immaculata rose
New Member
- Jan 10, 2016
- 3
- 15
Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.
Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.
Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa
Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.
Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.
Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.
Nipo njia panda nahitaji msaada wenu
Asanteni

Last edited by a moderator: