Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 187
- 334
Sisi abiria tunaosafiri na Basi la Kampuni ya Shabiby kati ya Dodoma na Dar es Salaam tunayo malalamiko yetu makubwa kutokana na huduma mbovu mjini Morogoro ambapo basi la Shabiby husimama kwa ajili ya huduma ya chakula na kuchimba dawa.
Mazingira ya hoteli hiyo ni machafu sana na hayaendani na hadhi ya basi la Shabiby ambalo abiria tunalipa nauli 30,000 hadi 45,000 Dar- Dom.
Tumelalamika sana kwenye basi hadi inafikia baadhi ya abiria wanashindwa kushuka kupata chakula kutokana na mazingira kutoridhisha na uchafu wa vyoo lakini hatusikilizwi
Tumeona tulete malalamiko hapa tukiamini uongozi wa juu ya Kampuni ya Shabiby utasikia malalamiko yetu maana hakuna box la maoni ya abiria kwenye basi.
Ni Sisi Abiria watiifu wa Kampuni ya Shabiby
Kutoka Dar-Dom