Kanisa limekataa kusalisha ibada ya mazishi ya Mushi

Kanisa limekataa kusalisha ibada ya mazishi ya Mushi

Matumaini ya nini? Sala au mahubiri yo yote wakati wa mazishi siyo kwa ajili ya marehemu bali ni kwa ajili ya wale walio hai. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu kwa hiyo kama aliyekufa hakutengeneza mambo yake na Mungu kabla hajafa sala yoyote baada ya kufa haina impact kwa marehemu. Hakuna sala inayoweza kumwondoa mtu kuzimu na wala hakuna purgatory kulingana na Biblia takatifu.

mimi nahamini zinasaidia kila mtu na imani yake.kila binadamu anafanya dhambi ni sala pekeyake zitasaidia.

lisilo wezekana kwako kusamehe kwa mungu linawezekana
 
Tatizo la msingi hapa ni watu kuwa na uelewa mdogo, au kutosoma michango ya wenzao.

Wako wanaodai kwamba Biblia inasema ukifa unahukumiwa saa hiyo hiyo na kwa hivyo sala za baadaye hazikusaidii. To that I say; "non sequitur", it does not follow!

It is Biblical that God is not bound by time. All times are available to Him. Intercessions for the dead are available to Him, at the moment of judgement, irrespective of when they are made.

Pia, ni lazima kusoma sehemu zote za Bablia, na kuzielewa kwamba hazipingani. Ni tafsiri mbaya tu ndizo zinapingana.

Iko sehemu ya Biblia inayosema ukifa unahukumiwa na iko inayosema ni jambo bora kufanya sadaka kwa ajili ya marehemu (2Maccabees 12:46). Hazipingani. Kushindwa kuelewa kwamba Mungu habanwi na nyakati ndipo kunafanya baadhi ya watu wadhani kwamba ukishakufa huwezi kunufaika tena na sala.

When we die we exit the Church Militant, we cannot pray for ourselves anymore, but the Church Militant can pray for us.
 
Sio kugoma hiyo ni taratibu za makanisa yote kwa mtu aliyejiua mwenyewe na ambaye amejitenga na kundi la Bwana. Yaani kaasi kanisa. Huyo mtu hazikiwi na kanisa. Hata Padri/Mchungaji akija haendeshi misa ya mazishi.
Marehemu Mushi aliyefanya mauaji ya mama wa mtangazaji wa ITV na kujeruhi kwa risasi na atimaye kujiua amezikwa bila huduma ya kikanisa.

Kanisa Katoliki parokia ya Uru imegoma kusalisha misa ya marehemu Mushi kutokana na mazingira ya kifo chake.

Familia ilitaka marehemu aombewe na kanisa ili asamehewe dhambi zake sababu atoaye hukumu ni Mungu si binadamu na ajuaye ukweli ni Mungu.

Lakin kanisa imekataa kusalisha ibada na Mushi amezikwa bila ibada.
 
kwani kifo ni hukumu?

Inapotekelezwa kwa uwezo wa kibinaadam inakuwa hukumu.. Mfano pale mshtakiwa anapohukumiwa kunyongwa ni hukumu ile.. Ni sawa na unapochukua uamuzi wa kujiua.. Ni hukumu umejipa hiyo..
 
Marehemu Mushi aliyefanya mauaji ya mama wa mtangazaji wa ITV na kujeruhi kwa risasi na atimaye kujiua amezikwa bila huduma ya kikanisa.

Kanisa Katoliki parokia ya Uru imegoma kusalisha misa ya marehemu Mushi kutokana na mazingira ya kifo chake.

Familia ilitaka marehemu aombewe na kanisa ili asamehewe dhambi zake sababu atoaye hukumu ni Mungu si binadamu na ajuaye ukweli ni Mungu.

Lakin kanisa imekataa kusalisha ibada na Mushi amezikwa bila ibada.

Hivi kumbe mu wageni wa unafiki wa wakatoliki? Wanamhesabia dhambi marehemu badala ya kufika kuwafariji wafiwa! Na ninakuhakikishia angekufa fisadi mwenye pesa nyingi za wizi angezikwa na askofu, kwa heshima zote za kanisa! Yani wao katika msiba wa Mushi hawakuona ndugu zake wanaohuzunika wanaohitaji kufarijiwa, walichoona ni maiti ya "muuaji" au/na "mzinzi", na hao mapadri wanajisahau kuwa mwenye kuhukumu ni Mwenyezi Mungu, na kwamba anayehitaji hiyo ibada ni wale waliobaki na wala si yule mfu.
 
ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani

Na lengo la kitendo hiki ni nini? Kwani wafiwa (wenye huzuni wanaohitaji ibada) wamehusika vipi na kitendo cha kujitoa uhai? Hapa wanaoadhibiwa kwa kitendo hiki ni wafiwa wenye huzuni na wala si huyo aliyejiua. Kwahiyo unaamini kuwa nduguyo akijiua hustahili kufarijiwa katika huzuni hiyo? Na je, watu wa kanisa mnafahamu kuwa kujiua ni matokeo ya ugonjwa wa akili? Kwamba ugonjwa wa akili unaweza kusababisha kifo (kwa kujiua) kama malaria inavyosababisha kifo? Kwanini mnahukumu marehemu? Huu ni unyanyapaa wa wazi kabisa, na ni uzandiki na unafiki mkubwa!
 
Tatizo la msingi hapa ni watu kuwa na uelewa mdogo, au kutosoma michango ya wenzao.

Wako wanaodai kwamba Biblia inasema ukifa unahukumiwa saa hiyo hiyo na kwa hivyo sala za baadaye hazikusaidii. To that I say; "non sequitur", it does not follow!

It is Biblical that God is not bound by time. All times are available to Him. Intercessions for the dead are available to Him, at the moment of judgement, irrespective of when they are made.

Pia, ni lazima kusoma sehemu zote za Bablia, na kuzielewa kwamba hazipingani. Ni tafsiri mbaya tu ndizo zinapingana.

Iko sehemu ya Biblia inayosema ukifa unahukumiwa na iko inayosema ni jambo bora kufanya sadaka kwa ajili ya marehemu (2Maccabees 12:46). Hazipingani. Kushindwa kuelewa kwamba Mungu habanwi na nyakati ndipo kunafanya baadhi ya watu wadhani kwamba ukishakufa huwezi kunufaika tena na sala.

When we die we exit the Church Militant, we cannot pray for ourselves anymore, but the Church Militant can pray for us.

Don't be deceived. There is no prayer that will change anything after death. If you want to go to heaven you repent your sins and amend your ways now. Remember the story of the rich man and Lazarus in Luke. My friend, it is now in this body or never.
 
ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani
Dhambi ni Dhambi tu iwe kunywa pombe au kunywa sumu hapa kanisa linafanya makosa
 
mimi nahamini zinasaidia kila mtu na imani yake.kila binadamu anafanya dhambi ni sala pekeyake zitasaidia.

lisilo wezekana kwako kusamehe kwa mungu linawezekana

Hizo sala ni kweli zinasaidia kila anayetaka isipokuwa marehemu. Mtu anatakiwa akiri kwa kinywa chake kumpenda Mungu na siyo kusaidiwa na watu wengine. Kwa imani hizi potofu imefika mahali watu wanamwelekeza Mungu mahali pa kuwaweka wanaokufa. Ndiyo maana utasikia mweke mahali pema peponi hata kama kajiua au alikufa akizini. Huku ni kujidanganya. Hats akizikwa na askofu haibadilishi cho chote kama alikuwa mwenye dhambi.
 
Si sahihi kusema ukifa maombi hayakusaidii. Mbona Martha alimwombea ndugu yake Lazaro kwa Yesu, baada ya Lazaro kufa, na Yesu akamfufua?

God exists outside time. Sala za baada ya mtu kufa ni available to God at the moment of judgement. Si za baadaye maana hakuna baadaye huko, kwani hakuna time.

Hatujui kama mtu yeyote amepotea. Hilo tunamwachia Mungu. Letu ni kuomba bila kuchoka.

Yesu alimfufua Lazaro si kwa sababu ya maombi ya Martha. Soma tena kwenye Biblia katika Yohana 11:11-45. Lengo la Yesu katika andiko hili linaonekana katika mstari wa 25 na 26 anaposema kuwa yeye ndiye ufufuo na uzima, na kwamba amwaminiye hatokufa. Lengo linahitimishwa kwenye mstari wa 45 ambapo tunaambiwa walipoona alichokifanya Yesu walimwamini. Kwa hiyo Yesu alikusudia mwenyewe kumfufua Lazaro ili kuwajenga kiimani waliokuwepo na si kwa maombi ya yeyote. Kukuthibishia hilo, jaribuni leo kumwombea yeyote aliyekufa hata kama mlimpenda vipi, muone kama atafufuka. Hatofufuka ng'o! Tendo lile alilifanya Mungu wakati ule kwa kusudio maalum la kimungu, si la kibinadamu. Yapo mengine mengi ya namna hiyo katika Biblia, mojawapo ni ile mana waliyoteremshiwa wana wa Israel jangwani enzi za Nabii Musa. Hii haimaanishi kwamba eti hata leo mnaweza kuomba Mungu awadondoshee makande kutoka mbinguni! Leo hii hata mkikesha katika maombi, mana haitoshuka.

Ibada ya mazishi si kwa ajili ya aliyekufa, la hasha. Ni fursa ya walio hai kutengeneza maisha yao na Mungu kwa kutumia kumbusho hilo la wazi la kifo cha mpendwa wao, na hii fursa itaweza kutumiwa kwa manufaa kama mtumishi wa kiroho (padri/mchungaji) atakuwepo kuiongoza. Kanisa linapowasusa wafiwa linakuwa limepoteza fursa na limewatelekeza wenye huzuni katika wakati ambao wanahitaji sana kufarijiwa. Aliyekufa anaelekea kwenye hukumu yake ambayo walio hao hawahusiki nayo. Waliobaki katika huzuni na majonzi ndio wanaohitaji faraja na maelekezo ya kukabiliana na hali hiyo huku wakiendelea kushikamana na Mungu, na hiyo ndiyo jukumu la ibada ya mazishi.
 
Hata mama yake Ufoo ni favor walifanya, alitakiwa asukumiwe shimoni kama mzoga tu. Mungu tunusuru, utu umetutoka hatuna tofauti na wanyama. Bwana alitoa na bwana ametwaaa Jina lake libarikiwe. AMINA
 
.... Kukuthibishia hilo, jaribuni leo kumwombea yeyote aliyekufa hata kama mlimpenda vipi, muone kama atafufuka. Hatofufuka ng'o! Tendo lile alilifanya Mungu wakati ule kwa kusudio maalum la kimungu, si la kibinadamu. .....
Na huyo Mungu uwezo wake kufufua "ulikoma" lini?
 
Hio familia ya mushi ingekata hela ya mboga!
Sasa hivi ungeona wachungwaji wana changamkia tenda!
Jamaa laana kwa pesa wale!!
Teh teh teh teh
 
Back
Top Bottom