tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,195
- 27,807
Kufuatia Askofu Dr Josephat Gwajima kutoa ultimatum ya siku 10 kwa kanisa lake kufunguliwa, taarifa za chinichini zinasema kwamba serikali, kupitia msajili wa vyama vya kijamii, iko mbioni kuandaa press conference kwa ajili ya kujiokoa na zahma ya bomu atakalolipua Gwajima ikiwa siku zitaisha kabla serikali haijafungua kanisa lake. Tukumbuke kuwa katika siku 10 alizotoa zimebaki 4 tu.
Huko serikalini ni patashika nguo kuchanika! Watu wanakimbizana usiku na mchana kuwahi deadline. Mkubwa mmoja amedokeza kwamba vigogo wanatupiana mpira kuhusu nani hasa ajitokeze hadharani kumjibu Gwajima, kuomba radhi na kisha kulifungua kanisa. Hata hivyo, kuna mwanapropaganda mmoja kutoka ndani ya chama na serikali ambaye amependekezwa kufanya hilo jukumu zito linaloogopwa na kila mtu.
"Hakikisha kabla siku hazijaisha kanisa la huyu Askofu liwe limefunguliwa". Alisikika kigogo mmoja akitoa maagizo aliyoyapokea kutoka juu.
MAONI YANGU
Kama kweli serikali ni sikio la kufa wangeacha wasifungue kanisa hili tuone kama bomu la Gwajima lingewaacha salama. Huyu Askofu sio muoga kama Polepole. Ikiwa serikali ingetia nta masikioni, yeye angeliamsha dude na kulipua kitu "paaaa!" bila kumuogopa mtu yeyote. Uzuri mtu anayemuamini na kumtegemea Mungu hana chochote anachokiogopa chini ya jua. Nashukuru serikali imesikia ushauri wa Gwajima na kutilia maanani kilio cha wafuasi wa kanisa la Ufufuo na Uzima wanaotangatanga huku na kule kama makinda ya ndege wakikosa mahali pa kumuabudia Mungu wao. Sasa kilio chao kimesikika na hivi punde watarejea kwenye madhabahu ya Ufufuo na Uzima kumuabudu na kumuimbia Bwana kama ilivyokuwa awali.