyo Walikuchagua sababu ya uwezo huko

Kibatala: Je unafahamu Mojawapo Ya Majukumu ya Upelelezi wako ilikuwa Ku Trace kila single Cents

Shahidi: Hilo siyo Muhimu cha Muhimu Kama alitoa pesa kufadhili Ugaidi

Kibatala: Swali langu nasema kwamba Kama Mpelelezi unajukumu la Ku Account for na Ku Trace Kila single Cent

Shahidi: Nisha Jibu Kuwa siyo Muhimu

Kibatala: Je nani alikuwa na Jukumu la Kuona na Kuthibitisha zile pesa

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Na hilo Jukumu Uliteleleza Kikamilifu la Ku Trace hizo pesa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Tayari Kwamba Denis Urio alituambia kuwa Watuhumiwa Walisafiri Kutoka Walipo kuwa Kuja Morogoro, Je Unafahamu Kwamba Walikuwa Refunded

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji nani alitoa Pesa Kuwa Refund (rejeshea)

Shahidi: Luteni Denis Urio

Kibatala: Na Kwamba Unafahamu Kwamba Hawa walikuwa wanajua Kuwa walikuwa wanapewa Pesa Kurejeshewa Nauli zao

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unafahamu Kwamba ni TSh ngapi Moses Lijenje alirejeshewa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Lini wewe Ulifahamu Kuwa Unakuja Kutoa Ushahidi

Shahidi: Alhamisi

Kibatala: Hiyo Taarifa Ulipewa na Watu serious au Uliwa chukuliwa poa

Shahidi: Nilichukua Serious

Kibatala: Hii Kesi ni Kubwa au Nyepesi

Shahidi: Kubwa

Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi ni nani atakuja kutueleza Kuhusu mabadilishano ya Pesa kati ya Moses Lijenje na Khalfani Bwire kutoka kwa Denis Urio

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Shahidi anaitwa Gladys Fimbari kutoka Airtel alileta Taarifa Ya Mihamala, Je Ulisoma na Kuelewa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Pesa ambayo Wali badirishana Mikono kati Adam Kasekwa na Denis Urio ilikuwa TSh ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Pesa ambayo ilibadilishana Mikono katika ya Mohammed Ling'wenya na Denis Urio ni TSh ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Ni wewe ulimuhoji Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: alikueleza?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ilikuwa TSh ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Pesa Iliyo badirishana Mikono kati ya Moses Lijenje na Khalfani Bwire ilikuwa TSh ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unafahamu Pesa kiasi gani ambacho alipewa Mohammed Ling'wenya Nauli ya Kwemda Moshi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Wakati Washitakiwa wa Kwanza, Wapili na Watatu wanaenda Moshi Kama wanavyo Sema Watuhumiwa, Je Walikuwa Wanafahamu Wanaenda Kufanya Nini huko

Shahidi: Walikuwa hawafahamu

Kibatala: Nikumbushe Kozi Uliyosoma Kwamba Ulisomea Masuala ya Ugaidi Botswana

Shahidi: Post Blast Scene Investigation

Kibatala: Ni sahihi Kuwa Kozi hiyo inahusu Juu ya Uchunguzi Baada ya Milipuko

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Umesoma Sheria yetu ya Ugaidi hapa Tanzania

Shahidi: Nimesoma Kidogo

Kibatala: Umesoma Kuhusu Vifungu Vinavyo husika na Ufadhili wa Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu Vipengele Vinavyo husika Katika Ufadhili wa Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Taja

Shahidi: 1. anayetuma lazima awe anafahamu Malengo ya fedha 2. siyo lazima awepo eneo la Tukio 3. Siyo lazima Matumizi ya pesa yajuliikane

Kibatala: Kwa hiyo hata Uchunguzi Wako Ulifuata hicho Ulicho elewa wewe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Conclusion Yako ilijilita Katika Tafsiri hiyo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Uwepo wa Pesa yenyewe ni sehemu ya Shitaka

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Je nilitaka kutuma pesa Kufadhili Kitengo Cha Ugaidi Mtwara, Je Ikiwa pesa ile imeenda Kutumika Kwenye Kilimo cha Mpunga Ifakara, Je Nitakuwa nimefadhili Ugaidi

Shahidi: Inategemea

Kibatala: Inategemea na nini

Shahidi: pesa kama Imekwenda

Kibatala: Narudi swali, Je nilitaka kutuma pesa Kufadhili Kitengo Cha Ugaidi Mtwara, Je Ikiwa pesa ile imeenda Kutumika Kwenye Kilimo cha Mpunga Ifakara, Je Nitakuwa nimefadhili Ugaidi

Shahidi: Ndiyo unakuwa umefadhili Ugaidi

Kibatala: Je una Ushahidi Wowote Kwamba Ile 199,000 ilitumika Kule Moshi Walipokuwa Wamefika

Shahidi: Hilo sifahamu, najua tu kuwa walifadhili

Kibatala: Maelezo Ya Luteni Denis Urio anasema alitumiwa Kiasi cha TSh 500,000 katika Simu yake ya 0787 555200, Je alikwambia

Shahidi: aliniambia

Kibatala: 500,000 Kwa Mujibu wa Denis Urio, Mbowe alituma Kwa sababu gani

Shahidi: Kwa sababu ya Kufadhili Vitendo Vya Kigaidi

Kibatala: ambavyo ni Vitendo Vipi

Shahidi: Kulipua Vituo Vya Mafuta kukata Miti Barabarani Kudhuru Viongozi Wa Serikali

Kibatala: Unafahamu Kwamba Luteni Denis Urio anasema Katika Maelezo Yake kwamba aliwapa Khalfani Bwire na Moses Lijenje aliwapa Kuwa Refund Kama nauli

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba afafanue Je ana refer katika Maelezo au Ushahidi

Kibatala: Katika Statement yake Denis Urio anasema alitoa TSh 300,000 akawapa Moses Lijenje na Khalfani Bwire Na Katika Ushahidi Wake Denis Urio anasema Kuwa aliwapa 150,000 kila Mmoja Kuwarejeshea nauli huko alipotaka, Je unafahamu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kati yako wewe na Denis Urio nani yupo katika nafasi Nzuri ya Kufahamu Jinsi pesa Ilivyo gawiwa na kutumika

Shahidi: Ni Luten Denis Urio

Kibatala: Je Shahidi Ulisoma Maelezo Ya Onyo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Shahidi: Nilisoma ila Sikumbuki Kiwango

Kibatala: Ungependa Kujikumbusha au Usinge penda

Shahidi: Ningependa Kujikumbusha

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Kielelezo Namba 1 na Kielelezo namba 13

Kibatala: Tuanze na Maelezo ya Adam Kasekwa

Kibatala: Tafuta sehemu ambapo anasema Tarehe 24 July 2020 Nilikutana na Mohammed Ling'wenya

Shahidi: "Tarehe 24 July 2020 Nilikutana na Mohammed Ling'wenya kasisitiza tuende Morogoro tukakutane na Luteni Urio tuliondoka Siku hiyo hiyo na Kukutana na Luteni Denis Urio, akasema Maelezo tutayakuta huko huko, Akatupa TSh 87,000 kila Mtu nauli ya Kwenda Moshi

Kibatala: TSh ngapi Umesoma

Shahidi: Ni TSh 87,000 kila Mmoja

Kibatala: Ulilinganisha Maelezo ya Mohammed Ling'wenya ni TSh kapewa dhidi ya Maelezo Ya Luten Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kama Mpelelezi Makini kabisa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Luteni Denis Urio, alikwambia aliwapa TSh ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Ungependa ujikumbushe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba D4

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hicho Kielelezo alikitoa Shahidi namba 12 akitoa Ushahidi Wake, Kwa hiyo Kilikuwa katika Matumizi ya Shahidi D4 tu, Siyo Sahihi kukitumia Wakati huu

