Kampuni ya utalii yapigwa faini kwa kuwaruhusu Watalii kula hadharani Zanzibar

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,938
Kamisheni ya Utalii Zanzibar imethibitisha kuipiga faini ya dola 500 kampuni ya utalii ya Organisateur Francophone Tours and Travel kwa kuruhusu watalii kula hadharani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Katika taarifa Afisa wa Uhusiano wa Tume ya Utalii Zanzibar Mohamed Nassor Bajuni alisema kampuni hiyo ilikiuka miongozo na maagizo yaliyotolewa kwa wafanyabiashara wa utalii wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.

''Toka kuanzishwa kwa kamisheni huo tunatoa notisi maalumu kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani kuhusiana na suala hili'' alisema Bw.

Muongoza watalii wa kampuni hiyo, Khamis M. Kahogo pia amezuiliwa kufanya shughuli zozote za utalii kwa muda wa miezi mitatu," aliongeza kusema.

Kamisheni hiyo imesisitiza umuhimu wa kufuata desturi na mila za visiwa vya Zanziba hasa wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.

Pia soma:
Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Sio sawa kung'ang'ania kula hadharani Zanzibar huku unapinga haki nyingine binafsi za wengine
 
Imani na matendo ya imani kwa Mungu wa kweli haihitaji kutumia nguvu za kimwili. Kufunga kwa ajili ya mambo ya kiroho kunahitajika imani na uvumilivu. Ni kujizuia kula kwa muda uliopanga wewe binafsi au kupangwa na dini au madhehebu yako. Haijalishi utakiona chakula mbele yako au utamwona mtu akila mbele yako. Wala hutakiwi kumshutumu au kumlaumu anayekula, kwani yeye hiyo funga haimhusu, inakusuhu wewe. Unachotakiwa ni kuonyesha ukomavu wako wa imani, kwamba pamoja na kusikia harufu nzuri ya chakula au kukiona chakula mbele yako, kamwe hutashawishika kutamani kula. Unatakiwa ushinde hilo jaribu.

Mimi nikiamua kufunga hamu ya chakula huwa inapotea kabisa, hata nikimwona mtu anakula siwezi kukwazika au kutamani kula kwa namna yoyote hadi nimalize funga yangu.
 
Biblia inasema ikimbieni zinaa. Sasa unakuta haohao wanaofunga ni wazinzi na waasherati waliokubuhu. Chakula unashindwa kukivumilia pale ambapo mmoja kafunga na mwingine hajafunga? Sasa mnataka tuamini kuwa waislamu wa Bara na zanzibari ni tofauti kabisa. Hawa wa Bara wako madhubuti kwa kuwa wana uvumilivu. Hawa wa visiwani ni rojorojo sana kiasi hawawezi dhibiti hisia zao hadi wawekewe miundombinu ya kufanya hivyo.
 
Kamisheni ya Utalii Zanzibar imethibitisha kuipiga faini ya dola 500 kampuni ya utalii ya Organisateur Francophone Tours and Travel kwa kuruhusu watalii kula hadharani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Katika taarifa Afisa wa Uhusiano wa Tume ya Utalii Zanzibar Mohamed Nassor Bajuni alisema kampuni hiyo ilikiuka miongozo na maagizo yaliyotolewa kwa wafanyabiashara wa utalii wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.

''Toka kuanzishwa kwa kamisheni huo tunatoa notisi maalumu kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani kuhusiana na suala hili'' alisema Bw.

Muongoza watalii wa kampuni hiyo, Khamis M. Kahogo pia amezuiliwa kufanya shughuli zozote za utalii kwa muda wa miezi mitatu," aliongeza kusema.

Kamisheni hiyo imesisitiza umuhimu wa kufuata desturi na mila za visiwa vya Zanziba hasa wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.
Huu ubaguzi
 
Kama wameanza huu utaratibu kwa watalii wazungu watakimbia maana vyakula vya wazungu ni bites na juisi ambazo mara nyingi huliwa hadharani
 
Sasa hivi sio polisi chombo cha muungano chini ya katiba ya muungano tena kukamata wala chakula mchana nashukuru polisi Zanzibar kujivua hilo jukumu la kamata wala chakula mchana wameachia hiyo kamisheni ndio wajijue impact yake kwa hatua zao badala ya kulitwika jeshi la polisi zigo mwisho wa siku

Zanzibar kila taasisi ibebe zigo lake

Polisi muungano huo mziki kaeni nao mbali ili hata kesi za katiba zikija msije bebeshwa zigo jumba bovu likawaangukia puuuuuu na IGP wenu

Kila mtu apambane na hali yake asitupie zigo kwa mwingine
 
Kwa watu wanaojitambua, unaweza kukuta mama amefunga siku nzima, anawapikia familia yake chakula ila yeye hata hashiriki kula..

Hawa wanaotaka kusaidiwa na polisi kufunga hawamaanishi kumuabudu huyo allah.

polisi tanzania nao wanatumika vibaya, wanavunja Katiba ya nchi kukamata watu wanaokula, labda tu kama hicho chakula wamekiiba. Hakuna sheria iliyo juu ya Katiba, so hiyo sheria yao ni batili.
Ingefaa polisi wafafanue hili suala
 
Kama wameanza huu utaratibu kwa watalii wazungu watakimbia maana vyakula vya wazungu ni bites na juisi ambazo mara nyingi huliwa hadharani
Mimi nashukuru safari hii polisi hawajatupiwa hilo zigo la kukamata hao watalii wazungu wala chakula mchana polisi chombo cha muungano kinachoongozwa na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Zigo lao wameamua wabebebe wenyewe v
badala ya kufanya polisi kama jalala la kutupa uchafu wao au devil hadi kupelekea Polisi Zanzibar wavunje katiba ya muungano
 
Back
Top Bottom