TAMISEMI ilivyonipokonya Mpenzi wangu

TAMISEMI ilivyonipokonya Mpenzi wangu

Mr Rich

Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
40
Reaction score
54
TAMISEMI ilivyoharibu Penzi langu

Ilikua mwaka jana nikakutana na binti mrembo, tulikutana kwenye harakati zangu za hapa na pale za kutafuta riziki. Niliongea nae vizuri na kuanza kufahamiana hadi kupendana haswa.
Tuliishi kwa kupendana na tukawa na mipango mikubwa siku moja tutafunga ndoa. Yeye alikua ni graduate amejishikiza kwenye kampuni fulani anapiga kazi, mimi nakomaa tu mtaani kila deal linalokuja mbele natembea nalo.

Siku zinasonga nikapata majanga kwenye mishe mishe zangu nikarudi nyuma kiuchumi sana hadi nikaona kama naelekea kuchanganyikiwa ikabidi nibadili mazingira nikatoka ile sehemu nilikua naishi nikahamia sehemu nyingine kwajili ya kupata amani ya moyoa na kuanza mwanzo mpya. Mrembo wangu alikua ananipa moyo daily nisikate tamaa nitakua sawa, niendelee kupambana.

Basi siku zikasonga, siku moja nipo geto nimetulia sielewi Mrembo akapiga simu kunipa taarifa kuwa amepata kazi ya Tamisemi, nilifurahi sana nikaona kabisa huyu mrembo sana angalau atakua ananipiga tafu mahali napokwama.

Basi mrembo akaenda kuripoti kazini ni wilaya ya mbali huko kijijini, akafika akafanya taratibu zote akarudi kwao kusubiri mshahara wa kwanza ndio akaanze kazi. Hapa sasa ndio mauzauza yalianza, Mrembo alipata rafiki wa kiume ambaye walikutana siku ya kuripoti kazini ambaye kipindi wanarudi nyumbani alikua yuko busy nae sana hadi nikipiga simu naambiwa subiri kwanza naongea na rafiki yangu, nauli yake ilipelea nikajikaza kiume nikamtumia kitita cha ‘afutatu’ mrembo hata hakusema asante, nilianza kuumia sana plus zile muda wote yuko busy na rafiki yake.

Akafika kwao mapenzi yakaendelea, nikawa namgusia kuwa kule kijijini anakoenda kazini na mimi niende huko nipambane na kilimo, mrembo alikua mkali balaa, kiufupi alikataa kabisa tuwe sehemu moja nikaona fresh.

Sasa akaanza kunipa story zilizo ‘rarua moyo wangu’ kwamba kipindi anaripoti kazini Mkurugenzi alimuomba namba, sijui Katibu tawala alimuomba namba hapa nikaanza kuvurugwa nikaona kabisa hili penzi tayari limeingia dosari sina ubavu wa ku compete na watu wazito.

Basi bana mshahara wa kwanza ukaingia mrembo akaenda kazini, mimi tayari nimekua na wasiwasi hili penzi siku zinahesabika, kwanza ‘Kwanini hataki twende wote kijijini?’ Pili ‘Hao watu wazito atawakataa kwenye mazingira ya ugenini?’. Stress zikaongezeka sura ikakosa nuru nikawa mtu wa mawazo daily, mrembo akaanza kazi vizuri. Kununua vitu vya ndani akaniomba nimuongozee anunue kitanda sina mambo nikashindwa akaniambia rafiki ya kiume amesema atamuongezea hiyo pesa ambayo sina, kijana wenu nikazidi kusonona na kuilaani Tamisemi kulaani serikali na wizara zake zote.

Basi siku zikaenda MO29 ikawa inakaribia, nikatafuta uongo wa kutosha nikampanga mrembo wangu akakubali niende kijijini kazini kwake, kijana wenu nikaingia Songesha, M-Pawa, Kamilisha, Busitisha, nikapigia washikaji nikakusanya michango ili nisiende kijijini kinyonge, nikanunua vijizawadi kwajili ya mrembo nikaenda kijijini. Nilikuta mrembo kijiji kimemkubali amekua mrembo zaidi sura inapendeza, machozi ya furaha na huzuni yalinitoka kabisa, hapa nawaza kwa huu uzuri hao ‘watu wazito’ kweli wamemuacha?.

Basi nikakaa pale kijijini wiki moja kwenye nyumba ambayo silipi kodi, ambayo niliambiwa niongezee kitanda nikasema sina akasema rafiki yake wa kiume ataongeza, muda huu nikafahamu watu wengine ambao wanamuwinda mrembo wangu mfanyakazi mwenzake ambaye amemzidi elimu na mshahara na Bosi wake wa kazini, kichwa kikawaka moto sana. Ndani ya wiki ya kuwa pale niliulizwa unaondoka lini zaidi ya mara kumi (ndugu zangu tutafute pesa). Siku ikafika nikaondoka

Penzi likaanza kushuka, mimi wivu umenijaa sina pesa, wasiwasi wa kuchapiwa ni mkubwa zaidi.

Mwezi mmoja mbele nikatafuta uongo mwingine nikampanga mrembo wangu niende kijijini tena mana msimu wa baridi ulikua umeanza, akakubali nikaenda kijijini bana.

Safari nikafanya kitu cha tofauti nimeshuka stendi pale kijijini nikaenda moja kwa moja kazini kwake nikaa nje pale namsubiri mrembo wangu amalize kazi twende nyumbani kwake ambapo kitu pekee ambacho nimenunua ni dustbin, basi nimekaa pale nje yeye akiwa hajui kama niko pale hadi muda wa kutoka unafika, anatoka nje ananikuta pale nje nimechakaa vibaya mno, suruali langu limepauka na shati la mtumba akaona aibu akanifata pale kwa sauti ya chini ‘Kwanini umenifata kazini?’ Mimi natabasam tu tayari nikijua nimeshavuruga, basi akamliza taratibu za kazini ikafika muda wa kwenda nyumbani, oyaaa niliambiwa nitangulie nipande boda kwamba yeye amevaa sketi fupi hatuwezi panda mshikaki kwenye boda moja, sina akili ila hapa nilichekecha fasta nikagundua mrembo tayari nimeshamchosha na hataki watu wajue kama tuko pamoja, nikaona sio kesi nikatangulia.

Safari ndio ilikua ya moto sana nilishika simu yake nikakuta anachati na yule mfanyakazi mwenzake yani mrembo wangu ndio anamuomba jamaa aende kwake nilivurugwa, haya kuhusu boss wake nae wanachati vile ambavyo unaona kabisa mrembo ‘ataliwa’ soon. Basi ikawa ugomvi hapo ila mrembo wala hawazi wala nini akatoka zake nje akawa anapiga story na wapangaji wenzie, mimi kijana mpumbavu ndio nikabaki ndani naumia moyoni, badae mrembo akarudi akanidanganya danganya nikakubali nikawa sawa kiasi chake ila moyoni najua tayari nafasi yangu haipo.

Sasa muda wa kuondoka ukafika sina nauli, mrembo wangu akanipa nauli na pesa ya kula njiani akanisidikiza kupanda gari nikarudi kwetu.

Wiki kama tatu mbele mrembo wangu akasema hataki tena kuwa na mahusiano wala urafiki na mimi, kiufupi nifanye kama hatujawahi kufahamiana. Nilijua kama ipo siku ataniacha ila sikutarajia kuwa iwe wakati ule niliumia sana, nilikua najifungia ndani kila siku nalia, nikajiingiza kwenye ulevi nikawa mtu wa hovyo sieleweki.

Tamisemi mmenifukizia njiwa wangu
 
Sawa acha mama amalize kuosha narudi
1791536300902.jpg
 
Ukisha sense danger jiongeze ili usidhalilike zaidi!!

Hatupati vile tunavyotaka kwenye maisha Bali tulivyojaaliwa TU hata tufanye juhudi kiasi gani mambo Huwa vile vile ukweli haujifichi
 
Anyway bwana mdogo stori yako ya kuungaunga ila umejitahidi kaza bado uandishi wako ni wa chini sana.

Back to the f*cking story.Bwana mdogo lets get to agree yakuwa wewe bado amature kwenye hii mbanga ya ISIDINGO(MAPENZI).

USHAURI WA BURE;
1. JITAFUTE UJIPATE,ILA WAKATI UNAJITAFUTA SHUSHA BRAND KIDOGO TAFUTA DEMU WA KAWAIDA AMBAYE UTAKUWA UNAPOOZA RIM.

2.GAME YA MAPENZI HAIPO FAIR KUWA NA HELA HAKUKUFANYI UKAPATA KILA DEMU.NA KUWA NA PESA HAKUKUFANYI UWEZE KUMTEKA DEMU.KUNA MAKAPUKO WANAZICHAPA PISI KALI AMBAZO WASHUA HAWAONI KITU NA VILEVILE KUNA WASHUA WANAPUSUA PISI KALI, MBAVU ZA MBWA MNAZIONA TU HIVIHIVI.

UKWELI NI KUWA MAPENZI YANAHITAJI UZOEFU NA KUJIPOSITION VIZURI( VIBE).NA UJIANDAE NA KITU KINAITWA KUKINAI.HATA WEWE HUWEZI KULA BIRIANI KILA SIKU.SO WEKA KWENYE UBONGO KUNA SIKU MTAACHANA TU.

3.KATIKA MAISHA YAKO YALIYOBAKI DUNIANI.JIWEKEE MSIMAMO YAKUWA HAKUNA MTU MWINGINE YULE WA KUMRIDHISHA ZAIDI YAKO.UKIFANIKIWA HAPO HAKUNA KITAKACHOKUSUMBUA.

-KUBALI MAISHA YANAKUPATA NA KUKOSA.NA MAPENZI HIVYOHIVYO KUNA DEMU ATAKUKATAA KWASABABU YAKE ANAYOIJUA YEYE,THATS NON OF YOUR BUSINESS AS LONG AS HAJSONESHA INTREST MPOTEZEE USIFOSI UTAUMIA.

-CHA MSINGI YULE DEMU ATAYEKUKUBALIA HAKIKISHA UNATUWAKILISHA VIZURI KAMA AFANYAVYO MMAKONDE MAYONIZE.ICHAPE KWELIKWELI MAANA LEO SIO KESHO.

4.MAISHA NI KUENJOY.HAKIKISHA KILA UNACHOKIFANYA WEWE NDIO WA KWANZA KUENJOY.WATU WENGINE WOTE WANAKUJA BAADA YAKO.

5.UKITAKA UISHI NA KIUMBE MWANAMKE VIZURI, MPUUZIE NARUDIA TENA MPUUZIE.HAKIKISHA YEYE NDIO ANAWEWESEKA NA WEWE KAMA HAWEWESEKI NA WEWE PIGA CHINI TAFUTA ATAKAYEKUWA ANAHANGAIKA YEYE KUKUTAFUTA,ANAYEWEWESEKA NA WEWE.

#MAPENZI SIO MAGUMU,SHIDA HUJAMPATA BWEGE WAKO.
 
TAMISEMI ilivyoharibu Penzi langu

Ilikua mwaka jana nikakutana na binti mrembo, tulikutana kwenye harakati zangu za hapa na pale za kutafuta riziki. Niliongea nae vizuri na kuanza kufahamiana hadi kupendana haswa.
Tuliishi kwa kupendana na tukawa na mipango mikubwa siku moja tutafunga ndoa. Yeye alikua ni graduate amejishikiza kwenye kampuni fulani anapiga kazi, mimi nakomaa tu mtaani kila deal linalokuja mbele natembea nalo.

Siku zinasonga nikapata majanga kwenye mishe mishe zangu nikarudi nyuma kiuchumi sana hadi nikaona kama naelekea kuchanganyikiwa ikabidi nibadili mazingira nikatoka ile sehemu nilikua naishi nikahamia sehemu nyingine kwajili ya kupata amani ya moyoa na kuanza mwanzo mpya. Mrembo wangu alikua ananipa moyo daily nisikate tamaa nitakua sawa, niendelee kupambana.

Basi siku zikasonga, siku moja nipo geto nimetulia sielewi Mrembo akapiga simu kunipa taarifa kuwa amepata kazi ya Tamisemi, nilifurahi sana nikaona kabisa huyu mrembo sana angalau atakua ananipiga tafu mahali napokwama.

Basi mrembo akaenda kuripoti kazini ni wilaya ya mbali huko kijijini, akafika akafanya taratibu zote akarudi kwao kusubiri mshahara wa kwanza ndio akaanze kazi. Hapa sasa ndio mauzauza yalianza, Mrembo alipata rafiki wa kiume ambaye walikutana siku ya kuripoti kazini ambaye kipindi wanarudi nyumbani alikua yuko busy nae sana hadi nikipiga simu naambiwa subiri kwanza naongea na rafiki yangu, nauli yake ilipelea nikajikaza kiume nikamtumia kitita cha ‘afutatu’ mrembo hata hakusema asante, nilianza kuumia sana plus zile muda wote yuko busy na rafiki yake.

Akafika kwao mapenzi yakaendelea, nikawa namgusia kuwa kule kijijini anakoenda kazini na mimi niende huko nipambane na kilimo, mrembo alikua mkali balaa, kiufupi alikataa kabisa tuwe sehemu moja nikaona fresh.

Sasa akaanza kunipa story zilizo ‘rarua moyo wangu’ kwamba kipindi anaripoti kazini Mkurugenzi alimuomba namba, sijui Katibu tawala alimuomba namba hapa nikaanza kuvurugwa nikaona kabisa hili penzi tayari limeingia dosari sina ubavu wa ku compete na watu wazito.

Basi bana mshahara wa kwanza ukaingia mrembo akaenda kazini, mimi tayari nimekua na wasiwasi hili penzi siku zinahesabika, kwanza ‘Kwanini hataki twende wote kijijini?’ Pili ‘Hao watu wazito atawakataa kwenye mazingira ya ugenini?’. Stress zikaongezeka sura ikakosa nuru nikawa mtu wa mawazo daily, mrembo akaanza kazi vizuri. Kununua vitu vya ndani akaniomba nimuongozee anunue kitanda sina mambo nikashindwa akaniambia rafiki ya kiume amesema atamuongezea hiyo pesa ambayo sina, kijana wenu nikazidi kusonona na kuilaani Tamisemi kulaani serikali na wizara zake zote.