Kibatala: Mh Jaji Kaka Yangu hafahamu, Mimi nimejemga foundation kwa sababu Shahidi Ndiye aliye Muhoji Luteni Denis Urio, na Nyaraka hii ipo Mahakamani Kama Kumbukumbu za Mahakama Hiki ni Kielelezo cha Utetezi.. Naomba ni Ruhusiwe Kuendelea bila Kuwapa nafasi ya Kuficha Ushahidi

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji nimesikia Kibatala amba Wenzetu waliomba Kielelezo hiki kwa Matumizi yao, na Waliomba kwa Kutumia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6.. Dhumuni ni Kum Contradict Shahidi ambaye alikuwa ni Denis Urio, Leo hii anaposimama

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji anachokifanya wakili Abdallah Chavula Kuhusu Kutaja Vifungu,

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Samahani

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa huyu anasimama kama Nani Mwenye Hoja Kakaa Chini, Mheshimiwa Jaji Wakili Pius Hilla anafanya Vurugu

Jaji: Wakili Peter Kibatala Kaa Kwanza, Tumsililize

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Anachokifanya Wakili Peter Kibatala siyo Sahihi, Harusiwi Kutumia hayo Maelezo Kwa sababu yalikuwa kwa kazi ile tuh

Jaji: Ulisimama Wakili Kibatala

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nimesimama na Mwenye Hoja akakaa Chini kwa sababu ni Educated, Kumbukumbu zitaonyesha nani alifanya Vurugu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mheshimiwa Jaji Hoja yangu ni kwamba Sijaleta Neno Jipya, Kuhusu Rejoinder ni Kujibu yale aliyo yajibu yeye, Hilo siyo Lengo letu

Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa kuwa Mwenzangu ametaja Vifungu na Mambo Mapya, Naomba Sasa Nipewe nafasi ya Ku' respond Kuhusu Vifungu

Jaji: Nimuache Kuhusu Kujibu Vifungu

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Muache aseme Kuhusu Vifungu, Kwa sababu Sheria haina Kificho

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wakati Wakili Robert Kidando anataja Hoja yake hakutaja Kuhusu Vifungu Vya Sheria

JAJI: lakini Sasa Wakili Chavula alikuwa hajamaliza

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji nilikuwa naeleza Kwamba Kifungu walicho Kutumia Wenzetu Kilikuwa ni Kifungu cha 164 na Kuhusu Kupokelewe Mahakamani Mahakama ilitumia Kifungu cha 154, Kwa Sheria ambayo niliyokuwa nayo Mimi inaonekana

Katika Mstari Wa tatu wa 154 ambayo haina Subsections ANASOMA Sisi tuna tulia Mkazo katika "intended to Contradict" na "for the purpose of Contradict" Kama shahidi ni Maker wa Ile Nyaraka, Then sawa,

Hata Ile Dhana ya fairness Haipo, Ndiyo Maana Wanasheria Waka Limit itike kwa ile tuh, Kwa Dhana hiyo, Mwenzetu hana Uwezo wa kuitumia

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwanza Maneno "Maker " ni Maneno Binafsi wala Siyo Kwenye Sheria, Sheria inasema Kwamba Kama ameshiriki, Ku reduce into Writing, Hata katika hiyo 164 haikuweka Ukuta/zuio, Kifungu cha 164 ni Kufungu Kinacho zungumzia Kuingizia

164(c) unasema By Proof of former Statement, Hakuna Ukuta au Zuio, Huyu tunamuuliza kwa sababu nidiyo Mpelelezi, Kwamba atanyimwa Haki Ya Kuzungumza wakati Kuna Re examination, Shahidi ame Own suala la hayo Maelezo

Na Ikumbukwe Mheshimiwa Jaji Shahidi amesha Jibu tayari Kuhusu hiyo Statement, Vipi Ukimikataza sasa hivi na Yale Majibu ya awali, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Jaji: Hoja Iliyo jitokeza ni Hoja ilianza kwa Mr Kidando Kwamba Upande wa Utetezi hawana Haki ya Kutumia Kielelezo husika, Ambapo akasimama Wakili Abdallah Chavula Kwa Kutaja Vifungu Vya Sheria, Kwamba Statement hiyo Inatumika Kwa Kum Contradict Shahidi namba 12 na siyo Vinginevyo.

