Sio sawa kung'ang'ania kula hadharani Zanzibar huku unapinga haki nyingine binafsi za wengine

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,660
46,349
Unaweza kukuta wengi wa raia wanaong'ang'ania au kukomaa kula hadharani huko Zanzibar kipindi hiki cha mfungo ndio hao pia wanaounga mkono manyanyaso, usumbufu na bugdha kwa wanawake wanaovaa nguo fupi za kubana Kariakoo au mitaani kwao!

Kigezo watakachotumia kuunga mkono usumbufu wa wahuni kwa wadada wanaovaa nguo hizo fupi au ndogo itakuwa ni hicho hicho cha "utamaduni wetu"!

Tusiwe na ndimi mbili au double standards katika haki binafsi za watu. Kama hukubaliani na utaratibu wa kunyimwa haki yako ya kula hadharani Zanzibar kipindi hiki kwa kigezo cha utamaduni wa huko basi pia usiunge mkono udhalilishaji au usumbufu kwa wanawake wanaovaa nguo fupi za kubana na kupita nazo Kariakoo.
 
Msaada please kwa alie elewa
GJiV0HoXsAA1Rk3.jpeg
 
Back
Top Bottom