Basi siku zikaenda MO29 ikawa inakaribia, nikatafuta uongo wa kutosha nikampanga mrembo wangu akakubali niende kijijini kazini kwake, kijana wenu nikaingia Songesha, M-Pawa, Kamilisha, Busitisha, nikapigia washikaji nikakusanya michango ili nisiende kijijini kinyonge, nikanunua vijizawadi kwajili ya mrembo nikaenda kijijini. Nilikuta mrembo kijiji kimemkubali amekua mrembo zaidi sura inapendeza, machozi ya furaha na huzuni yalinitoka kabisa, hapa nawaza kwa huu uzuri hao ‘watu wazito’ kweli wamemuacha?.

Basi nikakaa pale kijijini wiki moja kwenye nyumba ambayo silipi kodi, ambayo niliambiwa niongezee kitanda nikasema sina akasema rafiki yake wa kiume ataongeza, muda huu nikafahamu watu wengine ambao wanamuwinda mrembo wangu mfanyakazi mwenzake ambaye amemzidi elimu na mshahara na Bosi wake wa kazini, kichwa kikawaka moto sana. Ndani ya wiki ya kuwa pale niliulizwa unaondoka lini zaidi ya mara kumi (ndugu zangu tutafute pesa). Siku ikafika nikaondoka

Penzi likaanza kushuka, mimi wivu umenijaa sina pesa, wasiwasi wa kuchapiwa ni mkubwa zaidi.

Mwezi mmoja mbele nikatafuta uongo mwingine nikampanga mrembo wangu niende kijijini tena mana msimu wa baridi ulikua umeanza, akakubali nikaenda kijijini bana.

Safari nikafanya kitu cha tofauti nimeshuka stendi pale kijijini nikaenda moja kwa moja kazini kwake nikaa nje pale namsubiri mrembo wangu amalize kazi twende nyumbani kwake ambapo kitu pekee ambacho nimenunua ni dustbin, basi nimekaa pale nje yeye akiwa hajui kama niko pale hadi muda wa kutoka unafika, anatoka nje ananikuta pale nje nimechakaa vibaya mno, suruali langu limepauka na shati la mtumba akaona aibu akanifata pale kwa sauti ya chini ‘Kwanini umenifata kazini?’ Mimi natabasam tu tayari nikijua nimeshavuruga, basi akamliza taratibu za kazini ikafika muda wa kwenda nyumbani, oyaaa niliambiwa nitangulie nipande boda kwamba yeye amevaa sketi fupi hatuwezi panda mshikaki kwenye boda moja, sina akili ila hapa nilichekecha fasta nikagundua mrembo tayari nimeshamchosha na hataki watu wajue kama tuko pamoja, nikaona sio kesi nikatangulia.

Safari ndio ilikua ya moto sana nilishika simu yake nikakuta anachati na yule mfanyakazi mwenzake yani mrembo wangu ndio anamuomba jamaa aende kwake nilivurugwa, haya kuhusu boss wake nae wanachati vile ambavyo unaona kabisa mrembo ‘ataliwa’ soon. Basi ikawa ugomvi hapo ila mrembo wala hawazi wala nini akatoka zake nje akawa anapiga story na wapangaji wenzie, mimi kijana mpumbavu ndio nikabaki ndani naumia moyoni, badae mrembo akarudi akanidanganya danganya nikakubali nikawa sawa kiasi chake ila moyoni najua tayari nafasi yangu haipo.

Sasa muda wa kuondoka ukafika sina nauli, mrembo wangu akanipa nauli na pesa ya kula njiani akanisidikiza kupanda gari nikarudi kwetu.

Wiki kama tatu mbele mrembo wangu akasema hataki tena kuwa na mahusiano wala urafiki na mimi, kiufupi nifanye kama hatujawahi kufahamiana. Nilijua kama ipo siku ataniacha ila sikutarajia kuwa iwe wakati ule niliumia sana, nilikua najifungia ndani kila siku nalia, nikajiingiza kwenye ulevi nikawa mtu wa hovyo sieleweki.

Tamisemi mmenifukizia njiwa wangu
Hamna cha TAMISEMI broo kamuulize Adam au Samson.Mwanaume unaliaje yani ongeza hayo machungu kwenye juhudi yaani ikupe hasira tafuta maisha wanawake wote wako hivyo ukipata hela na wewe utaitiwa kipochi.
#wacha ulevi tafuta mapene
 
Back
Top Bottom