Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

Jamaa kajenga mazingira hadi watu wanamuona mwema,ajabu sana.

Eti kamuandalua supu,kamuona hospitalini.Itakuwa ndio tabia yake ya kuwawekea mabinti madawa ya kulevya na kisha kulala nao
Mbona una hasira sana?? Ulitaka kila mtu asimame upande wako?? Wewe ulishawahi kufanyiwa hivyo??

Mleta uzi kaleta hoja na anaomba ushauri, yeye, akili yake na moyo wake ndio utapima nini afanye.. Hakuna Guarantee kwa tunachoshauri hapa ndiyo kiwe lazima kifanywe na huyo dada. Na hata wewe unachoshauri sio lazima akifanye, na Psychologically mtu akifikia step ya kuomba ushauri ina maana ana two sides which are favorable na anaweza opt yeyote ile ambayo itampa haueni ya moyo wake... Hapa tunashauri tu kama anaweza kusamehe ni bora kufanya hivyo kuliko kupoteza muda na pesa zake. Kumbuka tu huyo kijana pamoja na aliyoyafanya inawezekana ana watu wanaomtegemea, kumfunga kunaweza haribu maisha ya watu walio nyuma yake na hata wewe uliyefunga ukaishia kusononeka au ukakumbwa na mikosi tu ya wale wanaosononeka juu ya ulichokifanya. Njia pekee ya kutatua mizozo kama hii ni kusameheana tu.. Ni wangapi mnalalwa kwa offer za Savanna tatu tu bila hata ridhaa yenu?? Tena wengine mpaka kukimbiwa mnakimbiwa mnajikuta asubuhi mko wenyewe...

Na wewe unayehukumu huyo jamaa ndiyo tabia yake umeyajulia wapi hayo?? Au na wewe alikubaka pia??


Grow up and act like a grown-a** woman...
 
Huwa unapanda gari lake kila siku! Jiulize kama angekutongoza ungekubali au ungekataa?
 
kwan unampenda? na unauhakika haitakusumbua kisaikolojia kama utaamua kuuchuna? kama kweli kimekuuma mi naona bora umwaribie maana hata yeye amekuharibu. for me take it foward
 
pole dada yangu,muhmu muchukue jamaa mkapime ikiwa hajaambukiza wewe UKIMWI,Nakama itathibitka hajakuambukiza msamehe kwani kaiacha kama ilivyo ila kama kakumbukiza ni bora kumshtaki atakuwa kaharbu future yako.
 
wafaransa wana msemo wao wanakwambia Quid pro Quo yaani ("something for something" in Latin yaani we kila siku upande lift ya watu kwenda na kurudi ofisini alafu vyako vikiliwa kidogo tu unaanza makelele.acha roho mbaya msamehe saba mara sabini


Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.

Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.

Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa

Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.

Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.

Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.

Nipo njia panda nahitaji msaada wenu

Asanteni
 
Ulienda kwa ajili ya counseling? Kama bado hujaonana na washauri nasaha uende na useme ulibakwa. Kuna issue ya mimba na ukimwi. Lakini pia huyo ni mhalifu, nenda tgnp ama lhrc ukawaeleze upatiwe msaada wa kisheria.

Ukilogwa ukaolewa na huyo mwanaume asiejua kutongoza, kesi za kubakwa zitakuwa sehemu ya ndoa yenu na utalia machozi hadi kifo kikutangulize. Usione aibu, huna tofauti na mtu alieibiwa. Huwezi kuona aibu kushtaki polisi manake watajua unapoishi na kuona kasoro zako.

Kama unahitaji kuongea zaidi njoo pm. Unahitaji support kutoka kwa mtu unaemuamini sana, ndugu ama rafiki wa karibu atakufaa pia. Pole sana, you will survive this.
 
Mkuu tumroge tuu huyo jamaa ama unaonaje?

Back to topic
Jamaa inaonekana ndo tabia yake na sio bahati mbaya. Huyo alikuwa keshajiandaa kabisaa na mzigo.
Huyu si wa kuroga huyu ni wa kumpeleka kwa pilato moja kwa moja akaeleze na mtandao wake wote
 
Pole sana kwa tukio baya hilo
  • Huyo ni mtu hatari. Keshawafanyia wangapi na ataendelea kuwafanyia wangapi kama wewe? hata mkishaoana kama anavyojaribu kukupooza.Ina maana alishapanga kwa muda mrefu. Amekubuhu huyo nduli
USHAURI WANGU:
  1. Pima kwanza vitu viwili. HIV na mimba
  2. Achana naye kabisa huyo jambazi wa miili ya watu. Ni mtu katili. Hafai hata kwa bure
  3. Kama namba 1 iko safi kwa maana huna mimba wala HIV,katoe sadaka kwa yatima na umshukuru muumba wako
  4. Kama namba 1 si safi,hiyo kitu ni kuhakikisha inafungwa jela ili kuepusha watu wengine wasiingie kwenye mtego huo. Mwache akakutane na wanaume wenzake huko
  5. Ukome kuhang na wanaume bila kuchukua tahadhari
  6. Usisahau Mungu kumshukuru sana maana ungeweza kuwa uko timu moja na akina John komba muda huu
 
Pamoja na kuwa sikubaliani na ustaarabu wa kujiandikishia lift ya kila siku, kumpa mtu lift haikupi haki ya kubakwa. Mola ayaepushe maneno haya yasikurudie kwa mwenza wako ama ww mwenyewe (wanaume wanabakwa pia baba)
wafaransa wana msemo wao wanakwambia Quid pro Quo yaani ("something for something" in Latin yaani we kila siku upande lift ya watu kwenda na kurudi ofisini alafu vyako vikiliwa kidogo tu unaanza makelele.acha roho mbaya msamehe saba mara sabini
 
kaaa wee then kumbuka kuna HIV + UJAUZITO Sijaona kama kuna kipengele umekiandika una hofu ya vitu hivyoo.kumbe na imekunogea ww wine hiyoooo,inakutoboa ,au ulisahau kuandika ?au mulitumia zana? wee ndoa tuu
 
Hamjifunzi tu! Usiwe karibu na mwanaume kama huna interest nae unless otherwise ndio kama yaliyo kukuta wengi wanafanyiwa hivyo japo hawasemi bora usalama tu, so kacheck afya before hujakitana na huyo jamaa mwingine. Pole.
 
kaaa wee then kumbuka kuna HIV + UJAUZITO Sijaona kama kuna kipengele umekiandika una hofu ya vitu hivyoo.kumbe na imekunogea ww wine hiyoooo,inakutoboa ,au ulisahau kuandika ?au mulitumia zana? wee ndoa tuu
Hii imekaa Kama nataka Sitaki vile, pengine alinogewa huwezi jua
 
Ulienda kwa ajili ya counseling? Kama bado hujaonana na washauri nasaha uende na useme ulibakwa. Kuna issue ya mimba na ukimwi. Lakini pia huyo ni mhalifu, nenda tgnp ama lhrc ukawaeleze upatiwe msaada wa kisheria.

Ukilogwa ukaolewa na huyo mwanaume asiejua kutongoza, kesi za kubakwa zitakuwa sehemu ya ndoa yenu na utalia machozi hadi kifo kikutangulize. Usione aibu, huna tofauti na mtu alieibiwa. Huwezi kuona aibu kushtaki polisi manake watajua unapoishi na kuona kasoro zako.

Kama unahitaji kuongea zaidi njoo pm. Unahitaji support kutoka kwa mtu unaemuamini sana, ndugu ama rafiki wa karibu atakufaa pia. Pole sana, you will survive this.

Siwaelewi wadada wanasema walibakwa halafu wanachelewa kuchukua hatua za kisheria na kisaikolojia. Tatizo huwa ni nini? Sitaki kuamini kuwa ni hofu. Nahisi na wao wana jambo wanaficha ambalo kwa mtazamo wangu ni 'uhusika wao katika kushawishi/kutengeneza mazingira ya kubakwa'.

I stand to be corrected ila iwekwe kwenye hansard kuwa sikubaliani na suala la kumsamehe MBAKAJI. Sheria na ichukue mkondo wake.



Kumbuka tu huyo kijana pamoja na aliyoyafanya inawezekana ana watu wanaomtegemea, kumfunga kunaweza haribu maisha ya watu walio nyuma yake na hata wewe uliyefunga ukaishia kusononeka au ukakumbwa na mikosi tu ya wale wanaosononeka juu ya ulichokifanya.

Grow up and act like a grown-a** woman...

Mh! mbona nawe umetumia hasira sana kujibu bro? It was uncalled for.

Point yangu iko kwenye hicho nilicho-quote, ARE YOU REALLY SERIOUS!???????????????????????

Lastly, kama kweli uko serious na kutoka moyoni umemaanisha ulichokiandika basi hiyo sentensi yako ya mwisho na ikurudie.

Ni hayo tu, I hope na mimi sijakujibu kwa hasira sana!
 
yote hiyo si kupenda rahisi,we kila siku lift,mpaka saa nane usiku unasubiri lift tu tena jinsia mbili tofauti,hata ningekuwa mimi nisingemuacha akupe lift bure kila siku kwani ni ndugu yako huyo??

Pamoja na kuwa sikubaliani na ustaarabu wa kujiandikishia lift ya kila siku, kumpa mtu lift haikupi haki ya kubakwa. Mola ayaepushe maneno haya yasikurudie kwa mwenza wako ama ww mwenyewe (wanaume wanabakwa pia baba)
 
Huyo mwanaume anastahili kufungwa jela, haijalishi alikuwa na hisia au hakuwa nazo. Hicho ni kisingizio cha kijinga sana, ameona utamfunga hivyo anaamua liwalo na liwe tu, akuoe then huko ndoani huwezi kujua atakufanya nini, watch out, he deserves to be imprisoned.
Japo huo uchumba wa tangu July last yr sioni ukizaa ndoa, angekuwa amekuja kiustaarabu ningekushauri umkubali muoane, lakini kwa gear ya kubwakwa, nope...anastahiki jela huyo!!!
kaka lakini binti mwenyewe anaonekana kumpenda huyu jamaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom