We nawe peleka povu lako banda la uani!!
Mkuu punguzeni sana mambo ya sadaka!mnashindwa kumsalia bila sababu ya msingi mnakuwa tayari kupiga kelele usiku mzima
We nawe peleka povu lako banda la uani!!
Marehemu Mushi aliyefanya mauaji ya mama wa mtangazaji wa ITV na kujeruhi kwa risasi na atimaye kujiua amezikwa bila huduma ya kikanisa.
Kanisa Katoliki parokia ya Uru imegoma kusalisha misa ya marehemu Mushi kutokana na mazingira ya kifo chake.
Familia ilitaka marehemu aombewe na kanisa ili asamehewe dhambi zake sababu atoaye hukumu ni Mungu si binadamu na ajuaye ukweli ni Mungu.
Lakin kanisa imekataa kusalisha ibada na Mushi amezikwa bila ibada.
akiombewa na kanisa anaweza kusamehewa dhambi ndio maana tunaomba asamehewe ata waislam uomba tumsalie mtume ili asamehewe.
Maajabu haya. Yawaje tena kanisa kuhukumu kabla ya muumba? Mmmh!
Lkn haya ndio matokeo ya kujisajili ktk kanisa na kuitwa muumini wa kanisa fulani badala ya kuitwa muumini wa dini fulani.
Nimeisikia hii habari kwenye Nipashe leo
Siku hizi Nakala ya Nipashe huwa inatolewa kwa mfumo wa sauti?
Hapana. Yesu alimuombea Lazaro akiwa ameshafariki, na ndio sababu Martha alimuona Yesu alimuambi angefika mapema ndugu yake (Lazaro) asingekufa.
Marehemu Mushi aliyefanya mauaji ya mama wa mtangazaji wa ITV na kujeruhi kwa risasi na atimaye kujiua amezikwa bila huduma ya kikanisa.
Familia ilitaka marehemu aombewe na kanisa ili asamehewe dhambi zake sababu atoaye hukumu ni Mungu si binadamu na ajuaye ukweli ni Mungu.
Unaegemea Biblia; ni sawa. Lakini Biblia hiyo hiyo inakuambia ni jambo jema kuwaombea marehemu. I quoted 2 Maccabees, Chapter 12. Isome hiyo chapter nzima. Na hasa angalia mstari wa 46, lakini ukisoma chapter nzima utaelewa vizuri zaidi.
Do not read only certain parts of the Bible. If you are going to base yourself entirely on the Bible, then you should at least be familiar with the whole of it.
kwa hiyo hao mapadre walikuwepo wakati anajiua wakashuhudia? au wameshapewa ripoti ya uchunguzi ya polisi inayoonesha kwamba amejiua?? au nao wamesikia kama sisi tulivyosikia?ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani
Marehemu Mushi aliyefanya mauaji ya mama wa mtangazaji wa ITV na kujeruhi kwa risasi na atimaye kujiua amezikwa bila huduma ya kikanisa.
Kanisa Katoliki parokia ya Uru imegoma kusalisha misa ya marehemu Mushi kutokana na mazingira ya kifo chake.
Familia ilitaka marehemu aombewe na kanisa ili asamehewe dhambi zake sababu atoaye hukumu ni Mungu si binadamu na ajuaye ukweli ni Mungu.
Lakin kanisa imekataa kusalisha ibada na Mushi amezikwa bila ibada.
Sasa kanisa lina uthibitisho gani kama alijiua au aliuwawa wakati uchunguzi bado kukamilika!!? Huku ni kuchukua sheria mkononi!
Mahakama hazitoi haki ya kweli, anayejua kuongea ndo anashinda kesi hata kama yeye ndo mwenye hatia.Hapo kwenye nyekundu ndipo kwenye utata. Au Kanisa siku hizi linafanya kazi za Mahakama na kutoa HUKUMU ?
Nadhani kanisa linachofanya si kuhukumu bali kujiweka mbali na mambo yenye utata lisije wachanganya kondoo. Kama unaonekana umejiua halafu kanisa ati linakufanyia misa hii itaonekana kuwa kumbe hata ukujiua ni sawa tu. Tukumbuke kuwa kama hakujiua ila kauawa, Mungu bado atampokea tu kwani yeye ndo anaujua ukweli wote.Ikitokea saa ama siku yoyote mkristo amekataliwa kupumzishwa kwa heshima mwili wake basi mmpeleke evangelical churches wao watamzika kwa heshima zote na ibada itafanywa kwaajili yake ambayo yaweza waleta wengi kwa kristo.....
For us its an opportunity to extend the love of Christ to the rejected. Kama yeye alimkubali jambazi aliposulubiwa pale Calvary na kusamehe wauaji wake na wengine wote waliomtenda vibaya then we have the same spirit that he had which persuaded him to love and forgive unconditionally!
Una hakika hajawahi kuingia kanisani mkuu?Rais ni Muislam, dini ambayo hairuhusu muumini wake kujumuika katika ibada ya imani nyingine. Kuingia kanisani kungeashiria vingine katika msimamo wa imani yake. Hayo ya kuleta kiti mkuu naona ni ushabiki wa kijiweni tu.
Mombolezo na sherehe ruksa.
Hivyo Waislam wanajumuika na wengine kwenye msiba na maziko bila kuingia kanisani na kusali...
Nakubaliana na mawazo yako - Kwa upande wa Wa-Kristo nakumbuka kwenye Biblia Bw. Yesu alipokuwa msalabani, alikuwa kati ya wahalifu wawili, mmoja wapo aka-kiri kuwa na imani naye, Bw. Yesu akamwambia leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso!Jamani hata kama ajaombewa kama alimkumbuka Mungu kabla mauti aijamkuta na kusema asamehewe basi Mungu atamsamehe lakini akuna hata kqenye maandiko mahali pameandikwa watu wengine au viongozi wa kanisa wanaweza kukuombea ukasamehewa dhambi zako huo ni uongo na akuna kiti kama hicho daima,
Maisha yako ya badaye unajiandalia peke yako kwa kumuomba Mungu kila mara na akusamehe dhambi zako ila siyo padri wala mchungaji eti atakuja kukuombea dhambi usamehewe mbinguni.