KERO Kampuni Ya Mabasi ABC upper class Mnakera Sana

KERO Kampuni Ya Mabasi ABC upper class Mnakera Sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nina mpango wa kuwafungulia mashtaka. wamenikatia tiketi ya kieletronic nikatumiwa ujumbe kwenye simu kwa SMS bahati mbaya sikusoma SMS yote. Nimefika Dar napeleka madai kwa muhindi wangu ili anirudishie nauli yangu nakuta nauli imeandikwa TBR to Dar shs 100 (Mia moja) . Muhindi kagoma kunirudishia 50,000 niliyolipa akidai tiketi inaonyesha nimelipa sh 100.Nimeshaenda Latra wameniambia niende kesho. Shenzi sana hawa
Hahhahah nimecheka sana mkuu, sasa kwanini hukusoma sms yote? kwahiyo mwajiri nae amekomaa nauli ni sh 100, halafu sikujua kabla ABC wana gari Tabora-Dsm?.
 
Kuna siku nimekata tiketi safari ya tunduma gari ya saa moja nafika manzese gari haijafika abiria tunaambiwa gari ipo garage matokeo yake tumepanda gari gari iliyotoka singida imewashusha abiria hapo hapo tumeambiwa wale wa tunduma mtapanda gari hii na safari ikaanza saa tatu kasoro. Hili tatizo kumbe bado wanalo
 
Siku zote ambazo nimesafiri nao usiku, siku zilikuwa mbaya

Last week wametuweka manzese mpaka saa sita kasoro, wakati gari ilitakiwa kuondoka saa 4

Unafika moro hotelin saa nane, noo food no anything yet wanaenda kuweka mafuta tunakaa tena Pale 45mn
Nimesafiri nao sana huu uzembe sijui wameanza lini, kwanini wasiweke mafuta ya safari nzima? maana Dar-Moro ni distance fupi sana kuongeza mafuta au wana kituo chao cha mafuta hapo, Singida-Dar nimetoka nao mara nyingi usiku na mchana pia.
 
Napenda basi linalosimama kuanzia 30minutes wakati wa kula au mapumziko. Sio mnakula juu juu dakima kumi tu. Kilimanjaro pia Wana utaratibu huo.
Mkuu sasa umetoka Dar saa 4 usiku, bado unahitaji kula tena wakati Iringa utafika saa 12 asubuhi?😄😄 Unakula saa 7 usiku si kujiongezea tu mavitambi yasiyo na msingi
 
Nimesafiri nao sana huu uzembe sijui wameanza lini, kwanini wasiweke mafuta ya safari nzima? maana Dar-Moro ni distance fupi sana kuongeza mafuta au wana kituo chao cha mafuta hapo, Singida-Dar nimetoka nao mara nyingi usiku na mchana pia.

Wanakituo chao cha mafuta pale cate hotel
 
Mkuu sasa umetoka Dar saa 4 usiku, bado unahitaji kula tena wakati Iringa utafika saa 12 asubuhi?😄😄 Unakula saa 7 usiku si kujiongezea tu mavitambi yasiyo na msingi

Gari linapaswa kuondoka saa 4, but linaondoka saa sita kasoro, tunafika moro saa tisa, pale hotelin hakuna ishu yoyote ya kufanya kwa muda huo, watu wangechimba dawa na kuondoka, sasa wanashusha watu then wanaenda kuweka mafuta 45mn abiria wanapigwa na baridi tu nje
 
Mimi pale huwa wananiboa kulazimisha abiria wote tushuke kwenye basi
 
Back
Top Bottom