Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

ushauri ni kuwa akulipe fidia tena pesa nyingi ili kesi iishe mezani
then huyo mwanaune hafai kuwa mumeo hiyo kukuambia yupo tayali kwa ndoa 7bu anaogopa msala wa hiyo kes
i mtu anaekupenda kweri awezi kukuingilia kimwili bila ridhaa yako hata siku moja sana kama domo zege atakuonyesha vitu flan we mwenyeye utajua uyo ni mtu mbaya sana na hafai kuwa partiner wa maisha yako achananae naye kabsa utakuja kujuta sana baadae ukiamua awe mumeo
we vuta subira msubili mchumba wako
 
Pole sana.

Kwa hiyo unafikiria kumpa nafasi aliyekubaka? Na unaongea unafikiri anakupenda huyo? Maneno yake ya sasa ni ili usimshitaki na sijui kwanini unamsumulia juu ya yote hayo.

Baada ya muda uliyotendwa hayataondoka sababu sasa ni bado mapema.

Mimi ningemshitaki, kazi tupa kule hata kama nikiikosa. kufanya nae kazi kwanza unazidi kujitesa wewe na yeye unampa mwanya wa kukubaka tena na kuchezea akili yako. kama msaada wa usafiri ndio shida kwako basi inabidi ujifikirie nini unataka maishani wakati mabasi yapo.
 
Dada yangu,kwanza usikubali kuolewa na huyo jamaa aliyekubaka,ww msamehe Mungu ndiye atakayekulipia sawa. Songa mbele na maisha yako,utapata mtu wa kukuoa hata kama huyo wa miaka mitatu atakuacha,kilichopo ni kumtangulza Mungu mbele daima.
 
vp jamaa fundi, au ndio ulikuwa ganzi hujui chochote zaidi ya kukuta udenda unakutoka asbh kunako IKULU...?
 
Labda akiona kesi inamuendea vibaya anaweza hata kukuondoa duniani ili asimwage ugali wake na kuhalibu mipango yake.
Pia kama na wewe umempenda huyo meneja na ukiangalia kwa vipimo vyako unaona anakupenda na umeridhika, kubali tu akuoe.
 
Yaani anibake halafu awe mume!!!!

Anaogopa jela ndio maana anahitaji ndoa

Na akisha kuoa tegemea mengi ni zaidi ya kubakwa
kweri kabisa nilikuwa na boss wangu mmoja Wakati nafanya kazi KENYA ye hulka yake ilikuwa kumuingilia mwanamke akiwa ajitambui au yupo usingizini kiasi hio tabia hipo mpaka kwa mkewe anamvizia akiwa kalala tulikuwa tunapatana sana 7bu wote tulikuwa watanzania ao alikuwa ananiambia mengi sana khs hiyo tabia yake anadai hiyo tabia aliianza tangu kijana kwa wadada wakazi wa hme kwao anawanyatia usiku anawafanya wakiwa wamelala akaendelea mpka leo ikiwa tuktoka outing yeye kazi yske kuwapigisha pombe malaya mpk wanapoteza then anawabeba km mzoga anaenda kuwala yaan ndo kazoea hvyo
so nina wasi sana na huyo jamaa isije akawa na tabia kama ya huyo mshkaji araf ukajuta hapo mbeleni dairy kubakwa tuu
 
Hiyo jamaa ingekuwa hakupendi asingefika Hosp kukujulia hali angefunga virango na kusepa!! Shauriana na halmashauri ya kichwa chako kama utaamua kumsamehe au LA!! Ili upande wangu naona bora umsamehe na maisha yanasonga maisha yenyewe mafupi unampeleka jela na ww hujui kma kesho utaamka salama!! Jela atakula mvua ya miaka 30
 
Psychologists would term this conflict as ID vs EGO..

A. Waste your time, waste your money, destroy his future, ruin your work, ruin your reputation b4 your mchumba

VERSUS

B: Forget and let it go, save your time, money, reputation, relationship.

Bora uchague B.
Then find a way to protect your self-esteem. Eg After all, it's not your first time to have Sex. Rmb the moments your very own partner forced to get you laid.
Ni mentality set up tu...
 
Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.

Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.

Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa

Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.

Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.

Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.

Nipo njia panda nahitaji msaada wenu

Asanteni
Chukua muda umchunguze isije kuwa ndio tabia yake! By the way madawa ya kulevya aliyapata wapi???
 
Chanzo cha yote hayo ni pombe. Ungekuwa hutumii hata kiasi kile cha kuonja yasingekupata.
 
Last edited:
kweri kabisa nilikuwa na boss wangu mmoja Wakati nafanya kazi KENYA ye hulka yake ilikuwa kumuingilia mwanamke akiwa ajitambui au yupo usingizini kiasi hio tabia hipo mpaka kwa mkewe anamvizia akiwa kalala tulikuwa tunapatana sana 7bu wote tulikuwa watanzania ao alikuwa ananiambia mengi sana khs hiyo tabia yake anadai hiyo tabia aliianza tangu kijana kwa wadada wakazi wa hme kwao anawanyatia usiku anawafanya wakiwa wamelala akaendelea mpka leo ikiwa tuktoka outing yeye kazi yske kuwapigisha pombe malaya mpk wanapoteza then anawabeba km mzoga anaenda kuwala yaan ndo kazoea hvyo
so nina wasi sana na huyo jamaa isije akawa na tabia kama ya huyo mshkaji araf ukajuta hapo mbeleni dairy kubakwa tuu

Jamaa kajenga mazingira hadi watu wanamuona mwema,ajabu sana.

Eti kamuandalua supu,kamuona hospitalini.Itakuwa ndio tabia yake ya kuwawekea mabinti madawa ya kulevya na kisha kulala nao
 
Kitendo alichodanyiwa ni kibaya sana regardless ni co worker or manager, haraka sana fungua kesi, in fact ulitakiwa kufanya hivyo ndo uje JF ili kupata legal advice. Kwa mnaosema amsamehe eti atapoteza muda au boyfriend wake atajua mnasahau one thing : mleta uzi ameshapata athari kubwa psychological na ataishi nayo, so the guy (guys?) needs to be severely punished so that he can not do it again.
 
Kakuekea dawa?alafu kakubaka alafu anataka kukuoa? UTAISH NA KOVU MIAKA YOTE UKIMUANGALIA
 
Chukua muda umchunguze isije kuwa ndio tabia yake! By the way madawa ya kulevya aliyapata wapi???


Mkuu tumroge tuu huyo jamaa ama unaonaje?

Back to topic
Jamaa inaonekana ndo tabia yake na sio bahati mbaya. Huyo alikuwa keshajiandaa kabisaa na mzigo.
 
Hao wanaokushauri yaweza ikawa si wema kwako, make mm nionavyo huyo hajakubaka ulipenda mwenyewe make kama ni mtu mzima mwenye akili timamu kupenda kwako lifti ndiyo kulikuponza yaweza ikawa nawe unampenda sasa amua moja kubeba mtungi au kuutua, kwaheri mm napita.
 
Aisee wanaume siku hizi tumekuaje sijui!!yani mtu unampa lifti kila siku unashindwa nini kumalizia maneno mawili matatu umalizie mchezo.yani inafikia hatua unabaka kabisa.kwangu mimi sioni kama alifaidi maana raha ya mapenzi muyafurahia wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom