Tetesi: Kanisa la Gwajima kufunguliwa hivi karibuni

Tetesi: Kanisa la Gwajima kufunguliwa hivi karibuni

Gwaji sindano inamuingia Barabara. kenge mmoja anataka kujitwisha mzigo asiouweza. Hakuna Tena jutapeli watu.
Amewatapeli nini mkuu? Humuoni Mwamposa anayeuza kijiko kimoja cha mafuta ya upako kwa Tsh 1000? You can't be serious mkuu.
 
Kaka unajua kama wewe ni padre au sheikh lakini una makandokando yako unayofanya sirini kama vile kua na nyumba ndogo au kuwafanya wanawake kinyume na maumbile halafu mtu akuambie, usipofanya kitu fulani nitaweka mambo yako hadharani, lazima u panic ili kulinda heshma yako uliyo jijengea kwa muda mrefu..
Yeah! Asante kwa kunisaidia kumjibu huyu jamaa mkuu. Gwajima sio mtu wa kuchezea hata kidogo.
 
Kufuatia Askofu Dr Josephat Gwajima kutoa ultimatum ya siku 10 kwa kanisa lake kufunguliwa, taarifa za chinichini zinasema kwamba serikali, kupitia msajili wa vyama vya kijamii, iko mbioni kuandaa press conference kwa ajili ya kujiokoa na zahma ya bomu atakalolipua Gwajima ikiwa siku zitaisha kabla serikali haijafungua kanisa lake. Tukumbuke kuwa katika siku 10 alizotoa zimebaki 4 tu.

Huko serikalini ni patashika nguo kuchanika! Watu wanakimbizana usiku na mchana kuwahi deadline. Mkubwa mmoja amedokeza kwamba vigogo wanatupiana mpira kuhusu nani hasa ajitokeze hadharani kumjibu Gwajima, kuomba radhi na kisha kulifungua kanisa. Hata hivyo, kuna mwanapropaganda mmoja kutoka ndani ya chama na serikali ambaye amependekezwa kufanya hilo jukumu zito linaloogopwa na kila mtu.

"Hakikisha kabla siku hazijaisha kanisa la huyu Askofu liwe limefunguliwa". Alisikika kigogo mmoja akitoa maagizo aliyoyapokea kutoka juu.

MAONI YANGU
Kama kweli serikali ni sikio la kufa wangeacha wasifungue kanisa hili tuone kama bomu la Gwajima lingewaacha salama. Huyu Askofu sio muoga kama Polepole. Ikiwa serikali ingetia nta masikioni, yeye angeliamsha dude na kulipua kitu "paaaa!" bila kumuogopa mtu yeyote. Uzuri mtu anayemuamini na kumtegemea Mungu hana chochote anachokiogopa chini ya jua. Nashukuru serikali imesikia ushauri wa Gwajima na kutilia maanani kilio cha wafuasi wa kanisa la Ufufuo na Uzima wanaotangatanga huku na kule kama makinda ya ndege wakikosa mahali pa kumuabudia Mungu wao. Sasa kilio chao kimesikika na hivi punde watarejea kwenye madhabahu ya Ufufuo na Uzima kumuabudu na kumuimbia Bwana kama ilivyokuwa awali.
​
Hakuna serekali duniani inayokubali kuchimbwa mkwara na raia wake
 
Kwanza vibomu vya Polepole havina madhara yoyote. Gwajima akirusha bomu moja tu nchi inasambaratika!
Lakini kiukweli wamemuonea...

Mtu unazungumzia utekaji, watu wanakufungia kanisa, hii nchi imefikia sehemu mbaya sana... kibaya zaidi askofu ndie kaongea, mnafungia maelfu ya waTanzania uhuru wao wa kuabudu... mnawapiga na kuwaumiza...
 
Lakini kiukweli wamemuonea...

Mtu unazungumzia utekaji, watu wanakufungia kanisa, hii nchi imefikia sehemu mbaya sana... kibaya zaidi askofu ndie kaongea, mnafungia maelfu ya waTanzania uhuru wao wa kuabudu... mnawapiga na kuwaumiza...
Ni aibu sana kwa kweli mkuu. Taifa linaloabudu sanamu halitaki kuona makanisa yanastawi.
 
Kwa mtu muabudu sanamu ,kama wewe, huwezi kuamini hili jambo. Hata Nuhu alitukanwa sana wakati anajenga safina. Cha ajabu haohao waliokuwa wakimtukana ndio walilia kumuomba awafungulie milango baada ya gharika kuanza kurindima.
Washupaza shingo hata stori za Nuhu huwa wanaona chai. Kila kitu kinachosimama kwenye Haki wao huona ni chai.
 
Wakifungua kanisa watakua wametengeneza precedent.
Gwajima atatoa ultimatum nyingine Lissu aachiwe ndani ya siku tatu. Wakitekeleza na hilo ukiongeza na speech ya Slow x2 Leo usiku watakua wame surrender.
Kuanzia hapo Gwaji boy atawafanya kila anavyotaka.
Gwajima huwa ni nani kitu ambacho hawajui Gwajima hata mkutano mkuu wa CCM ana ushawishi mkubwa angalia kipindi kile uchaguzi wa NEC Kura alizopata nyingi sana
 
Back
Top Bottom