Ituzaingo Argentina
JF-Expert Member
- Jun 20, 2020
- 1,870
- 2,176
Nimekuwa mpenzi wa kutumia usafiri wa basi la Shabiby mimi na familia yangu kwa miaka zaidi ya mitano
Dar, Dodoma, Dodoma Arusha.
Ila leo kwa yaliyo nikuta kupitia dereva huyu, imeniuma sana
Tulikata tiketi siti namba 4 kwa ajili ya mke wangu kusafiri toka Arusha kuelekea Dodoma ni katika basi linalo wasili Arusha saa nne asubuhi ili kuelekea Dodoma.
Katika pilikapilika za safari nikajikuta nimesahau kadi yangu ya benki ambayo nilidhamiria kuitumia kutoa pesa ili kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani na hii ndio ikawa sababu kwa mimi kukutana na maumivu niliyoyapata kwa dereva nisiye mfahamu jina lake ila ndiye dereva wa basi tulilo kata tiketi hii,yaani basi la Shabiby.
Kutokana na kusahau kadi ya benki nililazimika kumuacha ndani ya gari mke wangu ambaye nilikuwa nikimsindikiza kutafuta namna nyingine ya kupata pesa ili nimpe ya kula njiani,
Baada ya kufanikiwa nikarejea ndani ya gari, kwa lengo la kumpa hiyo pesa mke wangu,ndipo dereva huyu wa shabiby baada ya kuona kuwa mkononi mwangu nimeshika speaker ndogo ambayo huwa naitumia kwa ujasiliamali ,yeye akahisi labda naingia kuuza bidhaa fulani
Hata hivyo kwa upole nilimweleza kuwa, mimi siingi kuuza ila lengo langu ni kumpa mke wangu pesa ya matumizi njiani.
Kilicho niumiza, bado aliendelea kuni zuia kibabe
Hakuishia hapo tu alinikunja huku kondakta wake akinivuta mguu kwa nje,mbele za mke wangu,abiria na watu wengine,kiukweli nimedhslilishwa,naamini kosa langu ni kuutumia usafiri wa shabiby kumsafirisha mke wangu,halafu kuamua kumletea pesa ya matumizi mke wangu.
Kweli nimejaribu kumwelezea mtu niliye fahamishwa kuwa ni kiongozi wake hata sijaridhishwa na namna alivyoshughulikia kudhalilishwa kwangu,kiukweli nimeamua,maana mimi huwa hakuna aina ya biashara mbayo huwa naifanya ndani ya mabasi,zaidi ya leo kumsindikiza mke wangu.
Kweli,kama kampuni ya mabasi ya shabiby haita muwajibisha huyu,aliye nikunja hata kunitishia kunipiga,kisa,nimemweleza kuwa nampa mke wangu pesa ya matumizi njiani, basi kwa mimi binafsi na familia yangu nitafikiria kuto penda kuutukimia usafiri huu kwa mara nyingine,maana nimeaibishwa sana.
Nimejaribu kutafuta mawasiliano ya kampuni ya basi la shabiby makao makuu ili kutoa taarifa ya kero hii, ila sijatambua namna ya kuwapata,ndio maana nimeandika hapa ili wahusika wapatapo ujumbe angalau walishughulikie hili kama wana upendo na wateja wao,tafadhali wasilifumbie macho
Muda huu basi hilo bado lipo njiani kuelekea dodoma, mke wangu niliye msafirisha anaitwa Silvero Mwacha ,yupo sit namba 4, tafadhali wahusika popote mlipo nimekereka, naomba msilifumbie macho hili.
Ni mimi Emmamuel.
Pole sana mkuu