Kamwe usithubutu kutafuta maisha mikoani, utakosa hadi nauli ya kurudi Dar!

Objective football

JF-Expert Member
Oct 21, 2023
1,196
2,758
Bora msema kweli kuliko kuwa mnafiki. Kijana unaye jitafuta usije jaribu kufungasha mizigo kwenda kutafuta maisha huko mikoani, watu wa mikoani ni wabinafsi, roho mbaya, majungu na fitna.

Kijana ukiwa Dar una 85% za kutoboa hapa town, kapuku muuza maji leo mtafute baada muda utamkuta mbali sana, kikubwa creativity na flexibility tu kwenye kazi.

Dar ni hub ya domestic and multilateral companies zote hapa nchini, so fursa yoyote iwe vibarua ajira inaanzia hapa.

Soko la mazao ya wakulima wote wa huko mikoani mwao lipo hapa Dar, infrastructure facilities zote zipo hapa town.

NB: Ukitaka ufubae na uchakae vibaya kajichanganye huko mikoani kwakina Mwakarobo, Mabula Mabele nk, uone utakavyo pigwa vimbola.
 
Back
Top Bottom