KERO Utingo wa Basi la kampuni ya Dolphin Express (njia ya Dodoma-Arusha/Moshi) ndio kinara wa kuibia abiria

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,152
Kama ulikuwa hujui hilo basi sasa anza kuchukua tahadhari mapema. Ama usipande kabisa hilo basi au ukipanda huku ukikaa kwa tahadhari kubwa sana, maana utingo wa basi ndio mastermind.

Kampuni ya mabasi ya Dolphin Express kwa sasa huenda ndio inaongoza kuwa na makondakta (utingo) wezi wa mali za abiria katika njia ya Dodoma-Arusha/Moshi. Kama sio pesa zako, basi pochi(wallet) yako, simu yako, laptop yako au kitu chako chochote cha thamani kinaweza kuibiwa na mhusika mkuu akawa utingo wa basi.

Mchezo uko hivi. Utingo wa basi anapopata wasaa mzuri wa kuwafahamu abiria wake wana kitu gani cha thamani, yeye huchonga ramani ya wizi ili kuhakikisha abiria huyo anaibiwa na kusiwepo nafasi ya kumdai yoyote. Na kwa kuwa mizigo na mali za abiria wa ndani ya basi sio dhamana yao, utingo hatatoa ushirikiano wowote wa abiria kupata mali yake inapoibiwa. Yote tisa, usipoibiwa ndani ya basi huenda ukaibiwa utakashuka kwenye basi.

Ukiachana na hilo, utingo hutumia mwanya wa kuwaibia pesa zao za nauli abiria wanaopanda njiani kwa kuwaruka kuwa hawajamlipa nauli (maana abiria wa njiani mara nyingi hawapewi tiketi), kutokomea na chenji zao, kupoteza mizigo yao na kuwakana kuwa hawakupanda na mizigo yao.

Bahati mbaya sana michezo karibu yote hiyo huchezwa zaidi na utingo mmoja hivi (kijana wa makamo, mjanja mjanja wa maneno, mwembamba kiasi, mrefu, mwenye ndevu kiasi na akiongea kwa lafidhi ya kaskazini (mchaga? Mmeru? Muarusha?) mara ya mwisho kuonekana kwenye basi ni leo jumamosi (17/2/2024) akitokea Dodoma kuja Arusha/Moshi. Na siku akiwepo huyo kondakta ni lazima kuna abiria watakuwa wamelizwa tu.

Mwanzoni nilipuuzia hizo habari kwa kuwa nilidhani hazinihusu lakini baada ya jamaa yangu wa karibu kupigwa tukio imebidi nitoe tahadhari kwa watu wote.

Wamiliki wa kampuni ya Dophin Express nawaomba mchunguze hilo na ikiwezekana kuchukua hatua mapema. Msikubali kuendelea kufuga wezi kwenye kampuni yenu.
 
Kumbe matingo wapo seriously hivi
 
Kongole kwako ndugu mleta uzi.
Naomba nikiri kuwa nami ni mdau wa usafirishaji.

Umefanya jambo jema sana kuleta hili suala hapa JF, na nawaomba wengine mnaokutana na changamoto kwenye usafiri mulete humu ili zishughulikiwe kwa uharaka na umakini.

Kongole kwa wote wanaotoa kero hapa, maana traffic police, LATRA na LATRA CC hawana msaada.
 
Gari zenyewe hizi hupata abiria baada ya zile gari zenye customer care nzuri kujaa lakini bado wanafanya madudu.

Hili gari leo ndio nimelisikia.
 
Back
Top Bottom