GE2025 Kanisa Katoliki kuliombea Taifa kwa siku tisa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,853
Reaction score
3,098
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruai'chi ameagiza katika Parokia zote na Asasi zote katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam ifanyike Novena ya siku tisa (9) kuomba Haki na Amani kuanzia Agosti 15 -23, 2025.

Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi Takatifu, Kusali Rozari Takatifu na kusali sala ya Kuiombea Tanzania kama iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Agizo hilo alilitoa awali Julai 7, 2025 katika Sherehe za Upadrisho katika Viwanja vya Msimbazi Center, la kuwa na Novena ya kuliombea Taifa Haki na Amani.

"Aidha, katika siku ya kilele cha Novena hiyo, yaani Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025, ambayo kwa Kanisa zima la Tanzania ndiyo siku ya kufunga na kukesha katika kusali kwa ajili ya kuomba Haki na Amani, sote tunaalikwa kufuata Ratiba iliyotolewa na Idara ya Kichungaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambayo inaelezea namna ya kufanya sala na mfungo huo ambao utaanza hiyo tarehe 23 Agosti kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikifuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu ikiambatana na vipindi mbalimbali vya sala, mafundisho, na ukimya, na kuhitimishwa Dominika tarehe 24 Agosti kwa adhimisho la Misa Takatifu kama inavyoelekezwa katika maelekezo yaliyotoka TEC."

Screenshot_20250809_140459_All PDF Reader.jpg
 
View attachment 3436679
Tunasubiri matokeo kwa hamu kubwa!
 
Back
Top Bottom