Hoja hiyo ilipingwa na Upande wa Utetezi Kwamba Vifungu haviweki katazo, Mahakama kwa kuzingatia Hoja zote Kwa Kina, Inafahamu kwamba Upande wa Utetezi kwa shahidi aliyepo Mahakamani lao yao ni Kutengeneza Misingi, Shahidi aliyepo Mahakamani ni Mpelelezi Wa Shauri hili.

Wakati anaulizwa na Mawakili Wengine alisema Kwamba alitumia Nyaraka Zote Katika Upelelezi Kufikia katika hitimisho, Kwa Maana hiyo anaulizwa kuhusu Kitu alicho fanya nacho kazi, Ndiye aliye Muandika Maelezo ya Luten Denis, Kama hawezi Kujibu atatuambia kuwa hawezi.

Jaji: Kwa sababu hiyo Hatuoni sehemu ambayo ina udhibiti wa Kuendelea Kujibu. Kwa Maana hiyo Mahakama Inaruhusu Kutumika Kwa Kielelezo hicho.

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo (kimasta zaidi) ile dizaini ya shivooo

Kibatala: Shahidi Tulikubaliana kuwa Moja ya Investigative tool au Workonh tool ni hii statement ya Pesa na Maelezo haya

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Soma pale Baada ya Kupokea Pesa hizo nilizitoa

Shahidi: Tarehe 22 July 2020 Baada ya Kupokea Pesa hizo nilizitoa, na Kuwapatia Mohammed Ling'wenya na Adam Kasekwa Kama nauli

Kibatala: Sasa Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwamba Ile Tsh 87,000 anayosema Adam Kasekwa kila Mmoja, Je wewe Kama Mpelelezi unaona TSh 87,000 ya Adamoo na Ling'wenya inaendana na Taarifa ya Mtoa Taarifa Wenu

Shahidi: Hilo linahitaji Maelezo, Wote wanaelezea Swala la pesa, Luteni Denis Urio anasema aliwapa 190,000

Kibatala: TSh 190,000 Ipo wapi

Shahidi: Vyote Vinaendana Maelezo ya Denis Urio na akina Adam Kasekwa

Kibatala: sawasawa wacha Jibu lako liingie

Kibatala: Kama Walipewa Kila Mmoja TSh 87,000, Jumla ni TSh ngapi

Wakili wa Serikali: Samahani Ukisoma Statement ya Mshtakiwa Wa Pili (Kielelezo namba 1) kwamba alitupa nauli TSh 87,000 kila Mtu, Huku alipo Mrejesha katika TSh 199,000 aliyo wapa Adamoo na Ling'wenya

Kibatala: HAKUNA HOJA HAPO.

Jaji: Kabla ya hapo, Hoja yao ni kwamba kila Utakapo taja TSh 199,000 usiseme nauli

Kibatala: Kwenye hiyo Mheshimiwa Jaji, haina shida Nitarudi Nyuma na Kujenga Upya Misingi kurahisisha

Wakili wa Serikali Robert Kidando anamfuata Shahidi na Kutetea naye Kidogo

Shahidi: SAMAHANI MHESHIMIWA JAJI SIJISIKII VIZURI KWA KWELI.......

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Nimeongea na shahidi anasema hajisikii Vizuri kabisaaaaaa, na kapatwa na tatizo ghafla.. Mheshimiwa Jaji naomba tuweze Kupatiwa na airisho

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sisi tunaamini kuwa airisho linaombwa kwa sababu nyingine siyo sababu ya ugonjwa...

Wakili wa Serikali: Lakini Mwenzetu Kusema Shahidi aendelee tu sababu fulani fulani nafikiri Mheshimiwa Jaji si Vyema Kusema hivyo.. Baada ya Kusema hayo naomba airisho

Jaji: Je airisho la saa Moja, mpaka saa 7 au airisho la Siku Nzima au nini

Wakili wa Serikali Robert Kidando: anamfuata tena shahidi wa Jamhuri

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji anaomba airisho Mpaka Kesho pamoja hatuwezi Kujua itakuwaje..

