Kanisa limekataa kusalisha ibada ya mazishi ya Mushi

Kanisa limekataa kusalisha ibada ya mazishi ya Mushi

Hakuna mtu anaweza kumuhukumu mtu mwezake!

Kufanya ibada kwa marehemu ni heshima kanisa linatoa kwamarehem na ndugu wa marehem. Ni namna ya kuwaonesha binadamu wengine kwamba ukiishi vizuri hapa duniani utapata heshima fulan. Ni sawa na kumtangaza mtu mtakatifu lengo ni kutaka watu waliobaki hapa duniani Waige matendo yake. Hayo mengine kwmba mungu anapokea sala zetu au la sio kazi yetu. Sisi wajibu wetu kusali mengine ni ya mungu. Kwa hiyo liangalieni swala la mushi km kinyimwa heshima ya maziko ya kikanisa na sio hukum. Kanisa halijamhukum bali limemnyima heshima ya maziko yaliyotukuka kwa sabab kitendo chake cha kuua na kujiua havitoi mfano mzuri klwa waumini.
 
Msijitaabishe Bure, Kuzikwa kikanisa, kuzikwa kidunia aijalishi chochote. Yesu alizikwa bila hata ya maombi na akafufuka akatupa ushindi mkubwa tu kwa kila mkiristo,,, La muhimu Mungu awe upande wako unapo kufa, hata ibada za kidunia zikikosa Utakuwa ni Mshindi, historia inaonyesha wanafiki< Wanga na wenye pesa Wanazikwa kwa maommbi na Mbwembwe kibaooo.
dah jamaa unatisha wewe! wengine wanazikwa na jeneza lenye remote
 
ni kawaida mtu aliyejitoa uhai huwa hafanyiwi ibada kanisani,ukijinyonga,unywe sumu au ujiue kwa namna yoyote ile sahau uwepo wa kasisi au kupelekwa kanisani

Yesu alikuja kuhudumia wenye dhambi lakini makanisa yetu yamekuja kuhudumia watakatifu hasa wale wenye fedha na madaraka
 
Kufanya ibada kwa marehemu ni heshima kanisa linatoa kwamarehem na ndugu wa marehem. Ni namna ya kuwaonesha binadamu wengine kwamba ukiishi vizuri hapa duniani utapata heshima fulan. Ni sawa na kumtangaza mtu mtakatifu lengo ni kutaka watu waliobaki hapa duniani Waige matendo yake. Hayo mengine kwmba mungu anapokea sala zetu au la sio kazi yetu. Sisi wajibu wetu kusali mengine ni ya mungu. Kwa hiyo liangalieni swala la mushi km kinyimwa heshima ya maziko ya kikanisa na sio hukum. Kanisa halijamhukum bali limemnyima heshima ya maziko yaliyotukuka kwa sabab kitendo chake cha kuua na kujiua havitoi mfano mzuri klwa waumini.

Ni amri ya ngapi hiyo kati ya zile kumi; hekima ya kibinadamu si chochote mbele za mungu na kama ni kuiga matendo mema ni matendo ya Yesu pekee yawezayo kuwa njia na uzima na si kingine chochote
 
Sasa kanisa lina uthibitisho gani kama alijiua au aliuwawa wakati uchunguzi bado kukamilika!!? Huku ni kuchukua sheria mkononi!
Aliyechukua sheria mkononi ni kanisa au aliyejiua ndio kajichukulia sheria mkononi?

Kanisa lina sheria zake......halijazitunga wakati wa Mushi.
 
Weye msemaji wa Mungu? God in infinate wisdom, infinate mercy will do the right thing.

Narudia tena "tusikubaki kudanganywa na watumishi wanafiki" hakuna toba baada ya kufa,ingekuwa
tunatubu baada ya kufa YESU asingekuja duniani na kuteswa na kushinda ili sisi tupate wokovu kwa
kumkubali na kumpokea yeye ili atushindie dhambi,angetusubiri tukatubu hukohuko Mbinguni'Utakatifu
ni hapahapa duniani baada ya kufa ni hukumu.WAEBRANIA 9:27
 
Watu na wawazike wafu waho, yule aliingiliwa na shetani wa mauti akatenda lile kosa na wala sio yeye kama binadamu wamekataa kumsalia bule kwani hakuwa na dhambi wao ndio wenye makosa,kutwa kila Jpili wanawaombea viongozi wala rusha na mafisadi waendelee kudumu na kutunyonya

acha unafiki! kwa hiyo kila mtenda dhambi anamsingizia shetani, sasa ni nani atakayehukumiwa? hakuna ila shetani tu au sio!? basi binadamu tuna raha!
 
Ukiombewa unasamehewa dhambi? sasa watu si watakua wanafanya makosa maksudi wakijua kua wataombewa wasamehewe?
 
