GE2025 Kanisa Katoliki kuliombea Taifa kwa siku tisa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruai'chi ameagiza katika Parokia zote na Asasi zote katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam ifanyike Novena ya siku tisa (9) kuomba Haki na Amani kuanzia Agosti 15 -23, 2025.

Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi Takatifu, Kusali Rozari Takatifu na kusali sala ya Kuiombea Tanzania kama iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Agizo hilo alilitoa awali Julai 7, 2025 katika Sherehe za Upadrisho katika Viwanja vya Msimbazi Center, la kuwa na Novena ya kuliombea Taifa Haki na Amani.

"Aidha, katika siku ya kilele cha Novena hiyo, yaani Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025, ambayo kwa Kanisa zima la Tanzania ndiyo siku ya kufunga na kukesha katika kusali kwa ajili ya kuomba Haki na Amani, sote tunaalikwa kufuata Ratiba iliyotolewa na Idara ya Kichungaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambayo inaelezea namna ya kufanya sala na mfungo huo ambao utaanza hiyo tarehe 23 Agosti kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikifuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu ikiambatana na vipindi mbalimbali vya sala, mafundisho, na ukimya, na kuhitimishwa Dominika tarehe 24 Agosti kwa adhimisho la Misa Takatifu kama inavyoelekezwa katika maelekezo yaliyotoka TEC."

View attachment 3436679
Asante kwa taarifa. Tutashiriki kwa uaminifu na Mungu atajibu kwa wakati.
 
Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi
Aisee hayo maombi hatafiki popote
Yaani badala ya kuabudu Mungu wakatoliki mnaenda kuabudu Ekaristi

Biblia imeagiza kuabudu Mungu tu

Aiseeee upagani mtupu
 
Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi
Yaani Askofu anaahiza siku zote hizo badala ya watu kuabudu Mungu anaagiza waabudu kamkate ka ekaristi kalikopikwa jikoni na binadamu
 
Hii novena ya kuomba haki na Amani itajibiwa mapema sana,.
Baada ya hii novena Kuna jambo kubwa litatokea katika nchi hii haswa Kwa wale viongozi wasiopenda Haki katika uchaguzi.
museveni, kagame, lukashenko ,netanyahu na wadau wao wengine wote bado wapo madarakani
 
Mhashamu katoa agizo muhimu. Kuiombea nchi amani na haki na kuinginga na wanaotaka kuleta mtafaruko.
Uhuru, amani na umoja
 
Na waromani kumbe nao siku hz wanakesha Kama walokole.
 
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruai'chi ameagiza katika Parokia zote na Asasi zote katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam ifanyike Novena ya siku tisa (9) kuomba Haki na Amani kuanzia Agosti 15 -23, 2025.

Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi Takatifu, Kusali Rozari Takatifu na kusali sala ya Kuiombea Tanzania kama iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Agizo hilo alilitoa awali Julai 7, 2025 katika Sherehe za Upadrisho katika Viwanja vya Msimbazi Center, la kuwa na Novena ya kuliombea Taifa Haki na Amani.

"Aidha, katika siku ya kilele cha Novena hiyo, yaani Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025, ambayo kwa Kanisa zima la Tanzania ndiyo siku ya kufunga na kukesha katika kusali kwa ajili ya kuomba Haki na Amani, sote tunaalikwa kufuata Ratiba iliyotolewa na Idara ya Kichungaji ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambayo inaelezea namna ya kufanya sala na mfungo huo ambao utaanza hiyo tarehe 23 Agosti kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikifuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu ikiambatana na vipindi mbalimbali vya sala, mafundisho, na ukimya, na kuhitimishwa Dominika tarehe 24 Agosti kwa adhimisho la Misa Takatifu kama inavyoelekezwa katika maelekezo yaliyotoka TEC."

View attachment 3436679
Unaweza kudhani hawatembei na wake za waumini wao
 
Back
Top Bottom