Kanisa limekataa kusalisha ibada ya mazishi ya Mushi

Kanisa limekataa kusalisha ibada ya mazishi ya Mushi

Sasa kanisa lina uthibitisho gani kama alijiua au aliuwawa wakati uchunguzi bado kukamilika!!? Huku ni kuchukua sheria mkononi!
Mkuu,
Halafu kitu cha kushangaza kanisa Hilo husika na baadhi ya hao wanaoliongoza ndio wanaongoza kwa kashfa za Kulawiti watoto wa kiume na kutafuna wake za watu kwenye parokia :noidea:....Kama sio unafiki sijui hii ni kitu gani!!
 
kanisa halijafanya kosa.kama kweli mushi kajiua
 
Mambo ya imani!!! we acha tu! kwa hiyo huenda mushi anateseka huko aliko kwa kuwa Mungu hajapata msimamo wa kanisa amuhifadhi mahali gani!!!

akiombewa na kanisa anaweza kusamehewa dhambi ndio maana tunaomba asamehewe ata waislam uomba tumsalie mtume ili asamehewe.
 
Wanafiki mafisadi yanaiba mali za wanyonge wanaombewa, wao ndiyo wanahukumu? Kama jamaalijutia kosalake dk chache kabla ya kufa watajuaje wanajivika umungu.

apo sasa ndio panachanga ndugu zake wamejisikia vibaya sana
 
Huu utaratibu wa Kanisa Katoliki kukataa kumuombea mtu aliyejiua sio 'Universal'. Baadhi ya nchi nyingine wanamzika muumini mwenzao bila kujali chanzo cha kifo. Sifahamu kwa nini Kanisa Katoliki Tanzania limetoa wapi huu utaratibu?

Na kuhusu kifo cha Mushi, Kanisa lina uhakika gani kuwa Mushi amejiuwa mwenyewe? Wamefanya uchunguzi lini? Na kwanini kanisa linafanya kinyume na kilichoandikwa kwenye biblia, na kutoa hukumu?
Hao waliokataa kumzika Mushi wanataka watu waamini kuwa ni wasafi?
 
Usipotoshe.Martha alimuomba Yesu amuombee wakati Lazaro bado mgonjwa sio alipokwishafariki.

Labda husomi Biblia; Lazaro alikufa, akazikwa na kukaa kaburini siku nne kabla Yesu hajawasili kwenye msiba na kumfufua.

Pia, someni 2 Maccabees 12:46 "Thus he made atonement for the dead that they might be freed from their sin". Caution: kama Biblia yako ni ya Kiprotestanti basi itakuwa na upungufu wa vitabu saba, ikiwa ni pamoja na vitabu viwili vya Maccabees.

Msingi wa kutoelewa kwa wengi hapa ni kutofahamu kwamba NATURE yetu ni tofauti na NATURE ya Mungu. Angalia tofauti kubwa iliyoko kati ya NATURE ya binadamu na ya mti au mnyama. Iko tofauti kati ya nature yetu na nature ya malaika, na nature ya malaika na ile ya Mungu.

God is not bound by time. Scripture says that He knew you before you were born.

Sala anayosaliwa mtu miaka mia baada ya kufa iko machoni mwa Mungu siku aliyokufa huyo mtu. Mungu anaona, ahead of time, sala zako, and He factors them into the judgement.

Mtu anayezikwa bila viongozi wa Kanisa kuweko bado anaombewa. Ningependa wawepo hao viongozi lakini.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Usipotoshe.Martha alimuomba Yesu amuombee wakati Lazaro bado mgonjwa sio alipokwishafariki.

Hapana. Yesu alimuombea Lazaro akiwa ameshafariki, na ndio sababu Martha alimuona Yesu alimuambi angefika mapema ndugu yake (Lazaro) asingekufa.
 
Mm huwa sioni maana sana ktk kanuni kama hizi, kama Mungu angekua anatuhesabia maovu hata hao makasisi wasingefaa kuzikwa hata na wafanya usafi wa kanisa, wanadamu tuache unafki.
 
wanafki tuu utamuukumuje mtu kama muumini misa anaudhuria sadaka anatoa kwanini msimuombee
 
ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani

...Ila kama ulikuwa Wewe/Familia inajiweza na ina Vijisenti vya kutosha Wachungaji wanweza kugombea kuja kumfanyia Ibada marehemu. Inasikitisha sana kwamba siku hizi Fedha zimeingia hata makanisani. Dhambi yako yoyote inaweza 'Kusamehewa' ili mradi una mfuko unaojitosheleza na kuweza kuwatosheleza Wengine!
 
Mkuu,
Halafu kitu cha kushangaza kanisa Hilo husika na baadhi ya hao wanaoliongoza ndio wanaongoza kwa kashfa za Kulawiti watoto wa kiume na kutafuna wake za watu kwenye parokia :noidea:....Kama sio unafiki sijui hii ni kitu gani!!

hizo ni double standards.nadhani huwa wanaangalia upepo umekaaje.
 
huo ndio msimamo wa kanisa kutosoma misa ya mazishi kwa mtu aliyekatisha uhai wake mwenyewe na kwa bahati mbaya kanisa linaongozwa kiimani na sio siasa kwamba kila kitu utahoji ilikuwaje.....cha msingi ni kuheshimu uhai wako na wa mwenzako kwani hii ndio zawadi kubwa kuliko zote kutoka kwa Mungu.
 
Hakuna mwenye haki ya kumhukumu mtu katika hii dunia...kwasababu hakuna mwenye uhakika Mushi kajiua...
Lakini pia sala ya kumuombea marehemu haibadilishi hukumu yake,Ivo ndugu wasiumie sana
 
Sasa kanisa lina uthibitisho gani kama alijiua au aliuwawa wakati uchunguzi bado kukamilika!!? Huku ni kuchukua sheria mkononi!

Sasa ni kwanini ndugu walimpeleka kuzika kabla uchunguzi haujakamilika ili kujua ameuawa au amejiua mwenyewe???
 
Mambo ya imani!!! we acha tu! kwa hiyo huenda mushi anateseka huko aliko kwa kuwa Mungu hajapata msimamo wa kanisa amuhifadhi mahali gani!!!

Ewaaaaa ndicho wanataka kutuaminisha. Mungu hajui taarifa za mwanadamu anayekufa mpaka makasisi duniani wapeleke file..
 
Labda husomi Biblia; Lazaro alikufa, akazikwa na kukaa kaburini siku nne kabla Yesu hajawasili kwenye msiba na kumfufua.

Pia, someni 2 Maccabees 12:46 "Thus he made atonement for the dead that they might be freed from their sin". Caution: kama Biblia yako ni ya Kiprotestanti basi itakuwa na upungufu wa vitabu saba, ikiwa ni pamoja na vitabu viwili vya Maccabees.

Msingi wa kutoelewa kwa wengi hapa ni kutofahamu kwamba NATURE yetu ni tofauti na NATURE ya Mungu. Angalia tofauti kubwa iliyoko kati ya NATURE ya binadamu na ya mti au mnyama. Iko tofauti kati ya nature yetu na nature ya malaika, na nature ya malaika na ile ya Mungu.

God is not bound by time. Scripture says that He knew you before you were born.

Sala anayosaliwa mtu miaka mia baada ya kufa iko machoni mwa Mungu siku aliyokufa huyo mtu. Mungu anaona, ahead of time, sala zako, and He factors them into the judgement.

Mtu anayezikwa bila viongozi wa Kanisa kuweko bado anaombewa. Ningependa wawepo hao viongozi lakini.

Hapana. Yesu alimuombea Lazaro akiwa ameshafariki, na ndio sababu Martha alimuona Yesu alimuambi angefika mapema ndugu yake (Lazaro) asingekufa.
Hii league naona haitatufikisha popote.Ikiwa unaona ''imani'' yako itakuokoa endelea na maisha bila KUTENGENEZA au kuomba rehema kabla hujafa ukisubiri siku ukifa utasaliwa misa.
Mathayo 5:8
 
ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani
inamaana wameshamuhukumu alijitoa uhai wakati hata upelelezi haujakamilika? not good.
 
Hilo kanisa liko corrupted! kwa kufanya hivyo ina maana wamemhukumu marehemu jambo ambalo si kazi ya mwanadamu!, Ibada ingeleta faraja kwa wafiwa na waombolezaji wengine, and who knows pengine watu wangebadilisha maisha yao kupitia ibada hiyo??
 
akiombewa na kanisa anaweza kusamehewa dhambi ndio maana tunaomba asamehewe ata waislam uomba tumsalie mtume ili asamehewe.
acha kujifariji wewe, biblia inasema baada ya kifo ni hukumu!! maombi au sala juu ya marehemu hayasaidii chochote zaidi ya kufariji wafiwa!!
 
Back
Top Bottom