Yesu alikuja kuhudumia
wenye dhambi lakini makanisa yetu yamekuja kuhudumia watakatifu hasa
wale wenye fedha na madaraka

hao kanisa ni washenzi tu! nani amewapa mamlaka ya kuamua hatma ya maisha ya watu! ni mungu pekee anaweza kuamua
 
Nilijua tu lazima wafanye hivyo. Lakini hawajui kwamba ibada ni kwa ajili ya wale wanaomsikiliza maana wafu hawajui neno lolote kama kinavyosema kitabu cha Mhubiri.
 
Ktk akili zako za kibinaadam unaamini marehemu Mushi(Mungu amrehemu)alikosea au hakukosea????namaanisha kuua kisha kujiua sio kosa kwako/kulingana na imani yako!!?

Umejuaje Mushi aliua/kujiua?????? Kuna ripoti yyte ambayo ishatoka kuthibitisha hilo???? Uchunguzi wa polisi ushakamilika????? Au wote mnahukumu kwa kutumia stori za ufo?????
 
wanafki tuu utamuukumuje mtu kama muumini misa anaudhuria sadaka anatoa kwanini msimuombee

Ni taratibu tu za kuwafunza wanadamu pia kuwakumbusha kujiepusha na dhambi.mf mtu akizaa nje ya ndoa mtoto hatabatizwa mpaka wazazi watubu kwanza.
 
Marehemu Mushi aliyefanya mauaji ya mama wa mtangazaji wa ITV na kujeruhi kwa risasi na atimaye kujiua amezikwa bila huduma ya kikanisa.

Kanisa Katoliki parokia ya Uru imegoma kusalisha misa ya marehemu Mushi kutokana na mazingira ya kifo chake.

Familia ilitaka marehemu aombewe na kanisa ili asamehewe dhambi zake sababu atoaye hukumu ni Mungu si binadamu na ajuaye ukweli ni Mungu.

Lakin kanisa imekataa kusalisha ibada na Mushi amezikwa bila ibada.


kanisa limekosea, lingetumia nafasi kuhubiri waliofika kwa kukemea matendo ya Mushi kwa nguvu zote. Najiuliza wote wanaosaliwa huwa wanaenda mbinguni? Looooooo!
 
Ni taratibu tu za kuwafunza wanadamu pia kuwakumbusha kujiepusha na dhambi.mf mtu akizaa nje ya ndoa mtoto hatabatizwa mpaka wazazi watubu kwanza.

Dhambi ya wazazi ibebeshwe watoto? Luke 6 37 says ,Do not judge and you will not be judged ,do not condemn and you will not be condemned , forgive and you will be forgiven. The church has with haste jugded,condemned and failed to forgive Mushi. Mwenye Mungu atuepushe.
 
kanisa huwa linafanya ibada kwa wale wanaoshiriki imani husika, hasa wanaohudhuria kwenye jumuiya katika mahali wanapoishi. kabla ya kumwombea marehemu huwa wanatafuta uthibitisho kwanza kuona kwamba je marehemu aliuishi ukristo katika imani ile? kwa kuangalia mahudhurio kanisani na kwenye jumuiya, ubatizo wake na mengine. Hili huwa la kwanza kisha hayo mengine yanafuatia. Hivyo ni vyema kujua kanisa lilichukua uamuzi huo kwa kuangalia vithibitisho gani? Huwa hawafanyi ibada bila kuwa na uthibitisho wowote wa ukristo wa marehemu
 
sasa ilo si ni pigo kubwa kwa familia sababu inaondoa matumaini kabisa

Matumaini ya nini? Sala au mahubiri yo yote wakati wa mazishi siyo kwa ajili ya marehemu bali ni kwa ajili ya wale walio hai. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu kwa hiyo kama aliyekufa hakutengeneza mambo yake na Mungu kabla hajafa sala yoyote baada ya kufa haina impact kwa marehemu. Hakuna sala inayoweza kumwondoa mtu kuzimu na wala hakuna purgatory kulingana na Biblia takatifu.
 
Hapana. Yesu alimuombea Lazaro akiwa ameshafariki, na ndio sababu Martha alimuona Yesu alimuambi angefika mapema ndugu yake (Lazaro) asingekufa.

Lakini Yesu aliwambia kuwa Lazaro hajafa ila alikuwa amelala. Tujiulize nini kilicho jificha katika kauli hii ya Yesu. Haiewezekani kulala ikawa sawa na kufa.

Kabla hata ya kuangalia kujiua au kuuliwa, huyu situnaambiwa alikuwa mzazi mwenzake na mtangazaji. Sasa hakuna ndoa inayoitwa mzazi mwenzake katika ukristo. Hivyo tuna amini kabisa kanisa lilijiridhisha kabla ya kufanya uamuzi huu.
 
Back
Top Bottom