GE2025 Kanisa Katoliki kuliombea Taifa kwa siku tisa

GE2025 Kanisa Katoliki kuliombea Taifa kwa siku tisa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruai'chi ameagiza katika Parokia zote na Asasi zote katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam ifanyike Novena ya siku tisa (9) kuomba Haki na Amani kuanzia Agosti 15 -23, 2025.

Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi Takatifu, Kusali Rozari Takatifu na kusali sala ya Kuiombea Tanzania kama iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Agizo hilo alilitoa awali Julai 7, 2025 katika Sherehe za Upadrisho katika Viwanja vya Msimbazi Center, la kuwa na Novena ya kuliombea Taifa Haki na Amani.

"Aidha, katika siku ya kilele cha Novena hiyo, yaani Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025, ambayo kwa Kanisa zima la Tanzania ndiyo siku ya kufunga na kukesha katika kusali kwa ajili ya kuomba Haki na Amani, sote tunaalikwa kufuata Ratiba iliyotolewa na Idara ya Kichungaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambayo inaelezea namna ya kufanya sala na mfungo huo ambao utaanza hiyo tarehe 23 Agosti kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikifuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu ikiambatana na vipindi mbalimbali vya sala, mafundisho, na ukimya, na kuhitimishwa Dominika tarehe 24 Agosti kwa adhimisho la Misa Takatifu kama inavyoelekezwa katika maelekezo yaliyotoka TEC."

View attachment 3436679
Wazee wa novena nawaaminia
 
sasaivi kila kanisa linapambana kutafuta dirisha ili chochote kikitokea waseme wao ndio waliomba. namaanisha ikiwa amani waseme wao waliomba, na Mungu akishuka kutetea wanaoonewa waseme wao ndio waliomba. hata hivyo nasapoti, tunatakiwa kumwomba Mungu aingilie kati, hatutaki fujo, hatutaki machafuko, na wakati huo huo hatuwataki wanaoteka na kuua na kuonea watu, Mungu tunaomba ashuke yeye mwenyewe afanye jambo kututetea na kuweka mambo sawa. hao watekaji wajue yupo Mungu mpenda haki na anayetetea wanyonge, mamake mdude, soka na wengine wasio na sauti wala mtetezi wajue Mungu ndiye mtetezi wao. maombo pekee ninayoweza kuomba ni haya, siwezi kuwa mnafiki kuomba maombi aina ingine.
 
Hii novena ya kuomba haki na Amani itajibiwa mapema sana,.
Baada ya hii novena Kuna jambo kubwa litatokea katika nchi hii haswa Kwa wale viongozi wasiopenda Haki katika uchaguzi.
Amen
Huu mwaka itajulikana nani ni Mungu
Sie tuna mwendo wa 40+ mpk 31 October tukamilishe 90 days
Nione watatobolea wapi
 
Amen
Huu mwaka itajulikana nani ni Mungu
Sie tuna mwendo wa 40+ mpk 31 October tukamilishe 90 days
Nione watatobolea wapi
Mnatumia vinywa hivyohivyo mnavyonyonyea nyuchi na kunuwia uchawi?!
 
sasaivi kila kanisa linapambana kutafuta dirisha ili chochote kikitokea waseme wao ndio waliomba. namaanisha ikiwa amani waseme wao waliomba, na Mungu akishuka kutetea wanaoonewa waseme wao ndio waliomba. hata hivyo nasapoti, tunatakiwa kumwomba Mungu aingilie kati, hatutaki fujo, hatutaki machafuko, na wakati huo huo hatuwataki wanaoteka na kuua na kuonea watu, Mungu tunaomba ashuke yeye mwenyewe afanye jambo kututetea na kuweka mambo sawa.
Nikwambie sio issue ya dhehebu ni issue ya kanisa la Tanzania,sshv watu waneungana sio km zamani
Ndo maana unaona ht Rc wanewapa ufufuo sehemu ya kuabudia

Tushatoka huko mkuu
 
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruai'chi ameagiza katika Parokia zote na Asasi zote katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam ifanyike Novena ya siku tisa (9) kuomba Haki na Amani kuanzia Agosti 15 -23, 2025.

Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi Takatifu, Kusali Rozari Takatifu na kusali sala ya Kuiombea Tanzania kama iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Agizo hilo alilitoa awali Julai 7, 2025 katika Sherehe za Upadrisho katika Viwanja vya Msimbazi Center, la kuwa na Novena ya kuliombea Taifa Haki na Amani.

"Aidha, katika siku ya kilele cha Novena hiyo, yaani Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025, ambayo kwa Kanisa zima la Tanzania ndiyo siku ya kufunga na kukesha katika kusali kwa ajili ya kuomba Haki na Amani, sote tunaalikwa kufuata Ratiba iliyotolewa na Idara ya Kichungaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambayo inaelezea namna ya kufanya sala na mfungo huo ambao utaanza hiyo tarehe 23 Agosti kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikifuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu ikiambatana na vipindi mbalimbali vya sala, mafundisho, na ukimya, na kuhitimishwa Dominika tarehe 24 Agosti kwa adhimisho la Misa Takatifu kama inavyoelekezwa katika maelekezo yaliyotoka TEC."

View attachment 3436679

Asante kwa taarifa. Ntawaunga mkono TEC.

Vita yetu sio ya nyama kwa nyama. Ni vita ya kiroho.

Ni Mwenyezi Mungu pekee mwenye nguvu na uwezo wa kutunusuru.

Tulipo tumekwama. Tumejaa kiburi na hadaa. Tumekuwa waongo mno. Tunaona sawa kutumia hata mali za wanyonge kwenye starehe zetu na ubinafsi.

Ni Mwenyezi Mungu pekee mwenye nguvu za kuliponya Taifa letu.

Na namuomba sana amsambaratishe Mzee Kisebengo na vibwengo vyake. 😂😂😂😂
 
Nikwambie sio issue ya dhehebu ni issue ya kanisa la Tanzania,sshv watu waneungana sio km zamani
Ndo maana unaona ht Rc wanewapa ufufuo sehemu ya kuabudia

Tushatoka huko mkuu
watu wengi wanaamini gwajima alikuwa na bifu na katoliki, kumbe sio, alikuwa na personal bifu na "pengo'' ambaye alikuwa rafiki wa magu, na akatoa ushauri kwamba "ni bora wachache wafe kuliko wengi" akimaanisha taifa. RC awali walidhani wapo salama, walipoanza kufuatwa maaskofu na wasiojulikana wakaona kumbe na sisi hatupo salama, alipovamiwa kitima kanisani wakaona kumbe hatupo salama kama wengine. pengo awali alidhani yupo salama akiwa na rais, ila sasaivi wamestuka. hata hivyo, ilishawahi kutabiriwa, kuna siku wakristo hata kama hawataungana kuamini mlengo mmoja ila watakuwa kitu kimoja. wakristo wanapaswa kuungana au la makanisa tu ndio yatavamiwa na kutekana na kufungwa ila misikiti hutosikia imeguswa. sisi vita vyetu sio vya kupigana kwa mikono tutamwomba Mungu ila umoja ili kuwa na sauti moja walau ya kulalamika ni muhimu. washukuruwe RC kuona wakristo wengine nao ni wenzao tu kwa sababu pengine sote tumekuwa victims.
 
Mama ajiangalie
Unaota wewe kuna kitengo cha dini TISS

Msibabsishe watu na ushetani wenu huo wa kutishia na maombi na visala vyenu na vinabii koko

Watu wamesoma dini kuliko nyinyi

Na wanajua Mungu kuliko nyie .Hukesha wakiombea nchi masaa 24 miaka yote ya ajira zao nchi iwe na amani.Sio hivyo vi
Novena vyenu vya kusitukiza au vi unabii vya kutishia nyau
 
Mimi sio mkatoliki lakini nitashiriki maombi haya ya kuombea nchi. Lazima tuangushe ngome ktk ulimwengu wa roho ili Ufalme wa Mungu utawale Tanzania. Ufalme wa Mungu ni "Haki, Amani na Furaha katika Roho Mtakatifu" Rumi 14:17.
 
Acheni upuuzi, acheni ushirikina wenu wa kipuuzi. Sijawahi kuona RC wakiomba na kupata matokeo yoyote wao kila kitu ni km utamaduni tu.
Unafikiri hawa watu wanaotawala dunia miaka 2000 sasa hawapati matokeo yoyote? Unafikiri ni makanisa gani wanapata matokeo kwenye dunia hii? Nitajie na mifano hata ya kidunia tu.
 
Back
Top Bottom