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sisi tuna wasiwasi sana na Sababu zilizotolewa na Shahidi Kama ni sababu Njema, Sisi tunapinga airisho Mpaka Kesho, Ikupendeze Uairishe Mpaka Saa 9 Alasiri.. Tuje tuone progress Kwa sababu airisho linalo ombwa lina athiri Haki za Wateja wetu..

Na tutakaporejea tunaomba Shahidi aje na Uthibitisho Kwamba alikwenda Hospitali na alitibiwa, Ishawahi Kutokea Mara Kadhaa, Inspector Jumanne Malangahe hapa alisema hivyo hatukuona Uthibitisho, Inspector Ndowo alifanya hivyo hakuleta Uthibitisho na Sasa ni huyu

Hii ni Mahakama, Wateja Wangu Wanayo Haki ya Kufahamu au Kuona Japo Kuna Haki na kweli Inatendeka..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji anasema ana Wasiwasi, na Mheshimiwa Jaji hatuwezi kucheza na Haki za Watu, Ninachokumbuka Shahidi aliongea Asubuhi kuwa Leo hajisikii Vizuri.. Hizi Proceedings serious hatuwezi Kuleta Mzaha..

Wakili wa Serikali: Naomba airisho Mpaka Kesho ijulikane itakuwaje baada ya Shahidi Kupata Matibabu

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kurudisha Vielelezo

Jaji amekuwa kimya hapa akiandika

Jaji: Kufuatia Maombi yaliyoletwa na Shahidi, Kwamba Shahidi hajisikii Vizuri na Maombi hayo yaliungwa Mkono na Mawakili wa Serikali, Shahidi ameomba nafasi ya kwenda Kupata Matibabu, Maombi haya yamepingwa na Mawakili wa pande wa Utetezi kupitia Wakili Peter Kibatala

Kwamba Shahidi anakwepa Maswali ya Dodoso, Na Kwamba Kuna Mifano Kadhaa ya Mashahidi Waliopita, Na Kwamba Mahakama Itoe airisho Mpaka Saa 9 Alasiri.. Kwa Kuzingatia Maombi ya pande zote mbili na Shahidi Mwenyewe, Ukizingatia Shahidi alisema Kwamba Asubuhi hajisikii Vizuri

Katika Utoaji Haki wa Mahakama Zetu Shahidi lazima awe na Uwezo na Kusimama au Kukaa, Shahidi ameshasema hajisikii Vizuri, Kwa hiyo Mahakama Haiwezi Kwenda tofauti na Utaratibu juo, Mahakama Inaona Swala la Shahidi Kusema hajisikii Vizuri ni swala la Kutoa Hairisho

Na Suala linalobakia ni airisho Mpaka Muda gani, Mahakama Inaona kwamba suala la Ugonjwa siyo Suala la Kununua Spea na Kurudisha ni Suala la Afya, Mahakama Haiwezi Kumpangia Muda wa Kupata Matibabu, Kwa sababu hiyo Mahakama Inatoa airisho Mpaka Kesho

Suala la Hoja ya Utetezi wa kwamba Shahidi alikuwa anaumwa ni suala Muhimu hata Kama Uthibitisho huo utakuwa into details, Lengo ni Kulinda Privacy yake Shahidi.. Shahidi nakuonya Utatakiwa kuwa Kizimbani Kesho Saa 3 Asubuhi, Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Kamili

Jaji anatoka Mahakamani
 
Hii kesi angekuwepo;

1) Tundu Lissu
2) Peter Kibatala
3) Nashon Nkungu
4) Fredrick Kihwelo.
5) Mtobesya.
6) John Malya.
7) Fatma Karume.

Jopo la mawakili watetezi lingekua poa sana, formation hapo ingekua imekamilika ipasavyo, mashahidi wangeshikwa matumbo ya kuharisha.
 
Back
Top Bottom